Wewe na mpenzi au mwenza wako mmeachana au kutalikiana kwa wale wenye ndoa sikatai. Hoja yangu ni kwanini umnunie shemeji au wifi yako hadi kutokusalimiana? Je ni ni uungwana ama ni halali? Tujadiliane.
Walale mbele huko watasalimiwa na wengine
Mnasalimiana ili iweje labda?
Labda walitia chumvi iliyopelekea wahusika kufikia hatua hiyo maana ndugu wengine nuksi kweli kuingilia mahusiano ya ndugu yako inahuu?
Kama wanatia chumvi wewe tia maji muwapotezee. Kama mshaachana msahau na angalia mbele. Vinginevyo litakuumiza utamchukia kila mtu. Adui mwombee maisha marefu...
Inategemea nilikua na ukaribu nao vipi lakin kugombana na ndugu yao s kugombana na ukoo mzima ntawasalimia as usual
Kuna maisha baada ya talaka.