Watu wanatapeliwa kipumbavu, serikali inahangaika na kina tundu lissu, na ujinga wa kina dudubaya,
Mtu anachukua unga wa COLA anachanganya na maji na kujaza kwenye chupa za maji safi, na kuweka lebo kuwa ni damu ya Yesu ,anauza kwa chupa MOJA hadi kiasi cha Laki 1,
Biashara za kikabaila zinafanyika ,Serikal mpo wapi, ? Haya madhehebu yanayojiita ya kilokole, yanayoibuka kama UYOGA kila siku ,kwanini msiyafutilie mbali,kwanini msiweke REGULATION zitakazowabana hawa matapeli wanaoharibu UKRISTO na kuonekana ni UTAPELI
WATU wanauziwa chumvi, lesso, sabuni, maji , wanaambiwa yana upako ,wanauziwa hadi laki1,
Na hawa matapeli wanaoibuka na kujiita MANABII,MITUME ,WAFALME ,WACHUNGAJI .
Serikali mpo wapi? Msijifiche kwenye kichaka kuwa Serikal haiingilii dini, mbona yule tapeli NABII TITO mlimdhibiti,iweje hawa kina gwajima, mwingira ,mwamposa, malisa, n.k wanatamba tu na kuwaibia watu.
MKISHINDWA KUDHIBITI ,BAS BWANA MUNGU ATAFANYA KAZI YAKE ,
Wachungaji waongo wa Israeli
1Neno la BWANA likanijia, kusema, 2Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo? 3 Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 4Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala. 5 Nao wakatawanyika, kwa sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyamamwitu, wakatawanyika. 6Kondoo wangu walitangatanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala kuwatafuta. 7Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la BWANA; 8Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo wangu walikuwa mateka, kondoo wangu wakawa chakula cha wanyamamwitu wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo wangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo wangu; 9kwa sababu hiyo, enyi wachungaji, lisikieni neno la BWANA; 10 Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo wangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo; nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo wangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. 11Maana, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi, nitawatafuta kondoo wangu, na kuwatunza.
View attachment 1041084View attachment 1041085View attachment 1041086
Sent using
Jamii Forums mobile app