LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 457
- 1,725
Kuna wakati huwa inauma sana, baada ya kununua kitu halafu ukirudi mtaani mtu akikuuliza bei uliyonunulia ukamtajia halafu akakwambia mbona umeuziwa bei kubwa hivo na wakati zinauzwa tu bei rahisi.
Nimewahi kutana na mambo Kama haya kwa nyakati tofauti.
Nimewahi uziwa begi Kariakoo 40 baada ya kufika nyumbani kuna jirani akaniambia kuwa huwa zinauzwa 25 tu
Pia nimewahi katiwa tiketi na madalali kwa 25 baadae nikaona abiria wengine wakikatiwa kwenye basi kwa 15 kutoka itula to tabora mjini.
Funzo:
Hii ipo hasa kwenye biashara mfano. Mwaka jana nilitoka kijijini kwenda mjini kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vifaa vya umeme vya mteja wangu, nikiwa ndo kazi yangu ya Kwanza ya wring ya umeme.
Basi nikaenda duka la Kwanza kuulizia menu switch jamaa akaniambia 80 mwisho 70.
Nikashtuka baada ya kuona mbona hela haitatosha kabisa kununua vitu vingine, maana niliulizia kwa mtu mmoja jumla ya pesa aliyotoa kusukiwa umeme, akaniambia alitoa 180 wring ya taa 3 na soketi 1 basi bhana nikaenda duka la pili.
Jamaa akaniambia ni 25 dah! Nikawaza sana ni watu wangapi hufanyiwa hivo, nikagundua ni wengi ila pia mfanyabiashara wa aina hiyo ni ngumu kufanikiwa zaidi kibiashara.
Fikiria angeweza kunifanya mm kuwa mteja wake wa kudumu ila yeye akanifukuza mazima.
Tusiwe na tamaa kwani waweza muona mtu hajui kitu ila siku akijua hutamuona tena, na sio kila mteja huwa ni mpita njia was siku moja tu. Hapana tujitahidi kutoa huduma nzuri.
Mimi ni fundi electronics najitahidi kutoa huduma isiyokandamizi, ndo maana nimeweza kutengeneza wateja wa kudumu.