Nilichambwa mbele ya rafiki zangu niliabika mimi,niliaibika sana!.
Sikia tu mtoto wakike amesimama mbele yako,mguu mmoja mbele, kiunoni kajivika kanga kana kwamba anataka kukata mauno! Halafu ananesanesa halooo!! Lile neno la "UNIKOME" nilikuwa nalisikia kuanzia kiambishi awali cha Kati na kiambishi tamati!,mzizi wa neno,na ndipo nilijua hilo neno ni sentensi ya kujitegemea na iliyijitosheleza!.
Nilikuwa mnyonge kama nimemwagiwa maji!.. kitoto cha watu kimefura,ule mtaa niliacha kwenda kwa wiki kadhaa.😂