Umeme Haukatiki. Nini Kimefanyika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme Haukatiki. Nini Kimefanyika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Mar 25, 2011.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Ninahitaji sana huduma ya umeme. Na ninafurahia sana kukiwa na umeme nyumbani, pahala pa kazi n.k. Ninafarajika kwa kuwa ninahisi mimi kama mtu binafsi mambo yangu yatakwenda sawa, lakini pia kama mwananchi wa Tanzania, ninahisi taifa langu litapiga hatua kimaendeleo kupitia uzalishaji katika viwanda, masomo mashuleni na vyuoni na katika nyanja mbalimbali za kiutawala na kimaendeleo.

  Kukumbukumbu zangu zinaonesha kuwa ni hivi majuzi tu, nchi ilikuwa katika tatizo sugu la mgawo wa umeme na katika harakati za kujinasua kulikuwa na mapendekezo mbalimbali ya nini kifanyike, ikiwepo pendekezo haramu la kuwasha mitambo ya kampuni ya kitapeli ya Dowans. Mimi kama mwananchi nilikuwa nikiendelea kusikilizia maumizu ya mgawo wakati wanasiasa wa Tanzania wakiwa wanatafuta suluhisho la tatizo hili. Na mpaka ninakwenda mitamboni sikuwa nikijua nini suluhisho la hili tatizo kwani tuliambia mabwawa ya kuzalisha umeme yalikuwa na maji chini ya kiasi kinachotakiwa.

  Nikakaa kuomba mvua inyeshe. Hata hivi majuzi Bwana Kikwete naye akaagiza viongozi wa dini waombee mvua. Lengo tuwe na maji ya kutosha kwa ajili ya kilimo, pia mabwawa yetu ya kuzalisha nishati ya umeme yajae. Sijaona mvua (sijui dhambi zimedhidi nchi hii?).

  Lakini umeme sasa unapatikana masaa 24.

  Wahandisi husema:
  "The important thing about a problem is not its solution, but the strength
  we gain in finding the solution."

  Now that we have electricity without rationing gives us strength, coz we are sure of having our daily business activities run smoothly.

  Question: Nini kimefanyika?
   
 2. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  labda walikua wanakata makusidi ili Serikali/Tanesco inunue mitambo ya Dowans haraka.
  lakin baada ya kuona hasira na msimamo wa wananchi kupitia CHADEMA wameona ni bora watulie kidogo.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Shida yako ilikuwa kupata umeme , umeisha upata sasa hayo mengine ya nn ? pata umeme , washa feni nk furahia na familia yako
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  mtera itakua imejaa mkuu... mungu kasikia kilio chetu

  useless politicians!!!
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  that is what we call funika kombe.........
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  AA wapi. Wamewasha DOWANS . Wameingia mkataba wa mwaka mmoja.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  tutajua tu.
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mkuu maana wiki hii imekuwa hambo hambo!!!

  Lakini kupata umeme bila kujua kilichotokea nayo inasumbua maana unaanza kufeel ni favour, and I have favours!!!

  What really happened?
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Iptl hiyo! Milioni 15 kila siku mramba anakula kupitia kampuni yake -total tanzania inayosupply crude oil to iptl!
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Nadhani hujafatilia tume ya Januari Makamba.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  hata iwe tume ya yusuph makamba. we pay tax. we have the right to know how and where our taxes are spent.

  kutupatia umeme tu haitoshi.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hata Ngeleja anayependa kujinadi hajasema kitu! JK aliwaambia juzi pale wizarani kuwa mambo ya TANESCO yaanzie na kuishia TANESCO.
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  connect the dots.

  where is mwanakijiji's ka-nzi?
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ukikatika ndo tuanze kuongea tena eh?
  Lazima tuambiwe kwanini umeme ulikuwa unakatika katika na sasa haukatiki!

  Kama tatizo limeisha tuambiwe na bei watapunguza lini!
  Na lini tutegemee mgao tena,...we ukishiba leo huwazi kesho jombaa?
   
 15. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mgao wa umeme unatumika kama catalyst ya kufikia malengo fulani ya kifisadi.
  Equilibrium ikifikiwa basi!
   
 16. m

  msambaru JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Anaesema tusihoji kwanini mgao umeisha kinyemela katumwa na mafisadi, hii ilikuwa janja ya nyani ili tukikaa gizani muda mrefu tutakuwa wapole kuitikia malipo ya kuumizana.
   
Loading...