Ulizingatia nini na kujiridhisha mpaka ukaamua kufunga nae ndoa?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,959
12,234
Ulizingatia umri wako na wake, nidhamu, heshima na utii, uaminifu, upendo, hekima, busara, fedha, mali, kazi yake, hali na maisha ya familia yake au cheo chake...

Au ulizingatia siha na tabia njema, brain yake, IQ, elimu, rangi, dini, kabila, urembo, utanashati,sura, muonekano, umbo, kimo, sauti, ladha au ni baada ya kukamatwa ugoni na aidha mtoto wa watu mwanafunzi, alietoroka nyumbani kwao usiku na kuja kulala kwako, na kisha wazazi wake wakamshtukia na kukubambukia umuoe kabisa kabisa yaishe au wakupeleke mahakamani na mtoto mwenyewe ni mwanafunzi, kisha nawe ukapima kuliko ukachezee mvua 30 segerea bora umuoe tu hivyo alivyo?

Eti mpendwa, ulizingatia nini hadi leo hii mkawa familia iliyoimarika na kupendeza hivyo.

Usie na ndoa, si utulie tu ujifuze na kuchota uzoefu utakaokusaidia kuamua 🐒
 
Hapo sio one size fit for all mkuu ni wewe tu kuwa na vigezo vyako .. kikubwa sana ujue akili yake na mindset ndio italea watoto wako sasa nawewe kama unakimbilia tu rangi na ukubwa wa kule Nyuma .. yakhe acha ninywe maji
 
Back
Top Bottom