Umasikini umewageuza Wasomi kuwa Wajinga

Umasikini umewageuza Wasomi kuwa Wajinga

Kichwa cha uzi wako kinapaswa kuwa "JINSI ELIMU INAVYOZIFUKARISHA FAMILIA ZA WALALA HOI
 
Mkuu upo sahihi sana.Kwanza hakuna kitu kinanikera kama sasa hivi hawa watumishi wa umma kila siku wanapata Masters Degrees kama njugu,hivi muda wa kufanya research,kuandika proposal na Report wanautoa wapi?
Zamani watumishi wa umma walikuwa wanakwenda masomoni kwa ruhusa maalumu,hawa wa siku hizi tunawaona kila siku wanazurura Mikoani alafu baadaye unamuona mtu anatunukiwa Masters!!
Note:Sina wivu ila nimefanya sana kazi za consultancy najua ni jinsi gani kuandaa hizo documents ilivyo ngumu.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app



Mpaka vilaza waloungaunga kwa tabu Eti nao wanazo [emoji3][emoji28]
 
Najua mpo mtakao nipinga ila sijali nitajua napingwa na hao hao WASOMI waliogeuka WAJINGA.
TANZANIA kwa sasa kupitia utitiri wa VYUO VIKUU ni wazi inazalisha WASOMI wengi.Idadi kubwa sana ya hao WASOMI wanatoka FAMILIA MASIKINI SANA zilizodhani zikiuza Raslimali zake kwa ajili y Kuwasomesha Watoto wao mwisho wa siku zitafanikiwa .Masikini Watoto wao wamesoma tena wapo waliofaulu vizuri lakini ndio hivyo Nafasi za Ajira ni za kugombania na Watoto wa MATAJIRI na Wenye Uwezo . Sehemu kubwa wa Waliopata hizo AJIRA ni ya Watoto wa Matajiri na wenye uwezo.
Baada ya Watoto wa Masikini kukosa AJIRA tayari wakaingiwa na UJINGA tena UJINGA MKUBWA wa KUWASIFIA Watu wenye Kazi zao Uwezo wao wakiamini kufanya hivyo kutawasaidia kupata AJIRA.Masikini watoto wa Masikini waliosoma lakini wakaamua kuwa WAJINGA kwa Makusudi wamejaa Mitandaoni kuwasifia VIONGOZI wa VYAMA na SERIKALI wanaokula KEKI ya TAIFA huku Wazazi wao huko VIJIJINI na wao wakiendelea kupambana na UMASIKINI usiokwisha toka Mwaka 1961.
Ukitaka kuwajua vizuri WASOMI hao Waliogeuka WAJINGA ni hawa MACHAWA.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Dkt. Dyaboli amesema yote akamaliza kwenye kitabu chake cha Wasomi Wajinga. Kitafute ukisome ukiweza kaka. Kina madini adimu sana
IMG-20231213-WA0009.jpg
 
Back
Top Bottom