FLASH HIDER
JF-Expert Member
- Jul 13, 2012
- 397
- 501
- Thread starter
-
- #81
Kwani si inasemekana marekani anashiriki kwa kiasi kikubwa sana kufanya wizi wa madini congo,kimetokea nini mpaka akaamua kumbadilikia m23(rwanda) aliyeko on ground kupiga mzigo?
Mkuu Flash Hider umenifurahisha sana.Ila ntakusumbua wakati mwingine kuhusu biashara ya madini huko.Nafikira kuja huko hali ikitulia.
nimepitia mkuu na nashukuru kwa majibu yako
nasikia nkunda alipandikizwa na kinamseveni na kagame kwa ajili ya kupora mali ya drc kulipia ahadi walizopeana na kabila, na kunatetesi hawa ndo walimuua huyu mzee?
hii vita haiiishi labda DRC waishiwe madini mkuu!Uki-link chanzo cha mgogoro ambao ulipelekea mauaji ya Kabila baba, ni wazi kuwa Rwanda na hata Uganda wanahusika. Hebu jaribu kusoma historia ya Nkunda utagundua kuwa ni Mnyarwanda aliyezaliwa DRC. Kuapnikizwa kupo wazi kabisa hakuihitaji research ni logical thinking tu.
Kwanza hongera kwa kazi nzuri ingawa ninajiuliza kama ni mfanyabiashara wa kawaida kwa sababu ya uelewa waku upo juu. Ninaomba kujua katika hali hiyo ya mgogoro kuna ndege za abiria zinazotua Goma kutoka miji au nchi nyingine? Na kwanini DRC historia ya mapinduzi na mauji ya viongozi tangu miaka hiyo ya kina Lumumba kama sikosei?
hii vita haiiishi labda DRC waishiwe madini mkuu!
Tanzania yangu haijaishiwa wazalendo hongera mkuu FLASH HIDER kwa taarifa hizi binafsi nimenufaika..
Karibu kaka. Huku yaani tupo wengi kiasi kwamba masuala ya SUPU, CHAPATI, UGALI ni kama bongo. Uliza madereva hasa wa Azam wanaokuja mara kwa mara. Always sehemu yenye problems, there are opportunity.
Heshima kwako ndugu, na endelea na moyo huu huu, ASANTE SANA.
Ofcourse wanasema "Penye Mwamba Mgumu ndio Penye mafuta" Ni PM namba yako na e-mail tutakuwa tunachat mara mojamoja.
Nafikiri ingekuwa vyema kama ungeanza kwa kutueleza japo kwa kifupi unachokijua kuhusu mgogoro huo, ili kama kuna maswali basi yaanzie hapo.
Bwana Sixgates,
Suala moja ambalo ningependa watu wote waelewe ni kuwa ukweli DRC ina matatizo mengi kuanzia Political, Economical and Security. M23 ni sehemu ndogo sana ya tatizo la DRC. Mengi yanatakiwa yafanyike.
Nkunda ana uhusiano mkubwa na M23, na muda huo inasemekana Kagame anawasaidia M23; imekuwaje tena Nkunda awe under arrest huko Rwanda?Nkunda kwa sasa yupo under house arrest huko Rwanda. Ana uhusiano mkubwa na M23 kwani yeye andiyo mwanzilishi wa CNDP(The National Congress for the Defence of the People (kwa kifaransa Congrès national pour la défense du peuple) ambalo ndiyo chumbuko la M23. Hebu pitia uzi huu kwa ujumla nimejaribu kuelezea uhusiano wa M23 na NKUNDA LAURENT
Mdau hebu elezea ushiriki wa marekani katika mgogoro huu upoje? habari zilizopo ni kuwa kuna uhusika mkubwa wa mataifa ya kigeni hasa marekani. Interest kuu ni rasilimali zilizopo Congo (zaidi madini).Walimtumia Kagame akishirikiana na Mu7 kuharibu hali ya amani consistently ili waendelee kutimiza interest zao, lakini pia ushiriki wa tanzania katika kipindi hiki una mgongo wa Marekani.(Kwa kifupi Tanzania imetumiwa na Marekani)
Kagame hajatenda kadiri ya maelekezo ya marekani kwani naye amekuwa akichota rasilimali na kuijenga Rwanda na kufaidikia kuliko anayemtuma (hii pia inasemekana ndo chachu ya maendeleo ya haraka ya Rwanda). Hivyo Marekani anatumia JWTZ kuimaliza M23 yenye ufadhili wa Kagame na Mu7 kama njia ya kumshikisha adabu Rwanda. Inasemekana ziara ya juzi iliyowakutanisha kwa pamoja Obama na Bush hapa Tanzania ina nyayo za huu mgogoro. Hebu endelea kufunguka kuhusu hizi nilizoziita "inasemekana, inasemekana, inasemekana....."
Nkunda ana uhusiano mkubwa na M23, na muda huo inasemekana Kagame anawasaidia M23; imekuwaje tena Nkunda awe under arrest huko Rwanda?
Kuna tetesi kuwa banyamulenge wakishirikiana na m23 wanataka kuimega DRC vipande viwili ili watangaze taifa jipya la republic of kivu ili iwe kama ilivyo tokea kwa sudani hili liko vip?
Mkuu, kwa nyongeza tu historia ya DRC tokea uhuru wao pia ni sehemu ya tatizo. Swali langu ni kuwa DRC haijawahi kutulia tokea ilipopata uhuru, migogoro na mapigano yamekuwapo kwa miaka. Je kikosi cha UN cha wakati huu kina nini kipya cha kutoa matumaini kuwa sasa hatimaye DRC itatulia kimoja?