Ulokole umekuwa ajira rasmi?! Serikali mpo wapi?

Ulokole umekuwa ajira rasmi?! Serikali mpo wapi?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,723
Watu wanatapeliwa kipumbavu, Serikali inahangaika na mambo mengine yasiyo na msingi

Mtu anachukua unga wa COLA anachanganya na maji na kujaza kwenye chupa za maji safi, na kuweka lebo kuwa ni damu ya Yesu ,anauza kwa chupa MOJA hadi kiasi cha Laki 1,

Biashara za kikabaila zinafanyika ,Serikali mpo wapi, ? Haya madhehebu yanayojiita ya Kilokole, yanayoibuka kama UYOGA kila siku ,kwanini msiyafutilie mbali,kwanini msiweke REGULATION zitakazowabana hawa matapeli wanaoharibu UKRISTO na kuonekana ni UTAPELI

WATU wanauziwa chumvi, lesso, sabuni, maji , wanaambiwa yana upako ,wanauziwa hadi laki 1.

Na hawa matapeli wanaoibuka na kujiita MANABII,MITUME ,WAFALME ,WACHUNGAJI .

Serikali mpo wapi? Msijifiche kwenye kichaka kuwa Serikali haiingilii dini, mbona yule tapeli NABII TITO mlimdhibiti,iweje hawa kina Gwajima, Mwingira ,Mwamposa, Malisa, N.k wanatamba tu na kuwaibia watu.

MKISHINDWA KUDHIBITI ,BASI BWANA MUNGU ATAFANYA KAZI YAKE ,

Wachungaji waongo wa Israeli

1Neno la BWANA likanijia, kusema,

2Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?

3 Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 4Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. 5 Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyamamwitu, wakatawanyika. 6Kondoo wangu walitangatanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta. 7Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la BWANA; 8Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo wangu walikuwa mateka, kondoo wangu wakawa chakula cha wanyamamwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo wangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo wangu; 9kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la BWANA; 10 Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo wangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo wangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. 11Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo wangu, na kuwatunza.

FB_IMG_1552067589845.jpeg
FB_IMG_1551375364802.jpeg
FB_IMG_1551375361559.jpeg
 
Tunaangamia kwa kukosa maarifa.
.
Alafu mkuu mimi nazani ni shida nyingi za maisha kama maradhi n.k na hofu vimekuwa fursa kwa hao wapuuzi kuanzisha makanisa kila kukicha.
MBEYA ni hatari kuna makanisa kama matundu ya vyoo vya shule
Aisee ,watu wamegeuza matatizo ya wenzao ni fursa

,ona huyu ,akipata waumini wajinga kama 500

Ana bei gani, hajanunua V8 baada ya miezi 6

Ukiwaambia Enyi walokole mnaibiwa, na hao matapeli

Utasikia USIMGUSE MASIHI WA BWANA..

Pumbaff
FB_IMG_1552067589845.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais anasema Watanzania sio wajinga

Mimi nasema Rais wajinga wapo tena wengi

Unakuta prof. Doct ,au mwalimu, ananunua hii juis cola kwa laki had 2 anaambiwa ni damu ya Yesu itamkinga ,na anaamini

Hivi shetani Anaogopa juice cola?

Walokole acheni UTAPELI
FB_IMG_1551375364802.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi eti walokole, manabii, wachungaji wa bongo wanamnganga yule aliyefanya igizo la kumfufua mtu afrika ya kusini wakati wao ni wale wale kwa maigizo na mazingaombwe
Kwanza walianza kumtetea baadae wakamnanga,

Wakati huo Usanii hata GWAJIMA amewahi kuufanya, hata YouTube video IPO gwajima anafanya usanii wa kufufua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kazi ipo bora ingekuwa kibarua utalipwa kutwa taaaaaabu! inakuwa kazi lazima ukopwe siku 30 na kwakuwa leo ni siku ya wanawake hebu mwangalie upya ushiriki wenu wa makanisa kiasi mnakosa utii,unyenyekevu na majukumu kwa familia zenu.
 
Wacha kutaka kuwaingiza serikali mkenge. Nimekuelewa uliposema kuwa Mungu atafanya kitu hapo ndio umeongea. Jambo hili aachiwe Mungu pekee. Maana wakati mwingine unapog'oa magugu unaweza kuhani na ngano pia hivyo viache vikue pamoja mpaka siku ya mavuno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaonunua huo upako hawalalamikii bei, sasa wewe kinakuuma nini?
Acha kuingilia imani isiyokuhusu
 
Back
Top Bottom