Umbali mara uzuri sawa sawa sawa na ujinga

Umbali mara uzuri sawa sawa sawa na ujinga

Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2017
Posts
1,940
Reaction score
3,858
Habarini wana jamvi

Hesabu hiyo hapo juu imekumba zaidi ya 90% ya wanaume katika mahusiano kwa namna mbili kuu

1. Kumuona mwanamke kwa mbali na ukavutiwa nae mara baada ya kumkaribia ndo unagundua si wa viwango ulivyovifikiri ila tu umedanganywa na umbali

2. Kumpata mwanamke mzuri, mpole na mnyenyekevu, kisha unagundua katika upole wake na unyenyekevu kumefichwa udhaifu usiomithilika wala kuvumiliwa

3. Kudate na mtu mtandaoni kisha baada ya kukutana ndo unaelewa umbali mara uzuri ni hesabu halisi inayo upata ujinga wako bila chenga.

Iko stori ya jamaa angu mmoja alizama shivazi (chuga hiyo) akapiga maji, baada ya kuwa tila akamdandia manzi kwa sababu ya maji akaona ni chombo haswa akaenda kupiga mzigo, asubuhi anaamka hakuamini alichokiona yaani kama vile ubongo ulimsaliti kwa kumuuzia simu kumbe kipande cha sabuni.

Je, ulishawahi kutana na umbali mara uzuri kisha ukajipata ni mjinga?

Hebu tupe mkasa wako unao ukumbuka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom