Umefanana sura na baba au mama?

Umefanana sura na baba au mama?

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,801
Reaction score
43,177
Habari za siku tele,

Nipo kama sipo.... nimetingwa hatarii hadi nimesahau kama mahaba yapo.

Leo niko na issue ya kawaida tuu, tumezoea kusikia mti akisema mtu mwenyewe una sura ya baba au unajifanya mrembo huku sura ya baba. Au mtu anaambiwa na wenzie kwa kejeli, unatusumbua tuu hapa una sura ya mama na vitu kama hivyo.

Nimejiuliza tuu, sura ya kike ni ipi na ya kiume ni ipi? Au tumecremisha mwanaume ndo mbaya na mzuri ni mwanamke?

Ngoja niwaulize, inakuwaje pale mschana mrembo wa sura akija kuzaa mtoto wa kiume afanan nae mnoo, huyo mtoto akiwa mkubwa watasema ana sura ya kike. Na ikitokea mwana kaka wa kawaida tuu (waswahili wanasema ana sura ngumu) akipata mtoto wa kike na wakafanana mnoo, huyo mtoto akiwa mkubwa ataambiwa ana sura ya kiume.

What if mtoto wa kiume afanana na mama yake sanaa ile tunasema kopiraiti, lakini mama yake alifanana na baba yake mno (babu wa mtoto wa kiume) hapo hamuwezi sema huyo mtoto ana sura ya kike bali ya kiume.

Vivo hivyo pale mtoto wa kike anapo fanana sana na baba yake huku lakini baba yake alifanana mno na mama yake (bibi wa mtoto) huyo mtoto hatuwezi sema ana sura ya kiume.

Haifai na si vyema kubeza watu wana sura ya kike au ya kiume. Sote tumeumbwa kwa sura na mpango wa mungu, mzuri kwako mbaya kwa mwingine, mbaya kwako mzuri kwa mwingine.

Jumapili njema.

Ciao.

Kasie Matata.
 
Me nahisi nimefanana na baba'ngu kwa vyovyote.

Hivyo wanaokufahamunawanao mfahamu baba yako watasema umepata taswira ya baba na si kusema una sura ya kiume. Maana kuna uwezekano kuwa taswira yake imefanana mno bibi yako ambaye ni mama yake. Wengine husema umefanana na bibi yako.

Lakini pia yaweza kuwa taswira ya baba yako imefanana mno na baba yake ambaye ni bibi yako, yote ni heri. Hakuna sura ngumu wala sura ya kiume.

Msalimu sana baba mumu.
 
Basi tu ni kejeli za ki binadamu! lkn ukweli wa mwanaume au mwanamke ni jinsia tu, sura ni changanyikeni

Kweli kabisa usemacho, sura ni taswira tuu na ni changanyikeni.
 
Back
Top Bottom