Umaarufu wa Marekani barani Afrika washuka huku wa China ukiongezeka

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
78
155
无标题.jpg
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Shirika la Uchunguzi wa Maoni la Marekani Gallup umebaini kuwa umaarufu wa Marekani umeshuka barani Afrika, huku umaarufu wa China ukiongezeka.

Utafiti huo uliofanywa katika nchi 36 za Afrika unaonesha kuwa, umaarufu wa Marekani barani Afrika kwa mwaka 2023 ni asilimia 56, na umepungua kwa kasi zaidi ambazo ni asilimia 29, 21 na 14 mtawalia katika nchi tatu ikiwemo Uganda, Gambia na Kenya, na ulikuwa mdogo zaidi nchini Libya na Somalia na kuwa asilimia 23 na 25 mtawalia.

Wakati huo huo umaarufu wa China barani Afrika kwa mwaka 2023 uliongezeka kwa asilimia 6 ikilinganishwa na mwaka 2022 na kufikia asilimia 58.

Sababu za mabadiliko hayo zinaweza kuonekana kutokana na kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika. Rais Felix Tshisekedi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyekuwa ziarani nchini Ufarasan aliviambia vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa, Waafrika hawaelewi kwa nini nchi za Magharibi hupenda kufundisha nchi zao namna ya kufanya, haswa kuhusu haki za binadamu. Ikilinganishwa na nchi za Magharibi, kurokana na jinsi inavyoshughulikia mambo ya Afrika China inakaribishwa zaidi, kwani hailazimishi matakwa yake kwa nchi hizo.

Tarehe 30 mwezi uliopita, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema katika mkutano wa kilele wa maendeleo uliofanyika nchini Kenya, kuwa Benki ya Dunia na nchi za Magharibi zimekuwa zikitoa fedha kwa kile kinachoitwa “kujenga uwezo” barani Afrika, lakini zimepuuza kabisa miundombinu muhimu ikiwemo umwagiliaji na reli, lakini China ni moja ya nchi chache zinazosaidia nchi za Afrika kuendeleza miundombinu.

Kwa muda mrefu, China imefanya ushirikiano na nchi za Afrika kwa kufuata kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani, na kutendana kwa udhati na urafiki. Katika nyanja za biashara, China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara barani Afrika kwa miaka 12 mfululizo, thamani ya biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kutoka zaidi ya dola bilioni 10 za kimarekani mwaka 2000 hadi zaidi ya dola bilioni 280 za kimarekani mwaka 2023, na kuongezeka kwa mara 28.

Katika upande wa miundombinu, makampuni ya China yametekeleza idadi kubwa ya miradi ya miundombinu barani Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), makampuni ya China yamejenga au kurekebisha zaidi ya kilomita 10,000 za reli na karibu kilomita 100,000 za barabara, kujenga karibu bandari 20, zaidi ya vituo 80 vya umeme, bustani 25 za viwanda, na zaidi ya miradi 500 ya ushirikiano ya kilimo barani Afrika.

Katika ushirikiano wa uwekezaji, ingawa China ilichelewa kuanza kuwekeza barani Afrika, lakini ilipofika mwishoni mwa mwaka 2022, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani humo umezidi dola bilioni 47 za kimarekani, na kuwa nchi ya nne duniani kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika, na hadi sasa zaidi ya makampuni 3,500 ya China yamewekeza barani Afrika.

Mafanikio haya ya ushirikiano yamezifanya China na nchi za Afrika kuwa washirika wa maendeleo wanaonufaishana.
 
Hakika wawekezaji wa kichina ni wengi sana huku mtaani maana wamewekeza mashine za kamari kila mahali ni kwenye nyumba za ibada tu hawajaweza kuweka hizo mashine zao.
 
Ukiniuliza kati ya China na mataifa mengine ni nani awe super power wa dunia, bora dunia iwe chini ya Korea Kasikazini mara elfu kuliko dunia kuwa chini ya Mchina!

Ninazo sababu lukuki za kusema hivo, Wachina ni wabaguzi kinoma na wanapenda kusujudiwa saana yaani

Walioajiriwa na kampuni za kichina nadhani ni mashahidi aisee
 
Back
Top Bottom