Ulokole umekuwa ajira rasmi?! Serikali mpo wapi?

Ulokole umekuwa ajira rasmi?! Serikali mpo wapi?

Hahahahaha... hatare

kanisa ni moja tu Katoliki Takatifu na La Mitume..
Hao ndio waanzilishi au mama wa hao walokole

Maana hao walokole na manabii wote matapeli ni zao la RC,hata ibada ya jumapili,kunywa pombe, x. Mass, easter paganism, zote hao manabii wanazitumia ,ukiwauliza hawana majibu, ila wamezitoa kwa mama yao RC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kweli matapeli wameongezeka kila siku. Serikali inawaangalia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Leso ya jero unauziwa laki 2 unaambiwa ina upako

Ukiwa na lesso za miatano miatano kama 1000 ukaziuza kila leso laki 1

Kila jumapili ukawa unauza lesso 1000 , bado hujanunua RANGE ROVER baada ya mwaka 1?

WATU WANALIA AJIRA HAKUNA ,WAKATI AJIRA KAMA HIZI ZIPO NDAN YA ULOKOLE,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leso ya jero unauziwa laki 2 unaambiwa ina upako

Ukiwa na lesso za miatano miatano kama 1000 ukaziuza kila leso laki 1

Kila jumapili ukawa unauza lesso 1000 , bado hujanunua RANGE ROVER baada ya mwaka 1?

WATU WANALIA AJIRA HAKUNA ,WAKATI AJIRA KAMA HIZI ZIPO NDAN YA ULOKOLE,

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hiyo Range Rover inauzwa bilioni ngapi? Maana kama utauza leso 1,000 kwa wiki na kwa bei ya 100,000/= kila moja hautahitaji mwaka mzima kununua hiyo Range Rover.
 
Wajinga ndio waliwao!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujinga ni complicated word.Wewe unawaita wajinga wakati wao nao wanakuona mjinga wewe usiyeona umuhimu wa kununua mafuta ya upako kwa laki Moja!!!!!!!!!! Vita ya nani mjinga ngumu kuimaliza Catholic wanawaona wasabato wajinga,na wasabato wanawaona wakatoliki wapinga,Waislamu wanawaona wakristo wala nguruwe wajinga,na wakristo wanawaona waislamu wajinga kifupi hakuna jaji duniani awezaye kijijini kesi ya nani mjinga!!!!Na hakuna Sheria yoyote duniani inayotoa tafsiri halisi ya mjinga ni nani na sifa zake ni vipi sababu Kila mtu ana akili machoni Pake mwenyewe!!! Mambo ya imani yaache tu kama yalivyo
 
W
WATU wanauziwa chumvi, lesso, sabuni, maji , wanaambiwa yana upako ,wanauziwa hadi laki 1.
WAJINGA ndio WALIWAO, hapo sioni sababu ya Serikali kubeba lawama, hao ni kama matapeli wengine wengi walioko mjini.
 
Hii biashara inalipa sana,, unanunua maji ya uhai ya 500 chupa 1000 inakuwa 500,000.

Zinapigwa neno na kumwagiwa upako zinauzwa 5000.

Hapo kila chupa faida ni 4,500 × 1000 = 4.5m
Bado sadaka, Bado kumtunza mtumishi etc

Jumapili moja ukikosa saana 20m. Hata Kempiski hawaingizi hizo kwa siku.
 
Hii biashara inalipa sana,, unanunua maji ya uhai ya 500 chupa 1000 inakuwa 500,000.

Zinapigwa neno na kumwagiwa upako zinauzwa 5000.

Hapo kila chupa faida ni 4,500 × 1000 = 4.5m
Bado sadaka, Bado kumtunza mtumishi etc

Jumapili moja ukikosa saana 20m. Hata Kempiski hawaingizi hizo kwa siku.
Halafu watu wanasema AJIRA hakuna,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kama una uhakika na hizi taarfa zako juu ya hawa watumishi wa mungu ambao hawalali wanakesha kuombea amani ya taifa hili, weka namba yako hapa na majina yako, tunatanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna yule wa Afrika kusini aliyesema amewahi kupiga selfie na Mungu alikuwa anamshutumu Askofu Lukau yule aliyefanya usanii wa kumfufua mtu kuwa hana uwezo huo na anamkufuru mungu. ninachojiuliza hapa kwanini serikali haiingilii kati haya mambo ili wachukuliwe hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kama una uhakika na hizi taarfa zako juu ya hawa watumishi wa mungu ambao hawalali wanakesha kuombea amani ya taifa hili, weka namba yako hapa na majina yako, tunatanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
Majina yangu na namba zikusaidie nn?

Wewe matapeli unawaita ni watumishi wa Mungu,

Pumbaff kabisa,

Nyie ndio mnawapa kiburi hao kina gwajima, mwingira ,mwamposa, billionare, n.k

Hao ni matapeli kama matapeli wengine

Ona tapel mwingine huyu ,

Wewe unawaita watumishi wa Mungu, hiv nan kawaroga
FB_IMG_1552067589845.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye thread hii ngoja niwakumbushwe kisa kimoja katika mji wa Jonestown, Guyana America ambapo mamia ya watu walikufa kwa dini fake!

Tarehe 18/11/1978 yalitokea mauaji ya kihistoria huko Guyana,America katika mji wa Jonestown ambapo watu 918 walifariki dunia kwa kunywa cyanide.Mauaji haya yanajulikana zaidi kama Jonestown Massacre.

Habari hii inauzunisha na kushangaza vile vile.
Unaambiwa huyu mtumishi Bw. Jim Jones aliwaaminisha wafuasi wake kwamba kunywa cyanide ni tendo la kishujaa na ni ticket ya kwenda mbinguni.

Huyu jamaa aliteka akili na ufikiri wa watu. Unaambiwa kila kona aliweka walinzi katika jumba hilo waliokuwa na silaha za moto.Wafuasi walizidi kumiminika baada ya kuanza kufundisha watoto mashuleni na kutoa huduma mbali mbali za kijamii. Mpaka media na CIA zilimfahamu huyu bwana lakini zilibaki kumuangalia tu.

Waliomfuata walikula wali na mboga mwitu. Muda mwingine wali ulikuwa na funza wa kutosha waliouliza walipokea kichapo cha kutosha na kupelekwa kwenye kitengo maalum chakurekebisha tabia. Jamaa aliwafundisha watu waishi kijamaa wasaidiane kila kitu,hapakuwa na maskini au tajiri watu wote walipaswa kuwa sawa pia wapende mapenzi ya jinsia moja.

Wafuasi wengine walikuwa ni watu wasomi wenye uwezo mkubwa na maisha mazuri lakini mtego huu uliwanasa.

Siku ya tukio unaambiwa ilipigwa prayer ya hatari.Wazazi wakaambiwa wawanyweshe kwanza watoto wao cyanide. Wakawanywesha huku watoto wakitokwa mapovu na maji yenye damu midomoni.

Baada ya hapo akawaambia wazazi watoto wao wako sehemu ya raha mustarehe.Mzazi ukiona mtoto wako kafa na wewe unafanyaje?Wazazi nao wakanywa na kufa.Cha ajabu wakati yote haya yanafanyika kuliwa na recording kwenye tape aliyoiandaa mwenyewe. Kuna baadhi walikataa kunywa lakini walichomwa cyanide mikononi kwa sindano kwa lazima.Unajua baada ya hapa pastor huyu mwenye umri wa miaka 47 alifanyaje?Alijimwaga ubongo kwa kujipiga risasi kichwani.

Unaambiwa siku hiyo walikufa watu 918 kati ya hao 304 watoto.

Polisi na waandishi wa habari walipokaribia eneo hilo wakiwa kwenye helicopter walinusa harufu kali na waliona miili ya watu iliyokuwa imelala kifudi fudi mingi kama midoli.

Tunajifunza nini ?
Tuwe makini na utitiri wa dini kwani wengi sasa wanaanzisha dini wakiwa na nia ovu.Usikubali kuwa mtumwa. FIKIRI! Be sober !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom