Hapo ndio ametupa kigugumizi,kwa kweli nimeshindwa kusema lolote maana nimemuuliza huyu ndugu yangu anajua madhara ya kutembea na mtu anaekaa nyumba moja na mkewe?
Kama alimpenda huyu housegirl bora angemuhamisha hapo nyumbani wafanyie mbali,
Ni kweli wifi yangu amekosea lakini kweli alistahili hili??
Anataka kuondoka kabisa,analia muda wote,mimewe hata haombi msamaha ananikera sana,nadhani mapenzi hayapo tena lakini wakiachana wale watoto ni wadogo na kazi za wazazi wao watakua na mazingir magumu kukaa kwa mzazi yeyote maana wanahitaji msaidizi,huyu ndugu yangu najua hataweza kabisa kulea hawa watoto,sio kipato,ila ni jinsi anavyoendesha maisha yake,
Huyu mke tunaona kabisa bado anampenda mumewe ila mume kajitia kiburi
Unajuwa dadaangu hakuna kitu kibaya kama kudharauliwa na wifi yako alifanya hayo kwa mumewe. Dharau hasa ikitoka kwa mwanamke ina sumu kubwa kwa ndowa na huyo mdogo wako aliila hiyo sumu muda mrefu kiasi cha kuuwa kabisa penzi lake. Kifacho kinatabu kuja juu.
Iwapo mambo yaliyomfanya aowe hakuyapata kwa wifi yako na badala yake anayapata pengine, shida ya nini? Huyo wifi yako akashughulikie alichokithamini na akiondoka basi ndugu yako atahalalisha yule anaemjali.