Ulitumia mbinu zipi kufikisha million 10

Ulitumia mbinu zipi kufikisha million 10

Habari.

Jumapili inaendaje kwenu.

Vijana wengi tunajitafuta na hatujajipata ,tunatamani mafanikio tuwe na maisha mazuri ya kukidhi mahitaji.

Moja ya silaha kubwa katika mafanikio ni kushare na wenzio.

Karibu utuambia Ulifanyaje Hadi ukaweza kufikisha million 10 mbinu ulizopitia.

Je ilikupa utajiri ?

Au ilikufirisi?

Tuambie Tunaweza kujifunza.
Nili roll over odd 5 mara 3 kwa miezi miwili nilitumia 100k kama stake .


, kila ijumaa na jmosi ndio Nilikiwa nabeti
 
Duuuh nina laki 7 now ad nifke 10 milion sjui lin
komaa mkuu utafika mbali
IMG_20240910_101938_408.jpg
 
-Saving ni nzuri sana.

-Chochote unachokipata kumbuka kusave. Hata kama ni kidogo.

- huwa naSave pesa kwa mpango wa muda mrefu. Hapa namaanisha unaweza kufanya utafiti wa kufanya biashara fulani ukakuta inahitaji labda hyo mil.10. Kumbuka hapo hata hyo pesa huna lakini let say una kazi yoyote kwahyo kupitia hyo kazi unapata pesa lakini pia unakuwa na mpango wako wa muda mrefu,kama mimi nina mpango wa kuchana mbao aina ya pine nikipata mil.15.

-huwa situmii pesa kwa ushawishi wa macho. Macho huwa na kawaida ya kuwa na akili kuishinda akili ya mipango yako😀😀.

-usitamani mipango ya mtu mwingine. Kuna kawaida ya sisi vijana tukikaa pamoja huwa tunasimuliana mipango yetu na mwisho wa siku unakuta mipango ya mwenzako ni bora kuliko mipango yako. Kwa kukiuka mipango yako kunakufanya hata saving yako ibadilike kutokana na mahitaji ya mpango huyo rafiki yako labda unakuta anakwambia mtaji unaohitajika ni mdogo zaidi kumbe yeye ndyo hajafanya utafikti wa kutosha hatimae unapoteza mpango wako na wa huyo rafikiako.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom