Ulishawahi kupekua au kuchunguza simu ya mpenzi wako au mkeo?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,132
32,835
Habari za jumamosi wapendwa.

Bila ya shaka sote tu wazima wa afya na walio na maradhi Mungu awaangazie warudi kwenye afya zao.

Sote tunajua kuwa ukuaji wa teknolojia umeleta manufaa kwenye jamii zetu hata imekuwa rahisi kupashana habari na kurahisisha shughuli mbalimbali za kijamii. Bila ya kusahau ukuaji wa teknolojia kwa kiasi kikubwa kumewafanya watu kuwa karibu na hivyo kuifanya dunia kuwa kama kijiji kimoja.

Lakini kwa upande wa pili ukuaji wa teknolojia umeleta changamoto kwenye suala zima la mahusiano kiasi kwamba kiwango cha uaminifu kwenye ndoa au kwenye mahusiano kimeporomoka tangu kukua kwa teknolojia. Kwa upande mwingine, umeongeza uaminifu ingawa ni kwa wachache.

Je wewe mdau wangu ungependa kushare nasi mara ya kwanza ulipopekua au kuchunguza simu ya mpenzi wako au mkeo uligundua nini na pengine ulichukua hatua gani baada ya tukio hilo?

Karibuni sana
 
Huwa natamani sana kupekua, ila nikishawaza kuwa ikitokea nikakutana na nisichokitarajia sitaweza kuhimili naacha.

Najua siwezi kuhimili maumivu endapo nitakumbana na kitu cha tofauti. Sitaki kujipa maradhi mie maisha yenyewe haya bwana mafupi
 
Nilipewa simu kuchaji hata sikuwa na mpango wa kupekua ndanindani sasa wakati nachomeka kuna sms ikawa inapita juu ya kioo yaani sikuichaji kabisa na kesho yake nilimrudishia simu yake na nilimpa warning sign kuwa asije kurudia tena kunipa simu yake ntaivunja.
 
Jaman mm kidogo nipo tofaut, kama tukiwa na taratibu za kupekuana kweny cm czani kama mahusiano yatadumu, ila cha msingi kinacho takiwa heshima ndan ya nyumba idumu
 
Binafsi maishani mwangu sijawahi kuwaza kupekua simu ya mwanamke yeyote niliewahi kua nae kimahusiano lakini ilifika kipindi visa vilizidi kiasi kwamba ilinibidi tu nipekue. Ilikua ni usiku wa manane nilijitahidi kumuamsha kwa upole ili nimuulize lakini aliangalia zile msg na kunibinulia mdomo, hahahaaaa kilichofata Mungu pekee ndie anaejua, hua sipendi dharau hasa kwa mwanamke. Sidhani kama nilichukua uamuzi sahihi japo zilikua ni hasira nilimpiga sana na nikaondoka usiku ule ule na mpaka sasa sina mawasiliano yoyote nae
 
Simu yangu ni yangu na yke ni yake sitaki stress z kijinga ukimchunguza sana bata humli
Exactly!!!
Kuwa na mke/mme hakumuondolei kuwa na uhuru wake binafsi. Mi sihangaiki na kuchunguza simu ya wife... Yeye hata kama angekuwa na kimuhemuhe cha kuipekua hayo mapasswork nayobadili kila siku mwenyewe atakoma kujaribu.

Mi sipendagi ujinga kwenye maswala ya matumizi ya kilongalonga.
 
Back
Top Bottom