Elections 2010 Ulinzi wa wagombea uraisi wa kambi ya Upinzani

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,241
113,615
Kwa nchi kama Marekani, wagombea uraisi wote wa vyama vikubwa (Republicans na Democrats) hupewa ulinzi Secret Service wakati wa kampeni hadi uchaguzi unapoisha.

Je kwa Tanzania, wagombea kama Dkt. Slaa na Ibrahim Lipumba wana ulinzi gani? Najua Kikwete kwa vile ni incumbent anapata ulinzi wake wa kila siku kama raisi. Hawa wengine inakuwaje....au vyama vyao ndio vina jukumu la kuwapa ulinzi?
 
=====
Baada tu ya kurudisha fomu tume ya uchaguzi na kuclear mapingamizi yote, watapewa ulinzi kwa mujibu wa sheria uchaguzi. Wakati huu wa kutangaza nia ni jukumu la vyama kuwalinda wagombea wao. Natamani wangepata hata baada ya kutangaza nia, maana you never know. Sheria iliogopa kufikia huko kwa sababu si wote watangazao nia, wanaweza kuwa wagombea. Kuna watu wanaweza kutangaza, wakajipatia ulinzi wa mwezi mzima nyumbani kwao. Unajua Dar siku hizi na vibaka::)
 
Sadly,chombo chetu cha usalama kimekuwa too politicised na CCM kiasi kwamba security detail inayotolewa kwa wagombea wa upinzani inakuwa kama field officers wanaochimba taarifa kuhusu mgombea husika.Isingekuwa tatizo kama taarifa hizo ni za kiusalama au za manufaa kwa taifa,lakini wao wanahangaika kunyonya data za kuinufaisha CCM.
 
Je inaruhusiwa kuomba ulinzi toka nje kama FBI na CIA?? labda wapinzani wanaweza kuomba msaada wa ulinzi kama hawana imani na ulinzi uliopo chini ya chama pinzani, inakubalika hiyo????
 
Je inaruhusiwa kuomba ulinzi toka nje kama FBI na CIA?? labda wapinzani wanaweza kuomba msaada wa ulinzi kama hawana imani na ulinzi uliopo chini ya chama pinzani, inakubalika hiyo????

WatakuBASHE wewe, endelea kusema huna imani na ulinzi wa CCM
 
Back
Top Bottom