Umeitwa kwenye hii kesi,ungesuluhisha au kushauri vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeitwa kwenye hii kesi,ungesuluhisha au kushauri vipi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Wazo Langu, Apr 5, 2012.

 1. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  [h=6]Jana alfajiri amekuja wifi yangu mke wa mdogo wangu analia usiku wakuamkia hiyo jana kamfumania mume wake na house girl wao. Yeye ana salon yake m,nyamala na huwa siku zote anarudi saa 5 hadi 6 usiku hana hata siku ambayo anakaa nyumbani kuangalia watoto au kumpikia mume wake kila kitu anafanya h.girl. Sasa jana baada ya yeye kuja kushtaki tukamuuliza huyo mume kwanini amefanya hivyo? Anasema ameshachoka na mambo ya mkewe ameshamkanya sana hasikii vilevile hata unyumba hataki kunipa nina mwezi sasa nikimwambia anasema anaumwa kwahiyo nimeamua kuwa na huyu msichana siwezi kupata shida wakati kuna mtu ndani anaweza kunipa ninachotaka. khaaa tukabaki mdomo wazi nikasema haya mambo yakukosa muda kabisa na familia pia ni chanzo cha mume kufanya ujinga wake na house girl. je ingekuwa wewe ndio mie niliekuja kushitakiwa ungefanyaje?
  Hadi hapa napoandika,mke hamtaki tena mume anachotaka talaka yake tu. Mwanzo alimwambia huyo hg atabaki hapo awalee watoto wake mpaka wakue leo kabadilika kaenda kumchukua msichana hata hatujui kampeleka wapi na yy ndio aliemleta.
  [/h]
   
 2. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  hapo pagumu ila jamaa nae kama kazidiwa siangechukua wa mbali mpaka achukue beki3?jaribu kuwabembeleza wasameheane wote wanamakosa ila utengano wao utawaathiri watoto sana
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Waliwahi kukaa na kutishiana kwamba wakinyimbana unyumba mume atatafuta mtu mngine?
  Kama mke anataka talaka, na mume anamtaka housegirl, mbona hakuna kesi hapo? wamesha amua.
   
 4. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  sasa kama housegirl anafanya kazi nyingine zote kwa nini
  asimalizie na hiyo moja? looks like mke kashindwa kutimiza wajibu wake, so lazima asaidiwe..
   
 5. mito

  mito JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,612
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hapo hakuna cha kesi, mke amevuna alichopanda
   
 6. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Mwali,sio kama waliwahi kutishiana,ila kaka anasema mara nyingi amewahi kumsema mkewe kuhusu kutowajibika kama mke,
  Lakini kiukweli yule mke pia ana mchango mkubwa kwa familia yake kupitia hiyo biashara maana huyu ndugu yangu biashara yake ni ya kusafiri hivyo muda mwingi anapokua Dar anakua nyumbani zaidi.
   
 7. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Yeye kwa nini amnyime mumewe sukari? Mmemuuliza hilo swali?
   
 8. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Nimeongea nae na nimemuuliza mengi baada ya kusikiliza upande wa mumewe,
  Wifi anasema sio kweli kua anamnyima ila ni vile mumewe ni mtu wa kusafiri,anaweza akaenda huko akakaa kama tu weeks,akirudi anakuta mkewe labda yupo kwenye siku zake,akimwambia kaka anazua ugomvi mkubwa....
  Siku zingine mke anarudi toka kazini mumewe kalala nae anaoga analala hawaulizani habari ya ndoa.
  Kwa kweli nimepata ugumu kwa sababu sijawahi kabisa kusikia wakilalamikiana kwa lolote kuhusu ndoa yao japo najua kakaangu ni mwingi wa habari lakini mkewe hajawahi kushtaki chochote na mume hajawahi kumshtaki mkewe kwa lolote
   
 9. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli mke anarudi late basi wakae waongee tena nafasi yake
  wasimlazimishe kufanya hizo kazi za kuleta pesa, then wategemee tena
  kua atafanya na kazi za ndani sawasawa na yule alie chagua za ndani tu.
  Kama walikua wamesha yaongea na mke akasema hawezi badilika,
  Basi ilibidi mume achukue hatua ya kuongea na ndugu zake, au kumwachisha kazi etc.
  Sio kuanza uhusiano na mwanamke mngine, tena housegirl. Angemtilia sumu je?
   
 10. Wazo Langu

  Wazo Langu JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 1,344
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio ametupa kigugumizi,kwa kweli nimeshindwa kusema lolote maana nimemuuliza huyu ndugu yangu anajua madhara ya kutembea na mtu anaekaa nyumba moja na mkewe?
  Kama alimpenda huyu housegirl bora angemuhamisha hapo nyumbani wafanyie mbali,
  Ni kweli wifi yangu amekosea lakini kweli alistahili hili??
  Anataka kuondoka kabisa,analia muda wote,mimewe hata haombi msamaha ananikera sana,nadhani mapenzi hayapo tena lakini wakiachana wale watoto ni wadogo na kazi za wazazi wao watakua na mazingir magumu kukaa kwa mzazi yeyote maana wanahitaji msaidizi,huyu ndugu yangu najua hataweza kabisa kulea hawa watoto,sio kipato,ila ni jinsi anavyoendesha maisha yake,
  Huyu mke tunaona kabisa bado anampenda mumewe ila mume kajitia kiburi
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  huyo mwanamme hawatoshi wote wawili??
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wanaume bana, sasa waanze kufanya threesome
   
 13. g

  gambalanyoka Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dada sema na mwanamke mwenzio yeye arudi chini arudi nyumbani,mwambie atafute namna ya kumhudumia mumewe,awe anaweza kuwa anarudi home anampa mumewe unyumba halafu wanaenda wote kazini.Aangalie maisha ya watoto
   
 14. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Lazima tufahamu kuwa katika maisha watu tuna misimamo tofauti
  Binafsi naweza kumsamehe mke wangu au mume wangu kama (ningekuwa
  mwanamke) kwa kosa la kuniwekea Sumu n.k Lakini Abadani! Narudia....
  Abadani kwa lugha nyingine kamwe.... siwezi kusamehe kosa la kufumania.
  Hapo ni kuachana tu.
   
 15. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Unajua mwanamke aliumbwa kumuhudumia Mwanaume katika Maisha hasa hasa mambo ya Nyumbani. Kupika,kufua,Kufanya usafi, ndani na Nje bila kusahau TENDO ambalo ni Muhimu kuliko Yote.

  Wanawake wa leo wanaona wanapokuwa wanatetewa kwenye TV. Oh oh mwanamke akiwezeshwa anaweza. Kwahiyo akipata kazi Anasahau Majukumu Yote.

  Hebu Angalia Makosa ya Shemeji Yako.

  1. Inaonekana anaondoka Mapema Nyumbani, hata chai anapika na Kuandaa House girl

  2. Anamwacha Mume anaandaliwa chai na vitafunwa na House girl, na kuambiwa kwa sauti ya Upole "Karibu Baba" na Magoti anapigiwa anaponawishwa mikono

  3. Ule upendo aliokuwa nao wakati HG hajaja, umepotea maana yote amemwachia HG. Kwahyo majukumu yote ya kumhudumia mume amempa Mfanyakazi.

  4. Anaporudi Nyumbani amechelewa ajue kuwa kuna Mda hata mme anataka kuongea na mke wakiwa pamoja alone, sasa anajikuta yupo na House girl na Yeye anamihemuko


  kwahiyo kama akikuta amelala ajue kazi tayari imeshafanyika kwa House girl

  Wanawake mnatakiwa kujua hili, mwanaume anahisi wakati Wote. Na kama zikijitokeza halafu anayemtegemea anamzingua Mara Nimechoka,Sijisikii , Oh ninakazi. Atatafuta wa Kuzituliza hisia hizo hata kama ni Malaya atamtafuta. Maana ameshachoka na Visingizio vyako, visivyoisha
   
 16. m

  mdigoo Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo hapo juu maneno unajua kwa upande wa mwanaume uvumilivu umeshinda pia sio mtu muongeaji ndo maana kakaa nalo mpaka likamshinda na ndo hivo hata mda wa kuongelea hilo ukakosekana na yakatokea yaliyotokea..
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  huyo mwanaume ana tamaa ya fisi tu anatafuta sababu ya kutupa lawama...............

  Kama hiyo ndo ratiba ya mkewe siku zote alikuwa anaishije? Ndani ya huo mwezi alokosa unyumba alimuuliza mkewe ana tatizo gani? Au kama kaelemewa na kazi walisaidiana na mkewe kutafuta suluhu?
  Kwa hiyi mume akibanwa mke akalale na houseboy?

  Mnapoamua kutafuta kuna vitu mnasacrifice, unaposhindwa zungumza na mkeo.

  Pili huyo mke hadi saa 5-6 usiku saluni anamtengeneza nani nywele usiku wa manane?
   
 18. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Ebu angalia Mwanaume anavyosema

  1. Anasema
  ameshachoka na mambo ya mkewe ameshamkanya sana
  hasikii vilevile hata
  unyumba hataki kunipa
  nina mwezi sasa

  2.nikimwambia anasema
  anaumwa

  3.kwahiyo nimeamua kuwa na huyu
  msichana siwezi kupata
  shida wakati kuna mtu
  ndani anaweza kunipa
  ninachotaka

  Hebu angalia Mwanamke na Yeye

  1.Yeye ana salon yake

  2.huwa siku zote anarudi saa
  5 hadi 6 usiku

  3.hana hata
  siku ambayo anakaa
  nyumbani kuangalia watoto
  au kumpikia mume wake kila kitu anafanya h.girl.

  Ebu Angalia Nani ameacha Majukumu yake Hapo?

  Wanawake nawasihi huku Moyo wangu unauma TIMIZENI WAJIBU WENU KWANZA.

  hakuna Raha kama kuhudumiwa na Mke wako,
  Ndo maana Tunawaoa na Kuwatolea Mahali maana Tunataka Mtuhudumie sisi na Familia Tutakayoanza
   
 19. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Alichofanya jamaa ni sawasawa, simpingi hata kidogo ........kama hapati KITUMBUA angefanyaje?!
  MP.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ningewaachia wenyewe wayaamuwe, nisingependa kutetea upande wowote kwani kila mtu ana makosa yake!
   
Loading...