tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,804
- 18,231
Hodi humu jamvini wana MMU,
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha. Najua mnahangaika na utafutaji wa maji na mkate kwa familia wakati huu.
Kwa sababu ya suala la kuolewa kuwa gumu siku hizi binti akiolewa anajiona kama amepata degree (Hons) ya first class. Siyo siri ukimpa uchaguzi binti yako kama umlipie fedha asome degree yoyote au aolewe, bila kuchelewa wala kupepesa macho atachagua kuoelewa. Hasa ikiwa huyo mwanaume anayemchumbia ni mtoto wa kishua, utakuta amejiozesha mwenyewe bila mahari!

Juzi nilikuwa natatua kesi ya binti wa kidato cha III mwenye umri wa miaka 17 aliyeamka usiku wa saa 5 na kumfuata mwanaume mwenye umri wa miaka 23 mtaa wa pili. Huyu binti anaishi na mama wa kambo anayefanya kazi baa. Kwa kawaida, mama hurudi kutoka kazini kuanzia saa 7 usiku. Sasa siku hiyo mama alirudi mapema kabla ya saa 7 akakuta binti ametoka. Arobaini za binti zikawa zimefika.
Huyu binti hulala chumba cha uani, hivyo nafikiri ulikuwa ndiyo mchezo wake wa kila siku. Dada yake aliacha shule akiwa Kidato cha II akaolewa na lofa mmoja asiyekuwa na mbele wala nyuma. Sasa hivi anajishughulisha na uuzaji wa mboga nyumba kwa nyumba. Mdogo wake naye anatamani kuacha shule akaolewe. Hajajifunza chochote kutokana na makosa ya dada yake. Wanawake wa kizazi hiki ni kama nyani, hawajatulia hata kidogo. Hivi nyie mabinti wa kisasa mna nini lakini?
Ndoa imekuwa kama kilele cha mafanikio ya msichana. Huu ukuta unahitaji kubomolewa, hili ni gereza la kuyafunga maono ya msichana. Kuolewa ni maono ya chini kabisa, msichana unaweza kuwa na ndoto kubwa zaidi ya hii; ota ndoto kubwa zaidi.