Umeme Jua naitambulisha PREMIER ELECTRICS

Umeme Jua naitambulisha PREMIER ELECTRICS

Hongera mkuu kwa kujikwamua na kutengeneza nafasi za ajira kwa waTz wenzako pia. Kama ZeMarcopolo alivyosema jitahidini sana kuzitambua bidhaa halisi na zile feki ili katika kazi zenu muwe makini na muwe na msimamo wa dhati kuwa hamtatumia bidhaa feki kwa kazi yeyote. Vilevile uadilifu na uaminifu ni vitu cha muhimu sana. Mnapochukua kazi ya mteja fanyeni kama ni kazi yenu wenyewe bila kuchakachua kwa namna yoyote ile. Hii itawajengea jina zuri kwa jamii hivyo kuwavutia watu wengi. Trust me, mtaanza kidogo kidogo na hatimaye mtakuwa na kampuni kubwa ambalo mnaweza kuwa na link ya moja kwa moja na makampuni yanayotengeza bidhaa za ubora kutoka katika nchi zinazoaminika kwa viwango kama vile Ujerumani, Uingereza, Sweden, Marekani etc. Nawatakia kila la heri.
ZeMarcopolo upo, lete issues
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wanajamii,
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa jamiiforums hususani jukwaa la Uchumi na Biashara kwa muda mrefu. Mada mbalimbali kuhusu biashara, uchumi, kilimo, ufugaji na ujasiriamali kwa ujumla nilizifurahia na kuzipenda sana na hivyo nami nikashawishika kuanzisha kampuni ya ukandarasi wa umeme.

Hivyo leo nawatambulisha rasmi PREMIER ELECTRICS, kampuni ya ukandarasi umeme (electrical contractor) iliyosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (Contractors Registration Board-CRB) katika kiwango cha daraja la 6 (class 6).

PREMIER ELECTRICS inajihusisha na ufungaji wa umeme wa MAJUMBANI, MAJENGO YA BIASHARA na VIWANDANI na vilevile matengenezo (maintenance) ya mifumo ya umeme (electrical systems).

Kwa mawasiliano zaidi,
Ofisi: Stanford House, Tangi Bovu, Mbezi Beach,
S.L.P 13162 Dar es salaam, Tanzania.
Simu: (+255) 0715 050539/0766705332/0714693754/0614435355.
Barua pepe: premier-electrics@hotmail.com.

Karibuni wadau mfurahie huduma zetu.

Asanteni sana, pamoja sana.
Karibuni sana
 
Back
Top Bottom