Umbea. . .

yan mie kwa kusuta na kusuta
mdomo ushakuwa mrefu kama mkonga wa tembo

afu mkiwa mnaenda kusuta mmevaa na sare ya madira inanoga kweli
na skin tait za orange
kama tu sherehe nyingine yeyote

Hahahah. . . unashona kabisa vazi maalum?
 
Sijawahi wala sitegemei kusutwa! Sina muda wa kufuatilia mambo ya watu hivyo sio rahisi kukutana na umbea!
 
madira ya kusutia yanauzwa 6500 na skin tait 1500
tandale mall
kama huna hela used yapo
kama huna kabisa unaazima kwa jirani

Hahahah. . . unashona kabisa vazi maalum?
 
madira ya kusutia yanauzwa 6500 na skin tait 1500
tandale mall
kama huna hela used yapo
kama huna kabisa unaazima kwa jirani
Kaaazi kweli kweli. . .
Ila kama unataka kumsuta mtu ambae amepaniwa na wengi unawachangisha. . lolz
 
Hivi ukiwa mmbeya unaweza kuacha umbea kweli?
 
Hahahaha. . . eti wakaondoka na blender!!Kweli uswahilini kuna vituko.
Uswahilini watu wanaishi maisha natural siyo ya kuigiza kama hutakiwi unapewa za uso kavu kavu. Mambo ya kununuliana Khanga zenye maneno ya mafumbo na kufunguliana nyimbo za taarabu yameshapitwa na wakati!
 
Nasikia dalili za mtu mmbeya mdomo wake unakuwa mweusi kama wa kunguru..lol.
 
Uswahilini watu wanaishi maisha natural siyo ya kuigiza kama hutakiwi unapewa za uso kavu kavu. Mambo ya kununuliana Khanga zenye maneno ya mafumbo na kufunguliana nyimbo za taarabu yameshapitwa na wakati!
Siku hizi ni live live. . .
Kaaaazi kweli kweli. Kanga na taarab sasa zitakosa soko,soko lihamie kwenye madera na matarumbeta.
 
Sijawahi!, mambo ya online sijawahi kuyachukulia serious kivile.... Hivi kumbe kuna kusutwa online?

Hhmm kusutwa sijui ila umbea najua.
Or atleast najua mtu ambae anashiriki sema ndio kama hivyo hata nae hachelewi kusema "sijawahi mie". Au labda mwenyewe hakuona ni umbea. . . .
 
Na ulivyo muoga nafikiri ulilia sana na ndipo maana hawakukupa kipondo my switluv
 
Na ulivyo muoga nafikiri ulilia sana na ndipo maana hawakukupa kipondo my switluv

Hehehehe pamoja na udogo wangu wavulana walikua wananiogopa sembuse wasichana?

Mi sijawahi kuonewa aisee. . . kuna mvulana alijaribugi nikamfanya mfano, tangu siku hiyo sikuhitaji tena ulinzi wa dadaz, kakaz wala unclez.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…