Umeme Ruangwa ni shida

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,596
8,878
Wakuu, habari zenu.

Nimekuja one time kibiashara jimboni kwa PM ajabu toka nimefika naona umeme ni shida mno wenyeji wanasema ni kawaida sasa hata kwa Waziri Mkuu umeme haueleweki?

Nashauri wahusika wachukuliwe hatua kikawaida ni haki ya mteja kujulishwa katizo au tatizo lolote lililopelekea umeme kukatika.

Anyway niwaache na majanga yenu nirudi kwetu A TOWN
 
Yani katika jimbo ambalo liko hovyo na linatia aibu ni hilo jimbo la mkuu majaliwa, hapo maji ni utata mtupu, barabara hakuna lami, UMEME NDIO MAJANGA inapita siku moja hadi mbili umeme hakuna. yaani kajimbo kadogo TANESCO RUANGWA IFUMULIWE AISEE NI UOZO MTUPU.
 
Kila kitu kitu kitakuwa shwari Ombi letu la Ongezeko likipitishwa na Ewura.Tutakuwa na Ari ya Kufanya kazi zaidi.Kuwa mvumilivu.
 
Hili jimbo ni la hovyo sana pm sijui akifika anakuja kufanya nini mana kila akifika ndiyo kama anakuja kuongeza matatizo.
 
Hahaaa! machoni kama watu moyoni hawana utu, yaani hata kwake?! sitimbi ndio basi tena.
 
Yani kama Fundi feniture tu anawatengezea vitanda watu lakini mweyewe analala kwenye kitanda cha kamba
Afadhali hata fundi furniture anaweza sema anatimiza utamaduni wa kwao, sasa huyu kama yeye hautaki nyumbani kwake si awawekee wanaouhitaji?! Wacha waisome namba saa hizi PM yuko anakagua uwezo wa mitambo ya umeme Dodoma.
 
Hili jimbo ni la hovyo sana pm sijui akifika anakuja kufanya nini mana kila akifika ndiyo kama anakuja kuongeza matatizo.
Ila mkuu hilo jimbo kwa tatizo la umeme kwa mimi naona kama ni trela tu,picha yenyewe ni tatizo la barabara ukazunguuke hadi Nanganga,wakati naambiwa kuna njia ya mkato ikitengenezwa hiyo mtu anayeenda Lindi mjini na wewe wa Ruangwa mtafika kama sio muda sawa basi mtapishana kwa robo saa au nusu saa,wakati sasa hivi unafika Lindi mjini saa 6,lakini Ruangwa utafika kama sio 11 basi 12.
 
kwani solar hamtumii sikuhizi?
masasi vijijini njia ya newala umeme upo
ila wananchi wamezoea solar sana
 
Back
Top Bottom