Uliyonifanyia yalinifanya niwe mdogo kama piriton

Uliyonifanyia yalinifanya niwe mdogo kama piriton

Da kweli wako wapendao hata mlio tu. Kuna wakati nilikuwa sikosi yale majarida ya vikaragosi basi jamaa kapiga simu ofisi nyingine ile kusikia sauti tu akapagawa. Ikawa kila siku jamaa lazima aongee na mgeni ikawa mihadi wakakutana! Jamaa hakuamini aliyesimama mbele yake! King Kong mrembo! Njia alopita haijaota majani todate. Pole kaka ilikuwa unaonyesha urijali wako.

maisha ndivyo yalivyo dada. Mia
 
kaka mimi ilinikuta facebook. Nilifunga safari mpaka dar nikapangiwa na hoteli ya kufikia. Mpaka saa sita usiku mwenyeji haonekani bt akinipa moyo yuko harusini atakuja,hakuja mpaka kumekucha! Yani tunavyoongea sa ivi ufacebook nimeacha

dah! pole sana mkuu. Mia
 
kwa style hii wataingizwa mkenge wengi tu hapa JF na mitandao mingine ya jamii...; wapo wanaongia gia kwa porojo tu, wengine flirting, wengine majina, wengine avatar, wengine picha etc

sio wote. hata mimi watu ishirini nadanganywa na watu 3 tu. mia
 
tupo wengi kweli, wengine wanaona aibu kutoa ushuhuda. ama kuna mwengine mnapanga kuonana ukitarajia ndo alivyo kwenye picha., ila akija utaona ni king kong mrembo kama alivyosema mdau huko mwanzo.

wewe umeongea point sana. Mia
 
MIA unavyoonekana mjanja fulani kumbe na wewe umeingizwa kingi?? Mnajifanya mnajua kucheza na vichwa vya wanawake ila wanawake wanaoamua kuwakomeshea wanawakomeshea kweli kweli japo ni wachache wanaofanya hvo. Poyeeeee MIA

siku zote ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. sio siri alininyong'onyesha. asante kwa pole dada angu. mia
 
eeehh,hutaniwi?wake za watu hao!!!!hivi kumbe humu JF kuna watu wakware hivi?me najuaga humu ni kutaniana tu

kutania wakati watu humu wameoana? mwenyewe natafuta wa kuoa sasa hivi.
 
Hellow! jf
Huyu binti nilikuwa nawasiliana nae kwanza kwa pm. hadi tukapanga nae niende kumtembelea zanzibar. Jmos iloisha nikafunga safari hadi bandalini. Mpango ulikuwa ni kwenda nilale huko. Nikampigia simu ya kwamba napanda boti ya saa nane na akaahidi kuja kunipokea bandali ya zenj, Cha ajabu nilipofika zenji na kumpigia simu akanijibu "HIVI UMEENDA KWELI? MWENZIO NAKAA ARUSHA. YALE NI MAMBO YA JF BANA FIGGANIGGA, MI NKAJUA WANTANIA ATI!. POLE SANA".Akamalizia na kicheko!. Nimfanyeje huyu jaman?. Mia
hii ndio hasara ya kumpapatikia m2 kupitia mitandao ya kijamii.usirudie tena kosa hili.
 
pole sana ndugu yangu huo ndiyo uanaume,tunajifunza kutokana na makosa usikata tamaa wasiliana naye tena,huyo hakuwa Arusha shetani mkubwa huyo , huyu alikuwa hapohapo Zanzibar isipokuwa alikuwa na jemba mwingine,hawa wadudu ni waajabu sana.

siku zote nasema hawa wadudu waajabu sana. halafu ungekuwa mwanaume ndo umemfanyia hivyo msichana anaweza kukugeuza ndondocha kwa jinsi atakavyo fyumu. Mia
 
Uendelee kuniogopa hivyo hivyo, ukilogwa ukajifanya kichwa nazi ukipita anga hizi siku hyo utarudi kwenu bila nguo wala viatu.....,ukiona hii user name geuza macho yako au ufungue thread nyingine!!!

akuache kabisa sababu sasa hivi nmekuweka chini ya uangalizi wangu kabla sijakuface live. Mia
 
mie nlishawahi kudanganywa eti anakaa mabibo kumbe yuko hall 7, na wakati naenda panda gari pale bondeni toka hall 6, ye akawa anancheki kwenye madirisha ya hall 7. Ila mwishowe 'nilifanikiwa'. we usikate tamaa endelea kumfuatilia huyo utampata kwani kisha ona uko serious, atakuonea huruma, kazana mtoto wa kiume!

nmeshaa mwambia yeye ndo akazane. mimi sitaki tena hata kama kaomba msamaha. ili nmsamehe ajilete dar. mia
 
Umfanyeje? Mfate Arusha we vipi bana....usiwe mtu wa kukata tamaa kirahisi bana unakuwa ka sio Kinega bana!

hahahahaaaa....!!. sniper mambo vipi mkuu? ntakupa contact zake umcheki pande hizo kama yupo au laa. au sio? mia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom