Ulishawahi kukutana na mtu aliyevaa nguo zinazofanana na zako? How did you react to it?

Duh uliulamba sana miaka ya 90 savco ndo ilikuwa baba lao, enzi hizo ukipiga hizo pambana unaonekana bonge la mwanaume
 
Leo msikitini kanzu zetu karibia msikiti wote zilikuwa zinafanana, nika hisi walinunua kariakoo duka nililonunua mimi.
 
Ahahahaaaaa nilishawahi kwenda bar moja,sasa shati nililovaa linafanana na la meneja wa bar,sasa wahudumu wapya wakawa wananifata na kunielezea shida zao wakidhani ni meneja, mpaka baadhi ya wateja pia,aaaah ilibidi nisepetuke fasta
 
Shati langu la sherehe za uhuru liko kila pahala nikienda lazima nikutane na mtu kalikung'uta
 
Miaka ile ya 1990s kuna wakati nilikwenda Arusha, nikiwa ndani ya "SAVCO jeans, white T-shirt & white rubber shoes".
Mkuu, bila shaka hii ni old school moja matata sana. Ninatamani sana ningekuona face to face siku hiyo
 
Sina hili wa lile nikapita pale hoteli ya Golden Rose, na ile nafika karibu na uwanja wa Sheikh Amri Abeid, nikakutana na kundi la vijana wa "promotion" wa BONITE BOTTLERS waume na wakike wote tumeulamba sawa sawa na mimi.
Bila shaka hii ni Arusha mzee baba
 
wakati unainunua huko au unaishona ulidhani ndio ilikuwa ya mwisho ?
 
I never paid attention
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦