Umejipangaje usipoolewa?

Naomba unipe roughly ni asilimia ngapi haitaki kuwa kwenye ndoa. Usiangalie watu wanasemaje, moyo kuusoma ni ngumu.
 
Waliooolewa kutwa tafrani. Tusioolewa hao waliowaoa kutwa kutusumbua. So many unhappy human beings united just for the sake of children and society standards. Usitupanikishe mleta uzi 😏
 
Ifike wakati watu mtambue ndoa sio ya kila mmoja...And by the way nikikosa ndoa ntaingia shambani kulima, au da Joannah unasemaje😌

Nyie ndiyo mnabeba sonona baya sana!!

Kuna binti alijifanya mrembo, mwaka juzi katimiza 40, kajiolesha kwa konda wa school bus aliyekuwa anafuata watoto wake!! (Kajiolesha sababu gharama zote kuanzia mahari mpaka harusi hadi makazi wanayoishi ni ya mwanamke)

Mpaka sasa kajitahidi, mwanaume ana biashara na amebadilika kutoka umtaa mtaa sasa hivi ni gentleman!!
 
Kila mtu na maisha yake aliyojipangia na kujichagulia....unadhani ndoa ni kipaumbele cha kila mtu🙄🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…