Elections 2010 Umafia wa CCM sasa ni dhahiri zaidi

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
CCM imezidi kujidhihirisha zaidi kama chama kinachoongoza kwa kufuata siasa za Umafia. Mfululizo wa viroja vya CCM vya hivi karibuni vinatoa picha ya wazi bila kubakiza shaka yoyote.

Baada ya jaribio la Makamba la siasa za majitaka ya Ngono kupuuzwa na wapiga kura na ku-backfire vilivyo kuwarudia wao wenyewe, sasa CCM wameendelea na mhimili wao mkuu wa Umafia wa kisiasa kutangaza sms za hisia za vita. Shimbo alianzisha hili na sasa limeunganishwa barabara na SMS hizo za kimafia.

Msururu wa vitendo vya kimafia vya CCM dhidi ya wananchi ni mrefu na ulianzia siku nyingi ikiwemo kitendo cha kujaribu kuhusisha kifo cha Chacha Wangwe na CHADEMA. CHADEMA wamejitahidi sana kuirudisha CCM kutoka siasa za maji taka kuwa siasa za kutangaza sera na kulinda maslahi ya Tanzania na kuendeleza nchi. CHADEMA walimudu umafia wa CCM kuhusu kifo cha Chacha Wangwe, pia wamemuda umafia wa siasa za CCM za Ngono, sasa limekuja hili la sms za kimafia.

Umafia ni fani ya CCM na tunajua hawataishia hapo hadi umafia huo utaingia kwenye sanduku la kupiga kura. Na CCM watataka kulazimisha kutangazwa mshindi wa kiti cha uraisi anayetarajiwa kushindwa badala ya Dr. Slaa ambaye amekubalika kwa Wananchi. CCM imekuwa sasa si chama cha siasa bali ni kikundi cha wanyang'anyi.

Lakini nguvu ya umma itaushinda umafia huu wa CCM na Dr. Slaa atakuwa rais wa awamu ya tano kwa uamuzi halali wa wananchi kupitia sanduku la kura.
 
..... Kazi iko tusubiri lakini tukipiga kura sahihi.... Mungu atakuwa mwenye haki.... Hatakubali tena ushindi wa kimbunga huku ukiwa wa wizi.... Hatakubali usemi wa kuwa tutatawala daima na milele au ushindi daima au ushindi ni lazima.... Wakati yeye mungu ndiye atawalae milele peke yake... Yetu macho
 
hivi kama ccm inakubalika na wananchi mahangaiko yote ya nini! si wasubiri tu huo ushindi jue, wanahangaika na vikao vya usiku na mchana wa kazi gani!
 
hiyo ni kujihami tu wala hawana lolote hawa wameshaishiwa sera ndo maana mkuu wao amebakia kuahidi tu, hata hajui atapata wapi pesa, mtu waajabu kweli huyu, haamini hata makada wake, anaamini familia yake na ya makamba, lakini kura anataka zetu, mwaka huu wake
 
Too much complain

Isn't it obvious? Why should people keep silent when thuggish things are done by ccm? Is it a sin to speak out? ccm* acts like and is an organisation run by a bunch of crooks. Nothing more, nothing less. They are playing a dirty and dangerous game, dangerous to themselves, I would say, as they are playing around with minds of intelligent people who will see through the ploys and vote against it, come October 31!

* This is not a misspelling.
 
Mimi hii sms imeniharibia siku yangu, maana imeingia saa 11 alfajiri nikijiandaa kwenda kanisani! Nilihangaika sana kujaribu kupiga simu kwenda namba hiyo, lakini nilijibiwa namba hiyo haipo! Jamani ni nini hiki! Nadhani tuzidi kumuomba Mungu atuepushe na hili DUDE a.k.a CCM!
 
Mwenyezi Mungu kwenye utukufu wake alituasa yafuatayo:-

"ISAIAH 54:17 No weapon formed against you shall prosper, and every tongue which rises against you in judgment you shall condemn. This is the heritage of the servants of the LORD, and their rightness is from ME." Says the LORD."


Tumwamini Mwenyezi Mungu atasawazisha hii dhuluma ya CCM na JK wake hivi karibuni na sote tutastaajabia mno.
 
Tutashinda na zaidi ya kushinda tarehe 31 oct kwani aliyeko upande wawanyoge ni mkuu kuliko aliye upande wa mafisadi.
 
Poleni na harakati za kuikomboa nchi yetu!
Leo napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%. Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa.

Majid kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.

Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao.

Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya salva rweyemamu na mindi kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu.

Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; Maharage Chande na edgar masatu wanafanya kazi kwa karibu na Nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali Kubenea. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.

Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa CCM hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi.

Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya TISS. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu.


Usiniulize nimeikwapua wapi?
 
Kwa kweli inasikitisha,hivi ndo Kikwete ameamua iwe hivyo?ameamua kuwasaliti watanzania.This is too much,hakuna amani pasipo haki,ya nini kuendelea kusema kuwa Tz tuna amani wakati ni ya kinafiki?Haiwezekani watu wachache watuamulie viongozi kwa manufaa yao halafu tukipinga wanasema tunahatarisha amani.Tunahitaji amani ya kweli inayotokana na haki na si vitisho.Tanzania tuna amani mpaka sasa hivi kwa sababu watu walikuwa hawajui madudu yanayofanywa na viongozi wachache,walikuwa hawajui kupembua propaganda za ccm,lakini sasa wanajua mbivu na mbichi.Amani inayohitajika sasa si iliyo kwenye misingi ya ujinga wala hofu,bali katika misingi ya haki na uwazi.
 
Hawa jamaa wana nini mpaka watake kurudi madarakani kwa nguvu zote hizo..??
Ila Mungu ni mwema...
 
Too much complain

Episodes connects dots to complete the story about dirty games CCM is playing. Democracy is fairness not forcing getting to power at whaterver cost. Citizens need to decide for themselves not otherwise.
 
"If you think too much about being re-elected, it is very difficult to be worth re-electing."
 
Back
Top Bottom