Mambo 10 unayoweza kufanya kumlinda mpenzi wako badala ya kumchunga

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Kuwa na mipaka na mambo yako ya pembeni
Acha kuishi kama msela ikiwa unaye mpenzi au mwenza, unapokuwa bado na mambo ya kama uko pekeako unapaswa kutambua unachokifanya pipoas kumuumiza uliyenaye. Kulimwaga chozi la mpenzi au mwenza kwa makusudi ni kosa, ni kukosa kumlinda.

2. Kukumbuka ngono salama unapochepuka ama kuwa naye.
Wengi ujua ngono salama ni kwa ngono za nje, hapana hata ndani, ngono salama siyo tu kuepuka maradhi bali hata maumivu na uzalilishaji katika ngono. Kama kufanya asichopenda uwapo naye faragha. Uumiza mwili na saikolojia ya mwenza wako. Mlinde mwili na akili yake isivurugwe nawe.

3. Uzazi wa mpango.
Mwanaume na mwanamke watoto wasiotarajiwa, uleta msongo wa mawazo, kukimbiana, kulaumiana, kuvuruga mipango, amani ya wawili, kuchukia ngono na umaskini. Kusudia uzazi kwa kufuata hali ya mwenzio na malengo yake au lah! Muelewane.

4. Kumjali kiafya kwa kupumzika na chakula bora.
Mhudumie mwenza ale chakula bora na mwanamke pika vizuri chakula bora acha kuunguza, ujui jifunze acha aibu, Suala siyo mapesa mengi bali unakula nini na kinakupa nini. Kumpa muda naye apumzike, msaidie kazi na usimpande au usitake akupande kama punda, naye muache apumzike.

5. Kumliwaza kwa maneno na matendo yenye kuaminisha unampenda.
Zifungue hisia zako kwa maneno unapokuwa naye atambue upendo wako ulivyo hai kwake, fanya mambo yanayoonyesha unampenda kwa kumpa muda wako, nguvu zako, utashi wako, msimamo wako wa maisha na utayari wa yajayo katika maisha na maumbile. Imani ni amani kubwa ya mapenzi na maisha.

6. Kuonyesha kupenda watu wake wakaribu na familia yake.
Penda familia ya mpenzi (mwenza) wako na watu wake wa karibu. Ni mbaya kusema unampenda yeye alafu utaki wazazi na nduguze na rafikize. Wewe utakuwa ni sumu ya maisha yake na familia yake. Familia ya mpenzi wako unapoijali huwa ni watetezi wako na wapambe wako katika mapungufu ya mwenza wako.

7. Kumheshimisha machoni pa watu na ndani ya nyumba.
Onyesha yeye ndiye mmiliki halali popote na kama wewe ni malaya paka basi onyesha yeye ndiye namba moja kwako, yaani kwa lolote anza kwake ndiyo uende kwa waswantwa wako. Ni sahihi ukipenda ukakubali kumuweka ndani au akuweke ndani kisheria, kidini au kitamaduni. Maisha ya kunyooshewa vidole kwa kuteswa na mwenza wako, kufanywa kama nje ya boksi nk ni kuharibu akili na mwili wa mwenza wako.

8. Kumpa uhuru wa kiuchumi na kimawazo.
Kuacha unyanyasaji wa kimawazo na kumiliki njia za uchumi mwenza wako, muache naye ashauri, awaze na ajishughulishe na kwa mwanamke unampomzidi kipato mwanaume wako usimnyanyase au kumfanya chombo cha starehe na mdori.

9. Kusimamia majukumu ya jinsia yako na kuonyesha wewe ni jinsia hiyo.
Mwanaume anayo majukumu jamii imeyaweka wazi na mwanamke anayo majukumu jamii imayaweka wazi. Unapoyafanya basi ni kumlinda uliyenaye. Mifumo dume na usawa wa kijinsia visiwe ni harakati bali kujitambua kipi ni stahiki kwa mwenzio kukufanyia.

10. Kuishi wawili.
Kujitenga na majungu, maneno ya kuambiwa, kutafutana ubaya kupitia watu, kuingiza wengine kuwa walimu wa penzi letu na malezi yenu. Lazima mtambuame wenyewe na kwa kuwa nyie ni watu siyo malaika, lazima muweze kudhibiti mihemko yenu na hasira zenu.

Kusikia siyo kosa, kupewa mdomo siyo kosa, kupewa mikono siyo kosa, kupewa hasira siyo kosa ila kosa unavitumiaje katika kufanya maamuzi ili kufikia maamuzi sahihi.
IMG_20230204_094315_958.jpg
 
Mie napenda nipewe hela na mpenzi wangu ila sio kumfilisi nikiasi namie sipendi kuombwa pesa
Mi napenda mwanamke awe na uhuru wa kiuchumi, anapokuwa bize na kuumiza kichwa huwa anapata akili ya kujua ugumu wa fedha, nidhamu ya fedha na kuheshimiana.
 
Back
Top Bottom