Umasikini ni mbaya: Mtoto wa miaka 9 achomwa moto kwa tuhuma ya kuiba karanga Shinyanga

Bravo snr

Senior Member
Aug 16, 2020
182
472
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshilikilia mwanamke aliyejulikana kwa jina la Christina Mwagi (29) kwa tuhuma ya kumjeruhi kwa kumchoma moto sehemu mbalimbali za mwili wake mtoto wake mwenye umri wa miaka 9 akishirikiana na mme wake (baba wa kambo) Yohana Michael (34) kwa tuhuma za kuiba karanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Februari 7,2021 majira ya saa saba mchana katika kijiji na kata ya Usule wilaya ya Shinyanga.

Amesema Peter Mahona (45) ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Usule aligundua mtoto huyo wa kike mwenye umri miaka 09 ambaye ni mwanafunzi darasa la tatu katika shule ya msingi Usule kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na moto sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Aliyetekeleza tukio hilo Christina Mwagi ambaye ni mama mzazi na Yohana Michael ambaye ni baba wa kambo”,amesema Kamanda Magiligimba.

Amesema chanzo cha mtoto huyo kuchomwa moto sehemu mbalimbali za mwili wake ni mtoto huyo kuiba karanga.

Ameongeza kuwa madhura anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto kwa Jeshi la polisi ili kukomesha vitendo hivyo.
 
Mimi ndio ningekuwa baba wa huyo mtoto, nasubiri hao watuhumiwa wamalize kifungo chao, wakirudi tu uraiani, nachinja kama kuku wa kizungu , madafaka’s!!!!!
 
Wizi ni jambo baya sana,
Ila kuchoma mato kwa sababu ya wizi haikubaliki
Mtoto aibe karanga apeleke wapi? Karanga hizo huyo mtoto amekula tu, sasa mtoto ananjaa, asionje karanga tena zilizopo kwao? Mtoto wa miaka tisa anaweza akala punje ngapi unafikiri? Sema ndio kama anayosema mtoa mada, umasikini mbaya sana, hii serikali tupambane kutokomeza umasikini jamani.., daaah
 
Nikweli, mtoto hizo karanga alitafuna tu. Ila kwakuwa umasikini unafilisi hata uwezo wa kufikiri ndo maana wamefanya hayo mambo ya ajabu
 
Mh!nimeona video kamuunguza kweli mpaka huruma.
Sijui huwa kuna watu wanapata kichaa cha muda au vipi.
Mwanao wa kumzaa umuunguze namna hiyo kisa karanga hapo ukutwe kaponzwa na mumewe kisa tu anamhudumia akaona ngoja amfurahishe.
Wanawake tujishughulishe jamani unaweza kuta kafanya yote haya kisa tegemezi mume asichukie bora amwadhibu vibaya mwanae kwasababu ya karanga alizoleta mume.
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshilikilia mwanamke aliyejulikana kwa jina la Christina Mwagi (29) kwa tuhuma ya kumjeruhi kwa kumchoma moto sehemu mbalimbali za mwili wake mtoto wake mwenye umri wa miaka 9 akishirikiana na mme wake (baba wa kambo) Yohana Michael (34) kwa tuhuma za kuiba karanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Februari 7,2021 majira ya saa saba mchana katika kijiji na kata ya Usule wilaya ya Shinyanga.

Amesema Peter Mahona (45) ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Usule aligundua mtoto huyo wa kike mwenye umri miaka 09 ambaye ni mwanafunzi darasa la tatu katika shule ya msingi Usule kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na moto sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Aliyetekeleza tukio hilo Christina Mwagi ambaye ni mama mzazi na Yohana Michael ambaye ni baba wa kambo”,amesema Kamanda Magiligimba.

Amesema chanzo cha mtoto huyo kuchomwa moto sehemu mbalimbali za mwili wake ni mtoto huyo kuiba karanga.

Ameongeza kuwa madhura anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Magiligimba anatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto kwa Jeshi la polisi ili kukomesha vitendo hivyo.
Tangu jamaa yangu aniambie amepata house girl toka Chato mwaka huu nimeamini hii mikoa hata ipendelewe vipi haiwezi kutoboa
 
Back
Top Bottom