Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,498
- 28,723
- Thread starter
- #61
Asante sana kiongoz, matapeli wamekuwa wengi sanaKwenye thread hii ngoja niwakumbushwe kisa kimoja katika mji wa Jonestown, Guyana America ambapo mamia ya watu walikufa kwa dini fake!
Tarehe 18/11/1978 yalitokea mauaji ya kihistoria huko Guyana,America katika mji wa Jonestown ambapo watu 918 walifariki dunia kwa kunywa cyanide.Mauaji haya yanajulikana zaidi kama Jonestown Massacre.
Habari hii inauzunisha na kushangaza vile vile.
Unaambiwa huyu mtumishi Bw. Jim Jones aliwaaminisha wafuasi wake kwamba kunywa cyanide ni tendo la kishujaa na ni ticket ya kwenda mbinguni.
Huyu jamaa aliteka akili na ufikiri wa watu. Unaambiwa kila kona aliweka walinzi katika jumba hilo waliokuwa na silaha za moto.Wafuasi walizidi kumiminika baada ya kuanza kufundisha watoto mashuleni na kutoa huduma mbali mbali za kijamii. Mpaka media na CIA zilimfahamu huyu bwana lakini zilibaki kumuangalia tu.
Waliomfuata walikula wali na mboga mwitu. Muda mwingine wali ulikuwa na funza wa kutosha waliouliza walipokea kichapo cha kutosha na kupelekwa kwenye kitengo maalum chakurekebisha tabia. Jamaa aliwafundisha watu waishi kijamaa wasaidiane kila kitu,hapakuwa na maskini au tajiri watu wote walipaswa kuwa sawa pia wapende mapenzi ya jinsia moja.
Wafuasi wengine walikuwa ni watu wasomi wenye uwezo mkubwa na maisha mazuri lakini mtego huu uliwanasa.
Siku ya tukio unaambiwa ilipigwa prayer ya hatari.Wazazi wakaambiwa wawanyweshe kwanza watoto wao cyanide. Wakawanywesha huku watoto wakitokwa mapovu na maji yenye damu midomoni.
Baada ya hapo akawaambia wazazi watoto wao wako sehemu ya raha mustarehe.Mzazi ukiona mtoto wako kafa na wewe unafanyaje?Wazazi nao wakanywa na kufa.Cha ajabu wakati yote haya yanafanyika kuliwa na recording kwenye tape aliyoiandaa mwenyewe. Kuna baadhi walikataa kunywa lakini walichomwa cyanide mikononi kwa sindano kwa lazima.Unajua baada ya hapa pastor huyu mwenye umri wa miaka 47 alifanyaje?Alijimwaga ubongo kwa kujipiga risasi kichwani.
Unaambiwa siku hiyo walikufa watu 918 kati ya hao 304 watoto.
Polisi na waandishi wa habari walipokaribia eneo hilo wakiwa kwenye helicopter walinusa harufu kali na waliona miili ya watu iliyokuwa imelala kifudi fudi mingi kama midoli.
Tunajifunza nini ?
Tuwe makini na utitiri wa dini kwani wengi sasa wanaanzisha dini wakiwa na nia ovu.Usikubali kuwa mtumwa. FIKIRI! Be sober !
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app