Ulinitesa sana, sababu nilikupenda

Ulinitesa sana, sababu nilikupenda

Kutulia haimainiishi alishindwa kumpa vitasa. Nampongeza sana mtoa uzi sbb unaweza ukampiga ukamvunja hata mbavu ambapo baadae ingemgharimu hata kufungwa jela na faini pia. Baada ya kumpiga akaenda huyo mwanamke alipata nini? Malipo ni hapa hapa duniani. Ktk maisha yako yote epuka ugomvi sbb unaweza kupiga ukaua ukafungwa jela maisha au kunyongwa sasa hapo utakuwa umepata faida gani?
No halaf akasamehe sjui warudiane huko ndio namaanisha
 
Nafikiri wewe ni mzoefu sana hapa JF na ni moja ya watu walioona thread nyingi sana na mabadiliko ya aina mbalimbali kwa miaka yote uliyokuwepo kama ya kiuandishi,misemo,matusi na changamoto nyingine

Kwa uzoefu wako tayari najua unafahamu kuna watu wengine wanaleta mada ambazo either zimewakuta au wamezisikia hii yote ni kwa sababu tunatumia id fake

Kikubwa ni kuleta kisa ambacho watu wanaweza kuchangia full stop.
swadaktaaa, wengi hawaamini wanapo ambiwa ukweli. ukiwadanganya ndio wanaamini
Naona mtu na msemaji wake mmeanza kutofautiana ....

Haya endeleeni kudanganyana...
 
mhusika nikajua ni Ke....mpaka paragraph ya mwisho ndiyo nimeona kumbe ni Me.......usimrudie atakuchapa tena vibao
 
Mkuu katest uone kama kiporo kimechacha ama laa, kama hakijachacha pasha kula na chai ya tangawizi
 
Mwanaume ukapigwa kibao, ukakaa chini ukaendelea kulia.

Kuna shida juu ya uumbaji wako
 
Mwanaume ukapigwa kibao, ukakaa chini ukaendelea kulia.

Kuna shida juu ya uumbaji wako
nililia baada ya yeye kuondoka sio kama nililia kwa sababu kibao kiliuma. nililia usaliti
 
Habari wadau,

Leo jioni nimepokea simu kutoka kwa aliekua mpenzi wangu wa zamani, amenipigia simu na kuniomba msamaha kwa alionifanyia miaka 5 ilopita.

nilimpenda sana kuliko hata nilivyojipenda mwenyewe ila alinitesa sana,, nilivumilia mateso yake kwa sababu penzi langu kwake lilikua kubwa kuliko maumivu aliyokua ananipa.

kuna siku moja alihamaki kisa sikuwa na pesa ya kumnunulia viatu alivyokua anataka, tulivyorudi nyumbani nikamwambia anipe muda nipambane ili siku moja nkipata pesa nkamnunulie hivyo viatu.

Ila hakutaka kusikia chochote, akaanza kunitukana na kuniambia mimi ni boya na mzigo kwake, sina mchango wowote katika maisha yake zaidi ya kumpotezea muda tu. akaniambia rafiki zake wote wapenzi wao wanawanunulia vitu vizuri.

Aliponiambia hivyo niliumia sana moyoni, nikajikuta nimemwambia "basi na wewe nenda kwa hao rafiki zako wakutafutie mwanamme tajiri" .. baada ya kumwambia hivyo akanizaba kibao. akaniambia "usnitafute tena".

nililia sana siku hiyo hadi nikaishiwa na machozi, nikawa sina furaha tena, nilikua naona bora nife tu ili nipate kujipumzikia.

baada ya miezi 3, kidogo kidogo nikaanza kumsahau, nikaanza kutabasamu na kucheka tena. ilikua hadi nisha sahau namna ya kucheka, siku nacheka nilijihisi kama nipo ndotoni.

miaka 5 imepita, na leo ndio ameamua kunipigia simu na kuniomba msamaha na kuniambia anataka turejeane. nikamwambia nimekusamhe ila sitaweza kuwa nawe maana ninae mke ambae nampenda nae ananipenda, ameniambia hakutegemea kama nitamsamehe ila nimemwambia kuwa nilikuwa nimekusamehe tangia siku ulipo ondoka, akaanza kulia,,, akniambia hata pata mwanamme mwingine ataempenda sana kama mimi.
Naona mnatengenezeana mazngra ya kukumbushiana enz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom