Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,814
- 40,420
Mkiambiwa tumerudi enzi za Sultani Mangungo wa Msovero muwe mnakubali, msibishe maana mnayoyafanya hayana tofauti na enzi hizo. Tumesoma kwenye vitabu vya historia kwamba Waafrika wenzetu waliokuwa na nafasi enzi hizo za utumwa waliwapigia Debe matajiri wanunuzi wa Watumwa na kuwapa sifa za uzuri wa America kusini na maeneo mengine walikokuwa wanapelekwa. Kwa namna hiyo Watumwa wengine walijipeleka wenyewe na kuuzwa Kwa Hiari ili wakafaidi maisha Ulaya.
Sisi Wenye Mali ndo tumeuza au basi tukubali tumewakodisha DPW bandari zetu. Iweje Sisi ndo tunazunguka duniani kueleza uzuri wa DP-World badala ya wao au nchi nyingine ambayo iliwahi kuingia nao mkataba ijitokeze kutueleza uzuri wao?
Hebu wafungaji nisaidieni, unakwenda mnadani kuuza Ng'ombe wa familia, anatokea mnunuzi lakini Hana fedha taslimu anaomba umkopeshe na wewe unakubali unamwachia Ng'ombe. Unaporudi nyumbani unaanza kulaumiwa na ndugu zako unaanza kumsifia mnunuzi ambaye umeonana naye mnadani Kwa mara ya Kwanza?
Bora basi wauzaji waliowahi kufanya naye Biashara wangejitokeza kumsifu lakini eti wewe kuwathibitishia ndugu zako unakwenda nyumbani Kwa mkopaji unawapigia simu ndugu zako unaweka simu loud speaker halafu mkopaji anaanza kujisifu jinsi alivyo mwaminifu na mlipaji mzuri wa madeni? Hao ndugu zako wakikubaliana na huo usanii basi haziwatoshi.