Umeachana na Mwenzio, Mmeo au Mkeo chuki ya nini na (nduguze) Wifi au Shemeji zako?

chameleon

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
555
170
Wewe na mpenzi au mwenza wako mmeachana au kutalikiana kwa wale wenye ndoa sikatai. Hoja yangu ni kwanini umnunie shemeji au wifi yako hadi kutokusalimiana? Je, ni uungwana ama ni halali? Tujadiliane.
 
Wewe na mpenzi au mwenza wako mmeachana au kutalikiana kwa wale wenye ndoa sikatai. Hoja yangu ni kwanini umnunie shemeji au wifi yako hadi kutokusalimiana? Je ni ni uungwana ama ni halali? Tujadiliane.

Duuh ila kweli ebu waje watuambie huaga nn hasa kinawakumba after kuachana !???
 
Labda walitia chumvi iliyopelekea wahusika kufikia hatua hiyo maana ndugu wengine nuksi kweli kuingilia mahusiano ya ndugu yako inahuu?
 
inategemea na sababu ya kuachana na matukio yalo ambatana.hapo chuki inakua aihusiani na mahusiano tena bali matendo mlofanyiana.
 
Labda walitia chumvi iliyopelekea wahusika kufikia hatua hiyo maana ndugu wengine nuksi kweli kuingilia mahusiano ya ndugu yako inahuu?

Kama wanatia chumvi wewe tia maji muwapotezee. Kama mshaachana msahau na angalia mbele. Vinginevyo litakuumiza utamchukia kila mtu. Adui mwombee maisha marefu...
 
Inategemea nilikua na ukaribu nao vipi lakin kugombana na ndugu yao s kugombana na ukoo mzima ntawasalimia as usual
 
Muunganiko wao umeshavunjika hivyo wamebaki watu wa mataifa.... Jambo la msingi kabla ya kumtambulisha au kutambulishwa hakikisha umejiwekeza vya kutosha maana mengine ni aibu na fedheha kwa watambulishwaji..... Kuna wengine wanadumu kumwita shemeji au wifi milele, hapo si sawa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom