Mr Bean
JF-Expert Member
- Mar 17, 2018
- 206
- 178
Habari wadau,
Leo jioni nimepokea simu kutoka kwa aliekua mpenzi wangu wa zamani, amenipigia simu na kuniomba msamaha kwa alionifanyia miaka 5 ilopita.
nilimpenda sana kuliko hata nilivyojipenda mwenyewe ila alinitesa sana,, nilivumilia mateso yake kwa sababu penzi langu kwake lilikua kubwa kuliko maumivu aliyokua ananipa.
kuna siku moja alihamaki kisa sikuwa na pesa ya kumnunulia viatu alivyokua anataka, tulivyorudi nyumbani nikamwambia anipe muda nipambane ili siku moja nkipata pesa nkamnunulie hivyo viatu.
Ila hakutaka kusikia chochote, akaanza kunitukana na kuniambia mimi ni boya na mzigo kwake, sina mchango wowote katika maisha yake zaidi ya kumpotezea muda tu. akaniambia rafiki zake wote wapenzi wao wanawanunulia vitu vizuri.
Aliponiambia hivyo niliumia sana moyoni, nikajikuta nimemwambia "basi na wewe nenda kwa hao rafiki zako wakutafutie mwanamme tajiri" .. baada ya kumwambia hivyo akanizaba kibao. akaniambia "usnitafute tena".
nililia sana siku hiyo hadi nikaishiwa na machozi, nikawa sina furaha tena, nilikua naona bora nife tu ili nipate kujipumzikia.
baada ya miezi 3, kidogo kidogo nikaanza kumsahau, nikaanza kutabasamu na kucheka tena. ilikua hadi nisha sahau namna ya kucheka, siku nacheka nilijihisi kama nipo ndotoni.
miaka 5 imepita, na leo ndio ameamua kunipigia simu na kuniomba msamaha na kuniambia anataka turejeane. nikamwambia nimekusamhe ila sitaweza kuwa nawe maana ninae mke ambae nampenda nae ananipenda, ameniambia hakutegemea kama nitamsamehe ila nimemwambia kuwa nilikuwa nimekusamehe tangia siku ulipo ondoka, akaanza kulia,,, akniambia hata pata mwanamme mwingine ataempenda sana kama mimi.