Umaarufu wa CHADEMA waongezeka maradufu

Umaarufu wa CHADEMA waongezeka maradufu

chadema inafaidi na matangazo ya Bure , kwa sasa wamepata promo ya nguvu sehemu zote walizo pita wakubwa ambapo Magufuli anapiga kampeni za chadema Kigoma ma waziri mkuu yupo mbeya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_1500316484249.jpg
 
Na hiki ndicho kinachouangusha upinzani. Yaleyale ya mtoto mdogo ana kitambi cha kwashakoo, mzazi anasema "mtoto kopiraiti huyu, kama baba yake." Ni maradhi, sio afya njema.

Huo "umaarufu" unaoongelea ni katika lipi hasa? Kama ni kamata kamata ya wapinzani haijaanzia kwa akina Mashinji. Huko nyuma zilishafanyika jitihada za kutaka kuvifuta baadhi ya vyama vya upinzani kwa tuhuma kuwa ni vya kigaidi. Kuna watu wameshapoteza maisha yao kwa kushiriki maandamano ya vyama hivyo, damu ambayo leo baadhi yenu "mnaikebehi" na hoja za "kupanda umaarufu wa Chadema."

Tofauti kati ya zama hizo na sasa ni kwamba Chadema ilikuwa na ajenda ya kuwapigania walalahoi, na kwa hakika ilikuwa na ufanisi kama sauti ya wanyonge, na mbadala stahili wa CCM. Hivi leo Chadema inasimamia nini? Kama inabidi Mashinji akamatwe ndo ajulikane, basi mna matatizo makubwa mno.

Mkitaka umaarufu usio wa kufikirika bali utakaowawezesha kuingia Ikulu mwaka 2020 basi waonyesheni Watanzania kuwa mpo kwa ajili yao, ninyi ni bora kuliko CCM, na mtaipeleka Tanzania inapostahili kuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maneno lundo lakini hoja kibaba , ukiacha awamu hii ya 5 iliyojaa viongozi waoga wa siasa huru , kuna awamu nyingine iliwahi kuvunja katiba kwa kukataza siasa za majukwaa kama sheria ya nchi inavyoelekeza ? Unataka ajenda zetu tuzielezee wapi kama si majukwaani ?

Umeishaharibiwa na siasa za makinikia , endelea kusubiri Noah yako .
 
Katika mambo yanayoikwamisha CHADEMA ni kuaminishana ujinga na kuanza kuushabikia.
Hivi nani hajaona matokeo ya hizi chaguzi za marudio za serikali za mitaa zilizofanyika juzi???
Chama kinahitaji kuweka mikakati inayoweza kupimwa na kuthibitishwa na chaguzi.
Kufarijiana bila mikakati ni kujidanganya mwenyewe.
 
Iko hivi, zile kura milioni 6 ziko palepale. Na wale wenye milioni 8 kuna nyingi ambazo zimepungua kutokana na matatizo yaliyoletwa kwenye ajira zao, ukosefu wa nafasi za kusoma kwa kunyimwa mikopo, biashara zao kuharibiwa na sera mbovu, maonevu na matumizi mabaya ya Polisi nk nk. Kura hizi zinazopungua zinaenda kule kwenye 6.
Sasa kuna zile kura zaidi ya milioni 4 ambazo hazikutumika 2015 kwa sababu hawakuwa wanaona umuhimu wa kupiga kura kutokana na matumizi makubwa ya vitisho vya dola, media kutumika vibaya hata kuletewa mizengwe kwenye mchakato na kuona kama kupiga kura ni upotevu wa muda tuu, hizi 2/3 lazima ziende mahali pake yaani kule kwenye 6.
Baada ya hapo jiulize kama uchaguzi unakuwa huru na haki matokeo yanakuwaje? Kwanza 2015 mumshukuru sana Kinana na Nape kwa kufanya juhudi za ziada ingawa leo mnawaona hawana maana (tabia za shetani kukosa shukrani) pia muwaenzi sana Lubuva, Jecha na Wakurugenzi (Returning officers) wasio waaminifu kwa kazi kubwa waliyo wafanyia
Umefuatilia matokeo ya chaguzi za serikali za mitaa ya juzi.Tuache kujifariji uongo wakati chama kinafanya vibaya.
 
Na hiki ndicho kinachouangusha upinzani. Yaleyale ya mtoto mdogo ana kitambi cha kwashakoo, mzazi anasema "mtoto kopiraiti huyu, kama baba yake." Ni maradhi, sio afya njema.

Huo "umaarufu" unaoongelea ni katika lipi hasa? Kama ni kamata kamata ya wapinzani haijaanzia kwa akina Mashinji. Huko nyuma zilishafanyika jitihada za kutaka kuvifuta baadhi ya vyama vya upinzani kwa tuhuma kuwa ni vya kigaidi. Kuna watu wameshapoteza maisha yao kwa kushiriki maandamano ya vyama hivyo, damu ambayo leo baadhi yenu "mnaikebehi" na hoja za "kupanda umaarufu wa Chadema."

Tofauti kati ya zama hizo na sasa ni kwamba Chadema ilikuwa na ajenda ya kuwapigania walalahoi, na kwa hakika ilikuwa na ufanisi kama sauti ya wanyonge, na mbadala stahili wa CCM. Hivi leo Chadema inasimamia nini? Kama inabidi Mashinji akamatwe ndo ajulikane, basi mna matatizo makubwa mno.

Mkitaka umaarufu usio wa kufikirika bali utakaowawezesha kuingia Ikulu mwaka 2020 basi waonyesheni Watanzania kuwa mpo kwa ajili yao, ninyi ni bora kuliko CCM, na mtaipeleka Tanzania inapostahili kuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli tupu.
 
Katika mambo yanayoikwamisha CHADEMA ni kuaminishana ujinga na kuanza kuushabikia.
Hivi nani hajaona matokeo ya hizi chaguzi za marudio za serikali za mitaa zilizofanyika juzi???
Chama kinahitaji kuweka mikakati inayoweza kupimwa na kuthibitishwa na chaguzi.
Kufarijiana bila mikakati ni kujidanganya mwenyewe.
Hivi katika uwanja ambao siasa anafanya Magufuli na Polepole tu , matokeo ya uchaguzi yanaweza kuakisi kitu gani ?
 
Kinapata umaharufu siku hadi siku yapo wamekataza mikutano ya kisiasa
 
Uchunguzi wangu umebaini kwamba baada ya jeshi la polisi kutii maagizo ya ccm , ya kukamata na kuwashughulikia wabunge na viongozi wote wa CHADEMA nchi nzima , umaarufu wa chama hiki umezidi kupanda kwa kasi ya ajabu.

Kukamatwa kwa Dr Mashinji huko Nyasa kumeisambaza zaidi Chadema mpaka vijiji vya mbali kama Nkaya , Nsungu na Ilela kiasi cha kutishia uhai wa ccm maeneo hayo.

Habari za kukamatwa kwa Lissu The Great , kumeifanya sasa dunia nzima kuujua kwa undani moto wa CHADEMA nchini Tanzania , kwa ujumla kukamatwa na kuhojiwa kwa makamanda kadhaa kama Lowassa , Kubenea , Mdee na wengine kote nchini kumeipaisha zaidi Chadema .

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .
Ndio Kiki iliyobaki na wanayoipenda. Lakini inachuja haraka kama alivyochuja Harmorappa.
 
Uchunguzi wangu umebaini kwamba baada ya jeshi la polisi kutii maagizo ya ccm , ya kukamata na kuwashughulikia wabunge na viongozi wote wa CHADEMA nchi nzima , umaarufu wa chama hiki umezidi kupanda kwa kasi ya ajabu.

Kukamatwa kwa Dr Mashinji huko Nyasa kumeisambaza zaidi Chadema mpaka vijiji vya mbali kama Nkaya , Nsungu na Ilela kiasi cha kutishia uhai wa ccm maeneo hayo.

Habari za kukamatwa kwa Lissu The Great , kumeifanya sasa dunia nzima kuujua kwa undani moto wa CHADEMA nchini Tanzania , kwa ujumla kukamatwa na kuhojiwa kwa makamanda kadhaa kama Lowassa , Kubenea , Mdee na wengine kote nchini kumeipaisha zaidi Chadema .

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .
😀😀😀 mnapenda sana kujifariji vijana
 
CCM mwisho wake umefika, hawana Sera, kilicho baki ni kutumia mabavu, Ila siku IPO tutawazika tuu hata mtape tape, kaburi li wazi linawasubiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom