Umebarikiwa mkono utoao

Umebarikiwa mkono utoao

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
400
Reaction score
811
kuna mchungaji mmoja (MCHUNGAJI RUN DMC) aliwahi kuzungumza vitu vitatu kuhusu utoaji akasema
" 1. alisema UNAPOTOA, unaweza kua unaokoa maisha ya mtu; yaani kwa mfano chukulia umempa mtu shilingi elfu kumi halafu akaitumia kwenda hospitali

2. pili akasema UNAPOTOA unagusa watu; fikiria mtu hajala tangu asubuhi ukampa sahani ya chakula

3. na tatu akasema UNAPOTOA unaimarisha UPENDO. mfano fikiria unapompa kitu mtu lile tabasamu atakalotoa na shukrani ni upendo mkubwa pale anaposema AHSANTE MUNGU AKUBARIKI

hivyo ndivyo vitu vitatu alivyoongea mtumishi wa Mungu mchungaji RUN.Lakini pia biblia inasema UMEBARIKIWA MKONO UTOAO. hata hivyo tujitahidi kutafuta pesa maana SIJAWAHI KUSOMA MAHALA POPOTE MAANDIKO YANAYOHAMASIHA UPOKEAJI.

Siyo jambo baya KUSAIDIWA ila nadhani UNAPOPOKEA JITAHIDI NAWE UTOE japo kidogo maana kusema kweli baraka zinatajwa kwenye KUTOA tu. namkumbuka mkuu wangu wa shule kipindi niko sekondari Brother Martin Masabo aliwahi kusema The less you have, is the less you Give akimaanisha KIDOGO ULICHONACHO NDICHO KIDOGO UTOACHO.

Pia MASABO anaongeza THE MORE YOU GIVE IS THE MORE YOU GET.
 
Hapo unafundisha au unalaumu.

Toa kama umejaliwa kuwa navyo.

Mkono unaotoa ndio utakaopokea.
 
Back
Top Bottom