Mungu ni muandaaji na muongozaji bora wa filamu za maisha yetu

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Leo 12:15hrs 19/06/2022

Maisha ya mwanadamu ni filamu "movie" ambayo Mungu ameiandaa na anaiongoza mpaka mwisho wake,binafsi naifurahia na naendelea kuifurahia filamu ya maisha yangu hadi hapo mwisho, naamini mmewahi kuangalia filamu "movie" fulani mkavutiwa nayo na mkapenda kujua muongozaji wake wa filamu, wapo waongozaji wengi kama Peter wengi mnamjua, Spike Lee, Terence, Steven Spielberg, Quentin Tarantino, Kunle Afolayan, Zina Saro Wiwa, Desmond Elliot, Tunde Kelan,Yi Mou Zhang, Lee Moon Ji, zaidi ya hao wote muongozaji bora wa muda wote ni Mungu Mwenyezi aliyetuandaa, aliyetuumba na kuyaongoza maisha yetu hadi mwisho na kurudi tena kwake yeye Mwenyezi Mungu.

Duniani ni kama sokoni,tunakuja kununua bidhaa halafu jioni tunarudi nyumbani na bidhaa tuliyonunua,nyumbani ni kwake yeye Mwenyezi Mungu aliyetuumba,rejea kwenye biblia, Yeremia 1:4-19 neno la Bwana lilinijia,kusema,kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua,na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa, ndipo niliposema, Aa, Bwana Mungu! Tazama,siwezi kusema,maana mimi ni mtoto,lakini Bwana akaniambia, usiseme, mimi ni mtoto, maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru, usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.

Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu, Bwana akaniambia, tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako, angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme,ili kung’oa na kubomoa na kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda, tena neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia,waona nini?

Nikasema, naona ufito wa mlozi, ndipo Bwana akaniambia, umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize, neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema, waona nini? Nikasema, naona sufuria lenye maji yatokotayo,na mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini, ndipo Bwana akaniambia, toka kaskazini mabaya yatatokea na kuwapata watu wote wakaao katika nchi hii.

Tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema Bwana, nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu na kuzielekea kuta zake pande zote na kuielekea miji yote ya Yuda, nami nitatamka hukumu zangu juu yao kwa habari ya uovu wao wote, kwa kuwa wameniacha mimi, wakaifukizia uvumba miungu mingine,wakaziabudu kazi za mikono yao wenyewe, haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru,usifadhaike kwa ajili yao,nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao,maana,tazama,nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote,juu ya wafalme wa Yuda,na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake,na juu ya watu wa nchi hii,nao watapigana nawe,lakini hawatakushinda,maana mimi nipo pamoja nawe,asema Bwana,ili nikuokoe.

-Mungu anaiandaa filamu ya Yusuph "Joseph".

Yusuph anatoka katika uzao wa Ibrahim,anayemzaa Isaka,anayemzaa Jacob,Jacob aliyeiba uzao wa kwanza wa kaka yake Esau,anakimbilia Padan Aramu kwa mjomba ake Laban,anafanya kazi kwa miaka Saba ili amuoe Rachel,baada ya miaka saba anapewa Leah,anaambiwa hauwezi kuoa mdogo kabla ya mkubwa kuolewa,hivyo fanya kazi tena miaka saba ili umuoe Rachel,anafanya kazi miaka saba,anapewa Rachela,Mjomba ake Laban anamwambia fanya kazi tena miaka saba kila mnyama atakae zaliwa mwenye mistari au madoa doa atakuwa wako,utawachukua na kuondoka nao pamoja na wake zako,Jacob anafanya tena kazi miaka saba kila mnyama mwenye mimba,wakati wa kujifungua aliweka juu fimbo na kivuli cha fimbo kilichora mistari kwa kila mnyama aliyezaliwa,Mungu anamsimamia kwa hili baada ya kutapeliwa kwa Rachel lakini kumbuka nae alitapeli haki ya mtoto wa kwanza kwa Esau.

-Filamu ya maisha ya Yusuph ilihitaji watoto kumi na mbili,Yusuph akiwa wa kumi na moja.

Leah anamzalia Jacob mtoto wa kwanza,Racheli anashindwa kumzalia Jacob,Leah anamzalia tena Jacob mtoto wa pili Rachel anashindwa kumzalia Jacob,Leah anamzalia tena Jacob watoto wawili,Rachel anashindwa kumzalia Jacob,Rachel anamtoa kijakazi wake "house girl" anamzalia Jacob watoto watatu,Leah nae anamtoa house girl wake anamzalia Jacob watoto watatu,Leah aliwazaa Reuben,Simeoni,Lawi,Judah,Isakari na Zabuloni na mwishoni Mungu anafungua tumbo la Rachel,anapata ujauzito anamzaa Yusuph,Jacob na Rachel wote wanamtukuza Mungu,wakiwa njiani kutoka kwa mjomba ake Laban Rachel anajifungua tena mtoto wa pili, Benjamin lakini kwa bahati mbaya Rachel anafariki wakati wa kujifungua,hadi Leo mahali hapo pembeni ya barabara nje kidogo ya mji wa Bethlehem panaitwa "The tomb of Rachel".

-Yusuph anaota ndoto,Mungu anamuonesha Yusuph vipande vya mbele vya filamu yake.

Nakuombea katika jina la Yesu Kristo nawe uote ndoto,uone vipande vya mbele vya filamu ya maisha yako, Yusuph aliota ndoto akayaona maisha yake ya mbeleni akawasimulia kaka zake kumi na moja akawaambia nimeota nyota kumi na moja zikiniinamia na Jua na Mwezi,kaka zake wakakasirika sana,Baba yake nae akasema yaani hata Mimi Baba yako nikusujudie wewe,lakini ndivyo filamu ilivyo licha ya wao kukataa,siku moja kaka zake wakiwa malishoni wakichunga kondoo,Baba yake akamtuma Yusuph kuwapelekea kaka zake chakula,kaka zake walipomuona mdogo wao wakasemezana wao kwa wao wakisema "Bwana ndoto huyo anakuja" tumuue halafu tumwambie Baba wanyama wakali wamemla Yusuph,Simeone akapingana nao akawaambia tusimuue tumtupe kwenye kisima kilichokauja maji,wakakubaliana hivyo Simeone akajitoa akaenda upande mwingine wa malisho,Yusuph alivyofika wakamkamata wakamtumbukiza kwenye kisima kilichokauka maji,baadae wakauona msafara wa Wamidian na Waishmael,

Judah akawaambia ndugu zake,tumuuze kwa Wamidian na Waishmael tupate pesa,wakakubaliana wakamtoa kwenye shimo wakamuuza kwenye msafara huo wa watumwa wa Midian na Ishmaelites,na baadae Yusuph akauzwa Misri kwenye nyumba ya Potipher ambae alikuwa ni Afisa katika nyumba ya Pharaoh,Mungu alimbariki Yusuph,kila alichogusa kilibarikiwa,Potifa akampa Yusuph mamlaka katika nyumba yake,Mke wa Potipha akavutiwa kimapenzi na Yusuph,akamlazimisha Yusuph wafanye mapenzi,Kwa kuwa Mungu alimuonesha Yusuph vipande vya filamu yake vya mbeleni,Yusuph alikataa kulala na Mke wa Potipha kwa kuwa hiyo sehemu haipo kwenye ndoto aliyoota,ambayo Mungu alimuonesha Yusuph maisha yake ya mbeleni,Yusuph aliona maisha yake ya mbeleni kuwa atakuja kuwa Mkuu,nyota,Jua na mwezi zitamuinamia,lakini hakuna sehemu aliyoota kulala na mke wa Potipha.

-Yusuph anaota ndoto Gerezani na anatoa tafsiri itakayokuja kumtoa Gerezani.

Mke wa Potipha anaendelea kumlazimisha Yusuph afanye nae mapenzi,Yusuph anakataa,Mke wa Potipha anapiga kelele za kubaka,anavua nguo zake zote na kusema Yusuph anataka kumbaka,Potipha aliposikia habari hiyo akamtia Gerezani,Yusuph akafungwa katika gereza la wafungwa wa maofisa wa Misri,kumbuka hii ndiyo njia ya kumfikisha Yusuph kuwa Mkuu hata nyota,Jua na mwezi kumuinamia,bila hatia kaka zake walimchukia Yusuph na kutaka kumuua,amshukuru Simeone aliyesema tumtupe kwenye kisima,na Judah aliyesema tumuuze,bila hatia Potifa anamuweka Yusuph gerezani,hii ndio njia itakayomfikisha Yusuph kwa Pharaoh na kuwa Mkuu hata nyota,Jua na mwezi kumuinamia,zikapita siku gerezani,watumishi wawili wa Pharaoh,muoka mikate na mtengeneza Wine wakamkosea Pharaoh na kuletwa gereza moja alipofungwa Yusuph,siku moja watumishi hao wakaota ndoto, mtengeneza wine aliota matawi matatu,yakachanua na kutoa dhabibu,akazikamua na kumpa Pharaoh,asubuhi Yusuph akamuuliza Yusuph maana ya ndoto yake,

Yusuph akamwambia matawi matatu ni siku tatu na baada ya siku tatu Pharaoh atakutoa gerezani na utarudi kwenye kazi yako ya kumtengenezea Wine Pharaoh,na ikawa hivyo baada ya siku tatu yule mtengeneza wine akatoka na kurudi kwenye kazi yake ya kutengeneza wine,siku moja Pharaoh akaota ndoto ng'ombe saba wanene halafu baadae wakaja ng'ombe saba wembamba wakawala wale ng'ombe saba wanene na bado wale ng'ombe saba wembamba wakabaki vile vile wembamba licha ya kuwala wale ng'ombe saba wanene,alipolala aliota tena masuke manene mara yakaota masuke membamba yakaja yakayala yale masuke manene,ndoto hizi mbiki zikamsumbua sana Pharaoh hata akaita wachawi,na waonaji kutafsiri ndoto lakini tafsiri zao hazikuleta maana katika ndoto hiyo,ndipo mtengeneza wine akamkumbuka Yusuph aliyetafsiri ndoto yake gerezani na ikawa vile vile alivyotafsiri, akamwambia Pharaoh yupo mtu mmoja gerezani anaitwa Yusuph alitafsiri ndoto yangu na ikawa, Pharaoh akaamuru Yusuph aitwe kutafsiri ndoto hiyo,

25Ndipo Yusuph akamwambia Farao, “Ndoto zako zote mbili tafsiri yake ni moja. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni. 26Ngombe wale saba wazuri ni miaka saba, na yale masuke saba mazuri pia ni miaka saba; ndoto hiyo tafsiri yake ni moja. 27Wale ng'ombe saba waliokonda sana, ambao waliwafuata wale wanono, na yale masuke matupu saba, yaliyokaushwa na upepo mkavu wa jangwani, maana yake ni miaka saba ya njaa. 28Kama nilivyokueleza, ee Farao, Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni. 29Kutakuwa na miaka saba ya shibe katika nchi nzima ya Misri. 30Lakini baadaye itafuata miaka saba ya njaa, hata hiyo shibe isahaulike kabisa. Njaa hiyo itaiangamiza nchi hii. 31Shibe hiyo itasahaulika kabisa kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno. 32Ndoto yako ilirudiwa mara mbili kwa mifano inayofanana kukuonesha kwamba Mungu ameamua, naye atatekeleza jambo hilo karibuni.

37Shauri alilotoa Yusuph lilionekana kuwa jema mbele ya Farao na watumishi wake wote. 38Kwa hiyo Farao akawauliza watumishi wake, “Huyu mtu ana roho ya Mungu! Je, tunaweza kumpata mtu mwingine kama huyu?” 39Kisha akamwambia Yusuph, “Kwa kuwa Mungu amekufunulia haya yote, hakuna mtu mwingine mwenye busara na hekima kama wewe. 40Wewe ndiwe utakayeisimamia nchi yangu, na watu wangu wote watakuwa chini ya amri yako. Mimi tu ndiye mkuu kuliko wewe kwa kuwa nakalia kiti cha kifalme. 41Basi, sasa nakuteua rasmi kuwa mkuu wa nchi yote ya Misri!” 42Ndipo, Farao akaivua pete yake ya mhuri kidoleni mwake na kumvisha Yusuph, akamvalisha na mavazi ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni. 43Farao akampandisha katika gari lake la pili la farasi na walinzi wakatangulia mbele ya Yusuph wakipaza sauti na kusema, “Pigeni magoti!” Ndivyo Farao alivyompa Yusuph madaraka makubwa juu ya nchi yote ya Misri. 44Zaidi ya hayo, Farao akamwambia Yusuph, “Mimi ndimi Farao! Nasema: Mtu yeyote katika nchi nzima ya Misri asiinue mkono wala mguu wake bila kibali chako.” 45Farao akampa Yusuph jina la Kimisri: Safenath-panea. Akamwoza Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni. Basi, Yusuph akaanza kuitembelea nchi nzima ya Misri.

-Njaa ikaingia duniani.

Yusuph,Waziri Mkuu wa Misri akaamuru watu walime na kujenga maghala kuhifadhi mazao kwa ajili ya miaka saba ya njaa inayokuja baada ya miaka saba ya neema,Mazao yakahifadhia na ilivyofika wakati wa njaa,dunia nzima ilifunga Safari kwenda Misri kununua chakula,ndani ya dunia wapo Kaka zake Yusuph,nao wakafunga Safari kwenda Misri kununua chakula,walivyofika Misri wakaripoti kwa Waziri Mkuu, Yusuph ili kupata kibali,nae Yusuph akawatambua kuwa awa ni kaka zangu,akawauliza maswali akianza kwa kuwatisha kuwa ninyi ni wapelelezi,nao wakajibu hapana Mheshimiwa,sisi tumetoka kanaani,tumetumwa na Baba yetu Jacob kuja kununua chakula,Yusuph akapata uhakika,akawauliza mko wangapi,wakajibu kumi na mbili lakini tumebaki kumi na moja maana mdogo wetu mmoja alikufa, akawauliza mbona mpo kumi wakajibu mmoja wa mwisho amebaki na Baba maana ndiye mtoto mpendwa wa Baba baada ya kaka yake Yusuph kufariki.

Basi Yusuph akawapa chakula akawafungia na hela zao akawaruhusu waende,nyuma yao akawatuma askari wakawakamate kwa kuwa waliiba hela,Askari wakawaleta tena kwa Yusuph,nae akamfunga jela Simeone na kuwaachia wengine waende,akawapa na sharti la kurudi na mdogo wao wa mwisho Benjamin kama watarudi tena kununua chakula nchini Misri,na baada ya miaka miwili Jacob akawatuma tena watoto wake kwenda Misri kununua chakula, Wakamwambia tuliambiwa tukienda tena twende na Benjamin,Jacob akasononeka sana,lakini Judah akamwambia Baba yake,tupe Benjamin twende nae kuchukua chakula,tusiporudi na Benjamini basi uniue mimi,Jacob akawaruhusu waende na Benjamin,na baada ya kufika Misri,

Yusuph akafurahi kumuona Benjamini,akawapa chakula na kuwaruhusu waende,lakini aliweka kikombe cha dhahabu kwenye begi la Benjamin,akatuma askari akawakamate,walibisha wakasema ukikuta kikombe basi umchukue mtu huyo,na mara kikombe kikakutwa kwa Benjamin,kila mtu alilia maana Yusuph akataka kumchukua Benjamin lakini ahadi ya Judah kwa Baba yake ilikuwa tusiporudi na Benjamin basi niue mimi,Judah akamwambia Yusuph badala ya kumchukua Benjamin basi nichukue mimi,maana tulimuahidi Baba yetu kurudi na Benjamin,neno lile na kujitoa kwa Judah kwa ajili ya Benjamin kukamchoma Yusuph,akageuka akalia kwa sauti na kuwageukia tena akawaambia Mimi ni Yusuph mliyetaka kuniua,lakini mkaniuza kwa Wamidian na Waishmaeli na kuniuza kwenu ilikuwa ni mpango wa Mungu kutimia kwa ile ndoto niliyoota na kuwasimulia,nanyi mkachukia na kutaka kuniua,wote wakatazama na kuangua kilio kikuu cha majuto na kuomba msamaha.

Nimalizie kwa kusema,ndoto ya Yusuph,nyota kumi na moja,Jua na mwezi zikimuinamia ilitimia baada ya miaka 22 ,kwa miaka yote ishirini na mbili watoto wa Jacob walimdanganya Jacob kuwa Yusuph amekufa,kwa miaka yote ishirini na mbili kulionekana kuna msiba kwenye nyumba ya Jacob,kwamba Yusuph amekufa na maiti yake haijawahi kupatikana,niwakumbushe pia wakati Yusuph anakuwa Waziri Mkuu,Pharaoh akampa Yusuph, Asenath kama Mke wa Yusuph,Yusuph akawa Mkuu sawa sawa na ndoto yake ilivyokuwa,na hivi ndivyo vipande vya filamu aliyoonyweshwa Yusuph kuwa vitatokea katika maisha yake baada ya miaka ishirini na mbili.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Sawa Mungu alimjua tangu tumboni, Vipi Samsoni ambaye mimba yake iliandaliwa kuwa mnadhiri wa Mungu na hata vyakula vya mjamzito vilipangwa na alipoishia, nakupa changamoto tu😁
Waamuzi 13:7
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
 
Sawa Mungu alimjua tangu tumboni, Vipi Samsoni ambaye mimba yake iliandaliwa kuwa mnadhiri wa Mungu na hata vyakula vya mjamzito vilipangwa na alipoishia, nakupa changamoto tu
Waamuzi 13:7
lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hata siku ya kufa kwake.
Tatizo Samson alikuwa anapenda Pisi sana..

Na kawaida kile ukipendacho ndio kitakacho kuondoa... Mashtaka na Sera zinatungiwa hapo hapo.
 
Of course kama alivyo wa set akina Yuda na Farao ndio hivyo hivyo anawaset na wengine..

Bila yeye leo hii Jiwe angekuwepo anatuvimbia na kutukoromea kwa pesa zetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom