Uliza lolote kuhusu mgogoro ndani ya DRC hasa mapigano kati ya M23 na FARDC

FLASH HIDER

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
397
501
Ndugu zanguni hasa Watanzania,

Mimi ni mtanzania ninafanya biashara zangu huku DRC Goma kwa muda mrefu. Ninaishi hapa GOMA na nimekuwa nikisafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani ya DRC. Nimekuwa nikifuatilia mijadala kuhusu mgogoro wa M23 na serikali ya DRC, nimegundua watu wengi hawapo informed on what is going on.

Sasa kwa wale wenye swali au chochote wanachotaka kujua kuhusu mgogoro huu, mapigano yanayoendelea, na ushiriki na mapokeo ya WaKongo kuhusu JWTZ, mnaweza kuniuliza.

Nipo hapa kwa karibu miaka kumi na mbili sasa, bila sahaka nina kitu kipya ambacho huenda ninaweza kuwahabarisha.



----------------------------------------------------------------------------

HISTORIA KWA UFUPI ZA SIASA ZA CONGO, GOMA, M23 NA MAPIGANO YAO



---------------------------------------------------------------



---------------------------------------------------------------

BAADHI YA MASWALI NA MAJIBU KATIKA HII THREAD:-

A.


B.

C.


D.


E - "Maswali na majibu zaidi ndani ya thread"
 
Wananchi wa congo wanasemaje kuhusu mahusiano ya nchi yao na tanzania? Hasa baada ya kupeleka jeshi. Hebu tuambie je ni kweli Kabila ni sehemu ya tatizo? Maana zipo conspiracies kuwa yeye ni pandikizi.
 
Wananchi wa congo wanasemaje kuhusu mahusiano ya nchi yao na tanzania? Hasa baada ya kupeleka jeshi. Hebu tuambie je ni kweli Kabila ni sehemu ya tatizo? Maana zipo conspiracies kuwa yeye ni pandikizi.

Bwana Sixgates,

Tokea mgogoro huu uanze, wananchi wa DRC wamekuwa wakiomba sana Watanzania (JWTZ) waingilie kwani ilionekana wazi kuwa hili jeshi la UN lililopo na ambalo naambiwa limekuwepo kwa miaka karibu 14 limekosa uzalendo wa dhati wa kuisaidia DRC. Sababu kubwa ni kuwa majeshi yaliyokuwepo ni kutoka India, Bangredesh, Pakistan nk ambayo kimsingi hayawezi kuwa na uchungu wa rohoni wa matatizo yanayoipata DRC.

JWTZ limekuwa na hitoria nzuri katika DRC. Inasemekana Kikosi kimoja cha DRC likichofundishwa na JWTZ mwaka 1997 ndicho kinafanya vizuri kimapigano mpaka sasa. Siasa yetu inatajwa kuwa ni bora haina interest yoyote ndani ya DRC na Maziwa Mkaubwa kwa ujumla(hapa nisingependa kuingia kwenye malumbano ya kisiasa) Si hivyo tu, hata historia ya kuzikomboa Zimbabwe, Namibia, Msumbiji na kwingineko kunalipa jina kubwa JWTZ. Kwa ujumla wananchi wamekuwa na matumaini makubwa kuwa JWTZ kama lead army in this Operation litawasaidia hasa kupambana na M23. Tatizo nilaloliona ni namna ya ku-fulfil matumaini yote ya wana DRC.

Kuhusu Rais Kabila kuwa ni sehemu ya tatizo hilo binafsi ninalikataa. Najua amekuwa akibanwa sana na jumuiya ya Kimataifa kutatua mgogoro huu kwa njia ya kisiasa zaidi kuliko kivita. Wananchi wa kawaida hawawezi kuelewa hili. Amejitahidi sana hasa mwaka huu, ameimarisha JESHI kwa vifaa, mafunzo, kawapandisha vyeo baadhi ya makamanda, yote ni kuwaandaa kimapigano wanajeshi wake dhodo ya waasi. Wiki iliyopita ametoa hutuba kali na kueleza wazi wazi kuwa lililobaki ni vita tu, kitu ambacho ndiyo kinaendelea kwa sasa.

Suala moja ambalo ningependa watu wote waelewe ni kuwa ukweli DRC ina matatizo mengi kuanzia Political, Economical and Security. M23 ni sehemu ndogo sana ya tatizo la DRC. Mengi yanatakiwa yafanyike.
 
Kuanzia terehe 25 Oktoba mapigano mapya yameanza ambapo mpaka mchana huu taarifa zilizopo ni kuwa M23 wamekimbia maeneo yote na sasa wanaelekea BUNAGANA jirani kabisa na mpaka wa Uganda. Wananchi wanashangilia sana. Ujue hapa GOMA wananchi wamechoshwa sana na M23 kila siku tunafunga maduka na kukimbia huku na huku.

Saa hizi ni shangwe tupu, waendesha pikipiki wote wapo barabarani. Jana walifanya kitu ambacho hata mimi kilinigusa. Kila mwenye pikipiki (Boda boda) alinunua maji chupa moja (lita moja) na wote kwa pamoja walienda mpaka eneo la Kanyaruchina ambako majeshi ya Serikali yalikuwepo na kuwapatia maji hayo kama ishara ya kuwaunga mkono.
 
Leo asubuhi tumesikia kuwa mpaka sasa askari 7 wa Tanzania wamekufa huku kwetu tunajua mmoja tu, hebu tueleze ukweli.

Kwa nini nchi kubwa km kongo ishindwe vita na nchi ndogo km Rwanda unasemaje kuhusu hili.


Unafikiri vita ikiisha Tanzania ina fursa gani kiuchumi, ukizingatia kuwa bidhaa kutoka Tanzania kwenda Goma lazima zipite Rwanda iliyopandisha ushuru pia hakuna maelewano na Tz.

Je kuna njia nyingine kupitia Burundi kutokea Kigoma kwenda Kongo DRC na km ipo unashuri nini serikali yetu.
 
ok, ngoja niwape hili ingawa kwa ufupi

Mgogoro katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo "DRC") una historia ndefu. Tokea nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa Ubeligiji hapo tarehe 30 Juni 1960, haijawahi kushuhudia hali ya kiusalama ya muda mrefu. Migogoro isiyopata ufumbuzi w kudumu ilianza mara tu baada ya uchanguzi wa kwanza nchini humo uliomweka Patrice Lumumba kuwa Waziri Mkuu na Joseph Kazavubu kuwa Rais. Kutokana na matatizo mbalimbali ya kimtazamo baina ya Rais na Waziri Mkuu, Serikali hiyo mpya ilijikuta ikipinduliwa na Kanali Jopeph Mobutu hapo tarehe 14 Septemba 1960 ambapo wiki chache baadaye, Kanali Joseph Mobutu alimuua Patrice Lumbumba. Mara baada ya mapinduzi na kifo cha Lumumba, nchi hiyo ilishuhudia machafuko kwa vipindi mbalimbali kuanzia mwaka 1960-1964 ambapo mara zote majeshi ya Serikali yakisaidiwa na yale ya Marekani pamoja na askari wa kukodiwa kutoka Ulaya yalikuwa wakidhibiti machafuko hayo. Mwaka 1965, Mobutu ambaye alijipandisha cheo na kuwa Luteni Jenerali, alijitangaza kuwa ni rais rasmi. Tokea mwaka 1965-1977 nchi hiyo ilishuhudia hali ya utulivu kiasi ingawa ilikuwa inaendeshwa kimabavu katika utawala wa kidikteta chini ya Rais Mobutu. Mwishoni mwa mwaka 1990, Serikali ya rais Mobutu iliandamwa na upinzani mkubwa kutoka ndani na nje ya nchi ikilalamikiwa kwa kutofuata haki za binadamu, rushwa, matumizi mabaya ya mali za serikali nk. Mwaka 1991 hali ya kiuchumi nchini Zaire ilizidi kuwa mbaya ambapo ilifikia wakati wanajeshi waligoma kutokana na kutolipwa mishahara.

Mara baada ya mauaji ya Kimbari nchini Rwanda hapo mwaka 1994, nchi ya Zaire ilijikuta ipo katika mgogoro ambapo wahutu wengi waliokimbia Rwanda na kuingia Zaire walikuwa wanatumia makambi ya wakimbizi kujipanga na kufanya mashambulizi nchini Rwanda. Serikali ya Mobutu haikuwa inachukua hatua zozote kukabiliana na hali hiyo. Kitendo hicho kilileta uhasama baina ya Serikali ya rais Mobutu na ile ya Rwanda na Uganda. Kufuatia hali hiyo, Rwanda na Uganda zilikisaidia kikundi kilichojulikana kama "Alliance des Forces Démocratiques pour la Libération du Congo-Zaire (AFDL) chini ya Laurent-Desire Kabila kuishambulia Zaire.
Kikundi hicho kilianza kufanya mashambulizi na kuchukua miji mbalimbali ndani ya Zaire ambapo tarehe 20 May 1997, Rais Mobutu alikimbia nchi na bwana Laurent Desire Kabila akajitangaza kuwa rais na kubadirisha jina la nchi hiyo na kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mapigano haya ya kumuondoa Rais Mobutu madarakani hujulikana kama Vita kuu ya kwanza ya Kongo.
Mwaka mmoja baada ya kushika madaraka, rais Kabila alitangaza kuwaondoa washauri wake wote wa kijeshi kutoka nchi jirani zilizomsaidia kumuondoa rais Mobutu hasa Rwanda. Ikumbukwe kuwa wakati huo, Rais Laurent Kabila alikuwa na washauri wengi wa kijeshi kutoka Rwanda akiwemo Waziri wa Ulinzi wa Rwanda wa sasa Bwana James Kabarebe aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa Jeshi la Zaire mpya. Kitendo hicho cha kuwaondosha washauri hao kilifuatiwa na machafuko nchini humo ambapo watu wenye asili ya jamii ya Kitusi walianza kulengwa katika mashambulizi hayo. Hali hiyo ilizifanya nchi za Rwanda, Burundi na Uganda kuishambulia Kongo kwa kile kinachoelezwa kama kuwalinda watu wa jamii ya Kitusi. Nchi za Zimbabwe, Namibia na Angola zilipigana kuisaidia Kongo baada ya kuombwa kupitia Umoja wa Kimaendeleo wa nchi za Kusini mwa Afika (Southern African Development Community).

Nchi za Chad na Sudan nazo ziliingia vitani kuisaidia DRC baada ya kuombwa na Rais Kabila. Rais Kabila aliuawa tarehe 18 Januari, 2001 na mmoja wa walinzi wake aliyejulikana kama Rashidi Muzele, kwa namna isiyoeleweka vizuri hadi leo. Vita hiyo inayojulikana kama vita kuu ya pili ya Kongo au Vita Kubwa ya Afrika ilimalizika mwaka 2003 ambapo inakadiriwa kuwa jumla ya watu…..walipoteza maisha .
Baada ya kifo cha Rais Laurent Kabila, tarehe 26 Januari, 2001, Joseph Kabila (mtoto waLaurent-Desire Kabila) aliteuliwa na baadae kuchaguliwa kuwa rais wa DRC. Serikali ya Rais Joseph Kabila nayo ikajikuta inakumbwa na changamoto kubwa za migogoro. Tarehe 30 Desemba, 2006, liliundwa kundi la "The National Congress for the Defence of the People (kwa kifaransa Congrès national pour la défense du peuple, CNDP)chini ya Bwana Laurent Nkunda. Madhumuni ya kundi hilo yalidaiwa ni kulinda haki za Watu wa jamii ya Kitusi waliopo DRC. Januari, 2009, kundi hilo la CNDP liligawanyika ambapo tarehe 22 Januari mwaka huo huo, Nkunda alikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Rwanda ambapo yupo huko mpaka sasa. Tarehe 23 Machi, 2009, kundi lililobaki likiongozwa na Bosco Ntaganda lilisaini makubaliano na Serikali na lilijiunga katika Jeshi la Serikali. Makubaliano hayo yalidumu kwa kipindi cha miaka mitatu tu ambapo mwaka 2012, wanajeshi, wengi wao wakiwa ni wale waliokuwa wa NDP walijiondoa katika Jeshi la Serikali na kuunda kundi la M23 wakilalamikia kutotekelezwa kwa baadhi ya makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2009. Kundi hilo la M23 lilikalia eneo la Rutchuru ambalo linapakana na Rwanda na Uganda. Kiongozi wa kundi hilo alikuwa ni Bosco Ntaganda akisaidiwa na Sultani Makenga. Mwezi Mei, 2013 kulitokea mapigano kati ya makundi mawili ndani ya M23, lile linalomuunga mkono Bosco Ntaganda na lile linalomuunga mkono Sultani Makenga. Kundi lililokuwa linamuunga mkono Bosco Ntaganda lilizidiwa na kuamua kuvuka mpaka na kuingia Rwanda na Ntaganda akaamua kujisalimisha katika Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda. Kwa sasa wapiganaji hao wanaokariwa kuwa 682 wapo katika kambi maalum ya wakimbizi nchini Rwanda na Bosco Ntaganda yupo chini ya Mahakama ya Dunia ya Makosa ya Jinai(ICC) akishitakiwa kwa kwenda kinyume na haki za binadamu pamoja na mauaji ya raia.

Kundi la M23 lililobaki nchini DRC sasa linaongozwa na Sultani Makenga. Kundi hilo limeendelea kuukalia mji wa Rutchuru huku likisababisha madhara makubwa kwa jamii.
Tokea mgogoro wa DRC uanze, Umoja wa Mataifa umekuwa ukichukua hatua mbalimbali kujaribu kuleta hali ya amani ndani ya DRC. Ikumbukwe kuwa Katibu Mkuu wa Pili wa Umoja wa Mataifa Bwana Dag Hjalmar Agne Carl Hammarskjöld alifariki dunia tarehe 18 Septemba 1961 kwa ajali ya ndege katika Eneo la Ndola huko Zambia (Wakati huo Rhodesia)akiwa katika jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro wa DRC.

Mimi siyo mwandishi wa habari lakini bila shaka mmenipata ninachotaka kusema.
 
Katika makosa ambayo yatafanywa na Tanzania ni pamoja na kujaribu au kuondoa majeshi DRC. Hapa sisi watanzania tunaishi hapa GOMA imekuwa ni shangwe na ndelemo kutokana na mafanikio ya JWTZ. Sijui huko nyumbani mtachukuiaje lakini ukweli tupo juu. Hwa jamaa zetu wa Rwanda tupo nao wengi sana hapa nao hawaamini yanayoendelea chini ya JWTZ.
 

Tumesikia kutoka BBC, unasemaje kuhusika kwa majeshi ya Tanzania kwa vita ya sasa kati ya M23
 
tuambie kiini cha mgogoro ni nini, na kama unasema mgogoro unakaribia miaka 14 tuambie interest ni nini na kama hiyo interest inapersist kwa marais wote, na kama sio kwa nini vita isikome so long rais mwanzilishi au aliyehusika kwanza hayupo? na kama marais hawahusiki, basi wameshindwa mbinu ya kunyamazisha hiyo migogoro?
 
Hapana mpaka sasa habari tulizoambiwa hapa GOMA (hata na hao JWTZ) waliopo hapa ni kuwa amefariki afisa mmoja tu. Naambiwa yalikuwa ni mapiganio makali sana huko KIWANJA.

Unajua DRC haipigani kimsingi na RWANDA. Kilichopo ni kuwa Rwanda wana Interest hapa DRC na hivyo wanakisaidia kikundi cha M23. Wamekuwa wakikipa misaada ya vifaa, silaha, milipuko na hata kuwafundisha. DRC haiwezi kuishambulia RWANDA utakuwa ni uchokozi ambao kimataifa ni kosa.
Fursa za TZ hapa zipo nyingi sana. Hata sisi hapa GOMA tunanufaika na hilo. Tupo karibu waTZ 1500 tunaoishi hapa GOMA. Mpaka sasa kweli tnategemea kupitia hapa GISENYI kuingia DRC endapo jamaa watazuia au kupandisha ushuru hilo bila shaka litalamikiwa kimataifa kwani kuna Wanyarwanda wanafanya bisahsra ya kuleta bidhaa huku. Pia kuna maeneo ya KIVU YA KUSINI ambako bidha kutokea Kigoma huingia DRC kupitia Lake Tanganyika.
 
Umenena vyema kuwa wewe ni mtanzania ambaye umelowea Goma. Inaonekana huna habari na amri ya JWTZ kuwa sisi wananchi haturuhusiwi kuongelea masuala ya vita ya huko Congo mpaka kwa kibali chao. Angalia usije ukaingia matatizoni na jeshi letu kwa kuongelea vita ambayo tayari kuna katazo la chombo chetu cha ulinzi na usalama.
 
Hivyi ninvyoandika ninaangalia TV hapa, miji yote ambayo ilikuwa imekaliwa na M23 imekwishachukuliwa na FARDC. Kanzia Kiwanja, Rumangabo, Katale, Kibati (ulichukuliwa siku nyingi) yote ipo chini ya FARDC. Wamebakiza mji wa BUNAGANA ambapo ni mpakani kabisa na Uganda. Bila shaka kufikia Kesho mtasikia M23 imekwisha. Tuombe yasitokee tena mauaji kwa JWTZ maana naambiwa wanafanya kweli huko front.
 
Ndiyo maaana nasema kwa yale niyawezayo nitayajibu. RDC ni kubwa na mgogoro ni complex. Sikusudii kudanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…