Umefikiri Mara Ngapi Kuhusu Hili?

Kapo Jr

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
996
280
Mungu kaumba ulimwengu na walimwengu, katupa ruhusa ya kuvuta pumzi na kuenda sawia au tofauti na amri zake, hapa nimefikiri bila ukomo kwake Mungu na amri zake kwetu viumbe wake, je uongozi/utawala au milki za kidunia zina amri na taratibu zake? na ikiwa zipo kwa nini hazifuatwi au ni kizazi(sodoma)ovu? na kama kusingekua na utawala/uongozi wa kisheria tungeishi salama? au utawala wa kisheria ndio chanzo? kwa mwendo huu nna hofu hapa kwetu, ni fikra zangu kiufupi, tujadili wakuu
 
Pamoja na sheria na taratibu za kidunia, si rahisi kuzifuata kwakua kila kizazi na mwenendo wa kidunia, tulikua na imani ya kuomba mvua kuchinja wanyama sasa tunapiga mabomu kwakua hata IBADA pia zimewashinda wengi
 
Mungu kaumba ulimwengu na walimwengu, katupa ruhusa ya kuvuta pumzi na kuenda sawia au tofauti na amri zake, hapa nimefikiri bila ukomo kwake Mungu na amri zake kwetu viumbe wake, je uongozi/utawala au milki za kidunia zina amri na taratibu zake? na ikiwa zipo kwa nini hazifuatwi au ni kizazi(sodoma)ovu? na kama kusingekua na utawala/uongozi wa kisheria tungeishi salama? au utawala wa kisheria ndio chanzo? kwa mwendo huu nna hofu hapa kwetu, ni fikra zangu kiufupi, tujadili wakuu
Dah! mi ni kama sijakuelewa vyema mkubwa,hebu rudia rudia jamaa!
 
ni kama kizazi kilichopo hakina hofu ya Mungu na kiama,wengi wetu tunatenda maovu kwa kujua au kutojua kwa binadamu wenzetu,hapa nazungumzia viongozi na wasio viongozi!!
 
tumeumbwa kwa mfano wa Mungu(maandiko ya biblia),lakini mara nyingi tumetendeana ukatili baadhi yetu!!.Hapo natatizwa sana jinsi gani binadamu atende unyama kama vile kuua wakati imeandikwa,"mwanadam aliezaliwa na mwanamke siku za kuishi kwake ni chache",imani yangu ni kwamba watu wanaokesha maabara kuunda silaha mpya kama si ubinafsi wa kutaka kuonekana ni zaidi ya wengine,hapa vita au machafuko yasingetokea
 
Mungu alitupa amri 10(sheria kuu),ili tuishi bila kukwazana au kumkwaza Mungu ili tuikwepe jehanamu. **********Nchi mbalimbali ulimwenguni zina katiba na sheria katika mfumo wa ki-utawala/uongozi wao ambapo kila mmoja anapaswa kufuata bila shuruti,hapa haijalishi ana wadhifa gani,ila swali langu ni je,kama ulimwenguni tungeishi bila kuweka sheria zozote bali kuzingatia amri kumi za Mungu(kwa Wakristo,sijajua Kama Waislamu Wana Amri Hizo),kwa Mtazamo wangu nadhani ulimwenguni kusingekua na vita au uonevu kiasi kwamba hata wafitini na wachonganishi wasingalikuwepo. Angalau ntaeleweka wakuu!!
 
Mh nimerudia kusoma zaidi ya mara 2 nimetoka kapa,sijui kichwa changu,ngoja wengine wachangie labda nitaelewa.
 
Mtu mmoja akisema ajaelewa bas ndo kila mtu ajifanya hajaelewa, hapo sasa hamjaelewa nn? Au lugha yenu ni kichina waacheni wanaotumia kiswahili wachangie lakini sio lazima kuchangia unaweza ukafanya mambo mengine tu kama hujaelewa,kwa sababu baadae hautaulizwa.na hakuna mtihan ambao utatakiwa kujibu.
 
japo lugha kali sana umetumia,lakini kwa upande mwingine lugha inaeleweka hapo ni kufikiri kilichozungumza ni mambo yanayotuzunguka wadamu maishani
 
Back
Top Bottom