Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,080
- 1,448
UMASIKINI NI DHIKI,
Umasikini ni dhiki, kila siku mashakani,
Na tena hathaminiki, mtu kuwa masikini,
Fukara hana rafiki, humtenga majirani,
Ni dhiki umasikini, Umasikini ni dhiki..
Ukiwa hauna kitu, nani atakutamani,
Watakudharau watu, watakushusha thamani,
Heshima ipo kwa vitu, hana hadhi masikini,
Ni dhiki umasikini, unasikini ni dhiki..
Masikini hana jema, wala mawazo mazuri,
Ndivyo watu hisema, heti hawezi fikiri,
Umasikini ni kilema, je kwa mtu fakiri,
Ni dhiki umasikini, Umasikini ni dhiki..
Matajiri wanaona, fukara hana akili,
Masikini hana mana, tena ni mtu dhalili,
Ikiwa pesa hauna, ninani atakujali,
Ni dhiki umasikini, umasikini ni dhiki..
Kwenye vikao vya ndugu, masikini hana neno,
sio leo toka tangu, wasema hana maono,
Umasikini ni chungu, iliojaa sonono,
Ni dhiki umasikini, umasikini ni dhiki...
Maisha huvurugika, ikiwa hauna pesa,
Ndoa nyingi huvunjika, hata kwa dogo makosa,
Mambo yatanyooka, Ndugu utafute pesa
[emoji2398]Ibn kimweri.
ramadhanikimweri7@gmail.com
Moshi - Tanzania.