Umbali wa Ubelgiji hadi Marekani na Ubelgiji hadi Tanzania

UMBALI WA UBELGIJI HADI MAREKANI NA UBELGIJI HADI TANZANIA.

Waraka wa BASHIR YAKUB
+255784482959.


Kutoka Ubelgiji hadi marekani ni km 7573, wakati Kutoka ubelgiji hadi Tanzania ni km 7240.

Kwahiyo ni rahisi kutoka ubelgiji ukaja Tanzania kuliko kutoka Ubelgiji ukaenda Marekani.

Maana yake hata kwa kigezo cha afya kwa wale wagonjwa inawezekana zaidi kwao kutoka ubelgiji kuja Tanzania kuliko kutoka ubelgiji kwenda Marekani.

Mtu ambaye anaweza kusafiri kutoka UBELGIJI hadi Marekani na akafanya shughuli zake huko, anaweza maradufu kutoka Ubelgiji akaja Tanzania, akafanya shughuli zake na akarudi huko ubelgiji ama vinginevyo.

Kwa msingi huu mtu ambaye atasema hawezi kusafiri kutoka UBELGIJI hadi Tanzania kwasababu bado yu mgonjwa, lakini mtu huyohuyo akaweza kusafiri Ubelgiji hadi Marekani, atakuwa ni muongo mkubwa sana.

Na kama kuna majukumu yoyote ya kisheria ambayo anatakiwa kuyatekeleza hapa Tanzania na akawa hajayatekeleza kwasababu ati ni mgonjwa na hawezi kuja Tanzania, basi yafaa achukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kukaidi kutekeleza majukumu yake kwasababu anazozijua yeye mwenyewe.

Na kama anakesi mahakamani ambayo inaahirishwa kwasababu ya ugonjwa, basi waendesha mashitaka wanapaswa kuiongoza mahakama, na mahakama inapaswa kutoa adhabu kwa kukaidi kuhudhuria mahakamani wakati akiwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Unahitaji uendelee kupata mshahara wa bunge . Na unajua unapata mshahara huo kupitia migongo ya wananchi wa jimboni kwako waliokuchagua na kukuwezesha kupata mshahara huo. Lakini mbona unasafiri umbali mrefu kuwasabahi wasiokujua hata we ni nani badala ya kusafiri umbali mfupi kuwasabahi jimboni kwako ambako sasa inakaribia miaka miwili hawajakutia machoni.

Tatizo tuna bahati mbaya ya kuwa na mamlaka ambazo hazing'amui mambo haraka.

Ziara hizi za umbali mrefu na mfupi ni ushahidi tosha popote pale kuwa tayari anao uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kibunge na kimahakama huko aliko na kesi.

Kwa ushahidi huu spika anasubiri nini kuchukua hatua, kadhalika waendesha mashtaka wa serikali wanasubiri nini kuiongoza mahakama ichukue hatua kwa mshitakiwa kutohudhuria mahakamani.

Nyote si mmeona, kazi anazozifanya huko ni zilezile ambazo angezifanya akiwa hapa. Ni zile zile tu za kuzungumza kwenye forum mbalimbali.

Wananchi wa jimbo lake hawakumwezesha kupata mshahara wa bunge ili akajijenga ughaibuni bali awajenge wao.Anafanya ubadhirifu.

Mamlaka zinatazama mtu akifanyia kodi za watu ubadhirifu. Sio sawa. Amethibitisha mwenyewe kwa matendo yake kuwa sasa afya anayo. Basi aje atekeleze majukumu yake au atangaze rasmi kuachana nayo kwa yale ambayo anauwezo wa kuachana nayo.

Ni ushahidi gani mwingine mnausubiri kujua kama huyu mtu sasa yuko vizuri kiafya.
Usafiri wa wenzetu huko duniani ni rahisi sana kuliko kuja huku mbondeni kwetu. Pia kutembea siyo mtu amepona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom