Basi bana. Kama wiki kadhaa hivi iliingia meseji fupi lakini tamu ajabu. Ilikuwa imethibitishwa. Shilingi milioni sita (6,000,000) keshi zilikuwa zimeingia kwenye akaunti yangu ya benki. Nikasema labda ni matapeli wanataka kunizingua. Nikaenda kwenye akaunti. Nikakuta kweli mzigo upo umetulia. Sikuridhika. Nikaenda kuangalia kwenye ATM fizikale laivu kabisa. Nikakuta ni kweli.
Ajabu ni kwamba aliyetuma hizo pesa simfahamu na sikuwa na mchongo wo wote wa milioni sita niliokuwa nikiusikilizia. Nimeuliza kila mtu ninayemhisi mpaka watu wa diaspora huko lakini hakuna aliyenitumia hizo pesa. Kuna mahali nilipiga mchongo wa kuwa nalipwa kama milioni 4.5 hivi kwa mwezi kwa miaka 15-20 ijayo lakini mchongo huo hautakuwa active mpaka 2027. Niliwaandikia pia wakasema hawajatuma cho chote. Ni nani kakosea akatuma hizi pesa?
Mpaka ninapoandika hapa pesa hizo zipo zimetulia kwenye akaunti. Na mtumaji bado hajulikani.
Wengine wanasema eti jamaa wanaotakatisha fedha siku hizi wana mtindo huo. Wanaweka pesa kwenye akaunti yako hasa ambayo iko dormant kidogo halafu baadaye wanakuja wanazihamisha.
Lakini akaunti yangu haiko dormant kivile maana haiwezi kupita siku mbili au tatu sijaitumia.
Nikizitumia hizi pesa nitakuwa nimekosea maana mpaka sasa zipo tu naziangalia? Kuna dogo anahitaji kimtaji cha kama milioni tatu hivi nataka nimpe.
Ungekuwa wewe ungefanyeje kwenye situation hii?
View attachment 3525498