Umasikini wa kwetu Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Duuu,
Nimekuwa nikiimba kuwa Sikonge kuna umasikini wa kutisha ila hakuna anayeweza kujua ni wa kiasi gani. Ili kuonyesha hali hiyo, natuma hii link muone hizo picha:-

Album * Moravian Board of World Mission

Ukiona hii kitu hadi unashindwa kuamini kuwa Tanzania kuna umasikini wa aina hiyo. Halafu Wazenji wanasema Tanganyika tunawaibia. Wengine wanasema kuwa tulipie chuo kikuu. Hebu waambie hao watu walipe hiyo dola 20. Jamani msione Dar na kufikiri hiyo ndiyo Tanzania. Nendeni wenyewe mkaone hali halisi huko ambako hata shetani hataki kufika, maana kashaweka giza la kutosha.
Haya sasa, kwa wenye nazo au ukiweza muonyesha mtu huko, mwambie aje a-adopt kijiji kimoja na kukitunza maana wenye nchi, yes wenye nchi huwa wanakuja kuwaona watu wao kwenye uchaguzi tu.

Hayo majengo marefu mtakayoona si Magorofa, ila majumba ya kukaushia tumbaku. Tumbaku inamaliza watu na misitu. Kwenye manunuzi watu wanaibiwa na watu hawana jinsi nyingine...

Mods, hii baadaye unaweza ichanganya na ile ya kijana anayejenga shule Tanzania kwa kukusanya michango......
 
Tatizo kubwa la Sikonge ni unyamwezi, ubaguzi kama ule wa kenya, neda Sikonge ujionee wanataka mtumishi yeyote awe na asili ya sikonge tutafika?
 
Tatizo kubwa la Sikonge ni unyamwezi, ubaguzi kama ule wa kenya, neda Sikonge ujionee wanataka mtumishi yeyote awe na asili ya sikonge tutafika?

M-bongo,
Hivi mtumishi unayesema ni mtumishi wa wapi? Huko hata sehemu za kufanya kazi ni chache sana. Sanasana hospital huko ndiko kuna wafanyakazi wengi na hiyo ni ya Moravian church. Zinafuata shule za secondary za Lowasa na shule za msingi. Shule ya maana ni hiyo ya Mbirani ambayo pia ni ya Moravian na ni ya siku nyingi sana (Lipumba alisoma hapo dara la tano hadi a nane). Vinginginevyo inabaki bank, Polisi, Mahakama, Posta na labda sehemu za simu na Tanesco. Sasa hizi zote sanasana zina watu watano watano.
In short ni kuwa SIKONGE hamna ajira. Hivyo kusema mtumishi atoke Sikonge sijui una maana mtumishi yupi? Kama kuna mtu Sikonge anatoa ajira basi sanasana Waarabu na vigari vyao.

Tatizo la UNYAMWEZI. Hili nakubaliana nalo sana tu. Hili la unyamwezi limechangiwa sana na watu wa pale kuona UARABU ndiyo mali sana. Haka ka-uarabu tumekapenda na tunataka tuwe Waarabu kwa kila kitu. Maadamu wao wana duka, na sisi tunataka tuwe nalo. Tusifanye kazi yoyote tuwe wafanya biashara. Biashara yenyewe ni tufungu twa karanga, kamba za miti ya Miyombo, sindano na uzi, Bangiiiiiiili, nk Huu ni upuuzi wa hali ya juu.

Tatizo la kukosa zao au biashara ya maana inaumiza sana watu huko. Tumbaku si tu kuwa inaumiza na kuzeesha afya za watu. Inamaliza sana misitu ya huko. Ukiingia Google earth, sehemu inaitwa MOLE, utaona jinsi hilo eneo lilivyowekwa sawa na miti kibao imekwenda. Kijiji ni kikubwa sana na nafikiri kinazidi hata Sikonge ambayo ni wilaya.

Kulikuwa na wazo la kuleta Mibono (Jetroph) huko ili walau watu wakilima mara moja wanabaki tu kuwa wanakwenda safishashamba na kuvuna (kama kahawa). Hili zao linazalisha mafuta ya BIODISEL. Ila sijui hata kama hizo mashine zilishafika au zitajengwa huku kwetu. Nyerere aliihurumia Tabora akajenga kiwanda kimoja cha nyuzi. Ila hiki kilijengwa kiSIASA na si kiuchumi. Kilichotokea huhitaji kujua.
Umasikini wa watu ni rahisi sana kudanganywa. Hebu ona hao watu, unafikiri ukiwapa T-shirt si watakupigia kura ingawa wewe ni fisadi? Ukifanya na mnuso wa kurudi kwenu, baada ya kukamatwa kuwa wewe ni FISADI, basi utapokelewa kwa mikono minne. Nategemea hili zao la Mibono litasaidia wengi na kubadili hali ya huko. Ila serikali inabidi kutumia VIBOKO ili kubadilisha watu wa kule. Haka ka UARABU (Ka-Unyamwezi) kanaleta sana shida. Utawaona na kakiswahili kabovu "Habari ya Usubuhi......." wakiwa ndani ya vikanzu na vikofia. Hapo usifikiri ni Waislam, utashangaa sheick kaingia hotelini kujichana wakati ni mwezi wa Ramadhani.....
 
Kama ulivyowaelezea Wasikonge kupenda Uarabu kwa rangi yake, utamaduni wake na zaidi kama kipimo au kielelezo cha juu kabisa cha maendeleo, ndivyo hivyo hivyo nchi nzima ilivyo. Tuna Wabunge na viongozi wa kadhaa wa kitaifa kwa sababu ya rangi zao na asili yao. Pia tuna Wabunge wengi sana, hawa ni karibu wamejaza Bunge lote, asili ya kuchaguliwa kwao ni Utajiri walio nao,Umaarufu katika jambo lisilo na uhusiano na uwezo wa kuongoza kama kuimba vizuri na zaidi Imani yetu ya kuabudu kila kilichotofauti na sisi hata kama ni Mashonde( kumradhi).

MH Sikonge Wa Sikonge nakubaliana na wewe, ila usidhani ni Wasikonge tu hata wajanja waliozaliwa au kukulia pale Dar wajifanyao hawana Matongotongo wote wanahusudu Uarabu, uzungu na Uasili wa nje ya Tanzania.

Naomba kutoa hoja.
 
Mkuu Sikonge,

Tatizo letu ni kuwa tuna viongozi mabilionea sana ambao hajui kwa nini raia wetu wako vile. Viongozi wanaishi sehemu nzuri sana na hivyo wanachukulia kuwa nchi nzima watu wanaishi kama wao. Matatizo ya umaskini wa raia wetu hayatokani ni uvivu wao au ujinga wao, bali yanatokana na ujinga wa nchi kushindwa kuweka miundo mbinu za kuwafanya raia wajiendeleze kwa kutumia raslimali zao, na vile vile ujinga wa nchi kushindwa kuwathamini raia wake na kutoa kipaeumbele kwa raia wa nje.

Hebu angalia eti watoto hawa watatakiwa wajilipie elimu ya chuo kikuu kama watataka waipate, je kweli serikali ina akili?
full.jpg



full.jpg
 
Mungu anisamehe kwa kulalamika nina shida, hawa watoto kny picha watalalamika nini?
 
Nashukuru sana kwa kukubali u-nyamwezi wa Sikonge maana ninaishi jirani sana na Sikonge, nina rafiki zangu wengi pale si malizi mwezi bila kufika sikonge kwa hiyo ninaijua sikonge vizuri, ninajua mabo ya sikonge vizuri, mfano kwa sasa kuna kamati imeundwa ya kumuangusha mbunge aliyepo madarakani inaitwa SAIDIA SAID ASHINDWE! kamati hiyo hufanya vikao vyake kama vile vya harusi na huchangishana pesa kwa ajili ya maandalizi ya 2010, anayeitwa mbunge mtarajiwa yupo Dar na nadhani atakuwa ni Mh Sikonge! kwa maana hiyo basi hatuwezi kwenda popote mtu bado ana miaka 2 mbele vikao vinaanza vya kumuangusha mtu 4 2-3 yrs Bad luck Sikonge
 
Sasa Wandugu..nini kama wana JF mmefanya kwenu? Wote si mmekimbia kule na kujenga Dar, Mz? Si mnaye Speaker wa Bunge, Kapuya n.k?

Ni wengine ndo hivyo mko ughaibuni na tayari mmeshasahau kwenu!

Kuweni na safari muende Rombo, Machame au Marangu muwe na ziara ya mafunzo!

Acheni kulalamika ..do something..even small!
 
Last edited:
Nashukuru sana kwa kukubali u-nyamwezi wa Sikonge maana ninaishi jirani sana na Sikonge, nina rafiki zangu wengi pale si malizi mwezi bila kufika sikonge kwa hiyo ninaijua sikonge vizuri, ninajua mabo ya sikonge vizuri, mfano kwa sasa kuna kamati imeundwa ya kumuangusha mbunge aliyepo madarakani inaitwa SAIDIA SAID ASHINDWE! kamati hiyo hufanya vikao vyake kama vile vya harusi na huchangishana pesa kwa ajili ya maandalizi ya 2010, anayeitwa mbunge mtarajiwa yupo Dar na nadhani atakuwa ni Mh Sikonge! kwa maana hiyo basi hatuwezi kwenda popote mtu bado ana miaka 2 mbele vikao vinaanza vya kumuangusha mtu 4 2-3 yrs Bad luck Sikonge

M-bongo,
Hiyo kampeni ya kumuondoa Said Nkumba nilishasikia ila sijui inafanyika kwa kuchangishana pesa. Huyu bwana Nkumba kusema ukweli kakaa pale miaka kibao na hakufanya lolote la maana. Hakushirikisha watu wa huko Sikonge ili kuisaidia wilaya yake. Alikuwa ni yeye na CCM/baba yake. Ukija uchaguzi, baba yake ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM, anapitisha jina la mwanae na wewe hata uwe na sifa kama au kuzidi Obama, utawekwa chini. Hii ilimpelekea jamaa kujisahau kabisa katika kusaidia watu wake.
Jamaa ni mshamba fulani kwani nasikia hata akienda bungeni, akifika sehemu ya kupark magari hata kama iko nyeupe, atakwenda pembeni kabisa na kuweka gari lake huko. Huyu jamaa kama sikosei alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Hivyo hata muono wake wa mambo ni wa Kinyamwezi kweli. Watu kama hawa hawatakiwi sasa huku kwetu. Sikonge tumenusa sana makalio ya wilaya nyingine. Muda ufike walau tuanze kwenda sambamba na wilaya kadhaa pale nchini.
Juu ya UKABILA, si kweli hapa ulisema. Nkumba ni Mnyamwezi hasa. Sema kuna wakati mzee mmoja aligombea na wakamwangusha kwa gia ya kwamba yeye ni mtu wa kuja. Nkumba ni wa huko na kwa taarifa nasikia kaenda kujenga MOLE mzinga wa jumba. Ushamba huu jamani. Sasa usijenge walau hapo Sikonge mjini, unaenda kujenga MOLE? Ni kuwa ukifika Tutuo, unaenda ndani upande wa mashariki. Huko kuna kijiji kikubwa sana cha walima tumbaku. Wamekata miti yote huko. Unaweza kukiona kwenye GOOGLE EARTH kwani kinaonekana hadi nyumba, mashamba misitu nk.
Kuna mzee ambaye nasikia anataka kugombea UBUNGE wa huko. Huyu ni ndugu na yule mzee waliyemkataa kuwa ni WAKUJA. Huyu ni mmoja ya watu walio kwenye kamati ya KUENDELEZA SIKONGE. Nilisafiri naye mwezi wa tatu na tukaongea mipango mingi sana waliyonayo. Mmoja wa viongozi ni Ex-jaji Mfwalila. Kama kweli watafanikiwa, Sikonge itabadilika. Walikuwa na plan kubwa na mambo mengi ya kushughulikia. Sintasema mengi kwani mie simo na wala si msemaji wa hiyo kamati. Ila amini usiamini, wana malengo mazuri sana kubadilisha maisha ya watu wa kule. Hili jambo Nkumba wala hakuwahi kuota kulifanya. Nafikiri hata yeye anafahamu kuwa muda umefika wa kuachia wenye UCHUNGU na Sikonge wafanye kazi.
 
Sasa Wandugu..nini kama wana JF mmefanya kwenu? Wote si mmekimbia kule na kujenga Dar, Mz? Si mnaye Speaker wa Bunge, Kapuya n.k?

Ni wengine ndo hivyo mko ughaibuni na tayari mmeshasahau kwenu!

Kuweni na safari muende Rombo, Machame au Marangu muwe na ziara ya mafunzo!

Acheni kulalamika ..do something..even small!

Mzalendohalisi,
Hao unaowasema ni watu wa Tabora ila si watu wa Sikonge. Mtu pekee maarufu wa Sikonge alikuwa jaji na huyu sasa ataFISADI wapi? Hata RA ni wa Igunga. Barabara ya kwenda Urambo iko poa kabisa na huko, kumshinda Sitta kweli kazi. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Sikonge na Rombo, Machame, Marangu nk. Hizi ni eneo za mpakani. Zinaotesha Kahawa, utalii, ndizi nk. Pia zilikuwa na bahati ya kuwa na mawaziri kama Mramba. Pia kuishi Wazungu huko kulisaidia watu wakapata tabia nyingine na si sawa na Sikonge ambako wameishi Waarabu na kutudumaza akili. Usifikiri kuja kuona huko Rombo kutasaidia. Nikiona mnavyozalisha kahawa au Mauwa na kuuza Ulaya, unafikiri nikirudi Sikonge, ntazalisha??? Ntaleta watalii?? Hamna.

Ndiyo maana tumeanza na kampeni za kumuondoa Nkumba na kuleta viongozi na mikakati mipya. Kwa mipango hii, sikonge wataishia form six tu maana wenye uwezo wa kulipia wanao CHuo kikuu, watakuwa wachache sana. Nafikiri juhudi zilizopo, zinaweza kusaidia hao watoto zaidi kuliko kanisa langu linachofanya kuwa eti ku-adopt kijiji. Kwanza hizo hela ukipeleka wajanja wachache wanazila na hawa watoto hawapati kitu.
 
Bara bara ya kwenda Urambo poa kabisa! ningejua unapoishi ningekutafuta nikakuchapa viboko sita vya nguvu na kazi ngumu baadaye! bara bara ya Urambo kwa miaka takribani 40 ya SS ina mashimo, bara bara inayopitika vizuri bila natatizo yenye moram iliyoshindiliwa vizuri ni kutoka Urambo kwenda kaliua kwa kapuya na infact wa kumng'oa kapuya kwa sasa hayupo ila huyo jamaa yako SS anakwenda na maji maana ana kapambe kake hovyo kweli1 na hajafanya chochote Urambo zaidi ya kuwa bize kuhamisha watendaji wa CCM wenye dalili za kutomuunga mkono
 
Last edited:
Back
Top Bottom