William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Mauza uza said:kunakosa gani watu kusoma UDSM na kurudi kwao????Mbona wapo watu kibao wanachukua uraia wa Marekani au UK wanasomeshwa bure au kwa mkopo na wakimaliza wanarudi makwao(original) India,Pakistan,China na hata TZ na Kenya???mbona wamarekani au waingereza hawapigi kelele???Kusoma sehemu ingine na kurudi kwenu kuwa Waziri ni Kosa?????tuache ubaguzi usio na msingi???Acheni Warwandese waendeleze nchi yao,kama nchi yenu imewashinda msitafute sababu.....
Habari ndo hio....
hii scandal ya Col rusimbi ipi? tunaomba darasa pleaseMbona wako wengu tu mkuu.City Engineer wa Kigali aliyekuwa Engineer wa Manispaa hapa Dar es salaam amesoma UDSM,kuna Mawaziri si chini ya wawili waliokuwa wanafanya kazi baada ya kusoma hapa UDSM wako kwao.
Nadhani mtakumbuka na scandal ya Col Rusimbi jeshini.
Lakini pamoja na yote haya yaliompata Ulimwengu mbona yeye hajataka kurudi Rwanda ili akapate post nzuri n kubwa toka kwa Kagame???Lazima tukubali Ulimwengu ni mzalendo kuliko hata wazawa wengine.
Sisi TZ nani anatuandalia viongozi? Mafisadi? I think you need to aim above the mark in order to hit the mark. Kama hatutaki kujiorganioze, ili kushika hatamu za uongozi leo na baadae, mi naona dawa si kuwarudi watu wenye asili ya Rwanda. Tutachemsha bwana mana hiyo kazi tutakayojipa itakuwa yenye lawama kubwa kuliko kuwa ma mikakati ya kutayarisha viongozi sisi kama sisi.Ilivyo sasa where is the training ground for future leaders? UVCCM? Mi sioni!Au kule PCCB ambako walichukua young blood nyingi wakati wanaanza. Lakini wanaandaliwaje? Wawe waongo kuiita rushwa si rushwa mpaka bunge liamke kama Richmond?Mkuu, hayo unayo yasema ni kweli kabisaaaa.. nikushuhudie tu kwa macho yangu kwenye myaka ya 1987-90 kule mjini Bukoba, kulikuwa na vijana wengi wahima wakisoma katika shule za secondary nyingi zikiwemo Ihungo, Kahororo, Bukoba sec, Rugambwa, Nyakato, na Ntungamo major seminary na nyinginezo around hapo, waliweza kujiorganise wakasingizia kwamba wana kikundi cha ngoma sijui.. wakatengeneza event ya kuwakutanisha na wakapewa ruhusa mashuleni, kumbe huko wakaenda kujiorganise na kuwaambia vijana wao huko mashuleni wasome vipindi gani kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kushika nchi huko kwao..
Na kweli ndivo ilivo kuwa wengi wakaacha masomo ya sayansi japo walikuwa nauwezo sana wakachukua masomo ya arts, kwa mkakati mahsusi wa kwamba baada ya kuchukua nchi wanaenda kufanya kazi fulani!
There after, kwenye myaka ya 2000 nilibahatika kuonana na jamaa mmoja alinishuhudia ukweli wa mipango yao, kwamba kweli walirudi kwao na kweli walishika hizo nyadhifa. Sipendi kwenda ndani zaidi mkuu, lakini ni ukweli mtupu, hawa jamaa wako well coordinated na determined!
Na niwabaguzi wa kufa, Yaani wadada wao ni warembo sana, lakini ukimuoa, kaa tayari hata kaa azae nawewe, atakuja mgeni hapo kwenu atadaiwa ni binamu/kaka/mjomba huyo ndo atakuzalishia watoto wenye pua ndefu utakao walea ukidhani wa kwako! na atahakikisha unasaidia kila jamaa mwenye pua ndefu atakaye kutana naye popote akidai ni 'mwenewachu' Ndugu yangu.
Well pengine si vyema kusema haya but ndo ukweli.
Lazima tukubali ukweli Ulimwengu ni mtanzania pure just ana asili ya Burundi/Rwanda.Kama alikuwa anapata pesa na support toka kwa Kagame kulikuwa na ugumu gani kukimbilia huko na kuishi maisha ya raha mustarehe???kwa nini alikubali kuomba tena uraia na kujaza mikaratasi kibao wakati alikuwa na short cut ya kupata post nzuri sana na pesa bweleleee??Huyu ni mtanzania mwenzetu tuache propaganda za kizushi...wangapi ni wandereko,wanyamwezi,wasukuma,wachaga n.k na bado ni mafisadi kupindukia???UTANZANIA /UZALENDO SIO KABILA WALA RANGI.......ni uchungu wa nchi yako thats it.No matter asili yako or where u r coming from.Tuache huu ujinga wa ukabila/rangi..Hautusaidii.
Lazima tukubali ukweli Ulimwengu ni mtanzania pure just ana asili ya Burundi/Rwanda.Kama alikuwa anapata pesa na support toka kwa Kagame kulikuwa na ugumu gani kukimbilia huko na kuishi maisha ya raha mustarehe???kwa nini alikubali kuomba tena uraia na kujaza mikaratasi kibao wakati alikuwa na short cut ya kupata post nzuri sana na pesa bweleleee??Huyu ni mtanzania mwenzetu tuache propaganda za kizushi...wangapi ni wandereko,wanyamwezi,wasukuma,wachaga n.k na bado ni mafisadi kupindukia???UTANZANIA /UZALENDO SIO KABILA WALA RANGI.......ni uchungu wa nchi yako thats it.No matter asili yako or where u r coming from.Tuache huu ujinga wa ukabila/rangi..Hautusaidii.
Ulimwengu awamu ya nne aliianza kwa kuisifia sanaaa..aliwahi kumtaja muungwana (JK) kwenye mkutano mmoja kuwa ni raisi wa kwanza bongo kukemeaa rushwaa hadharaniii...wakati mwalimu aliwahi kumchapa viboko waziri wake hadharani..lol..Jamaa si tayari kasema kasikia mara mbili tatu kutoka kwa wakuu mtaani na akaileta hapa ili wenye data wamwage. Sasa mbona unataka kumsakama bila kosa au kosa lake hapa ni nini???? Au Ulimwengu kwenye awamu ya nne haguswi?????????????
Joka Kuu,jina halisi la ulimwengu ni Bwana Twaha Khalfan.Jina la Jenerali Ulimwengu alilichukua ukubwani kwa sababu enzi za ujana wake ndo kulikuwa na vuguvugu la mapinduzi Afrika na yeye alikuwa ni mwanaharakati.Kumbuka siku ya uhuru Desemba,09,1961 wakati bendera ya Tanganyika inapandishwa mjini Bukoba Ulimwengu ndiye aliyesoma utenzi wa Uhuru,upo hapo?..inasemekana Jenerali alikuwa kwenye timu ya Kikwete wakati wa kampeni za Uraisi za 95.
..baada ya Mkapa kushinda Jenerali akahamia kambi ya ushindi ya Mkapa.
..baada ya Mkapa kuingia Ikulu, akaanza kumzawadia Jenerali kwa kumteua mjumbe ktk Tume mbalimbali zilizokuwa na ulaji mzuri kwelikweli.
..wananchi wakaanza kulalamika kulikoni Jenerali ateuliwe kwenye kila Tume ya Raisi?
..Mkapa kwa kusikiliza malalamiko hayo akaacha kumpa ulaji Jenerali.
..wakati huohuo Mkapa akaanza kucheza dili za ulaji yeye mwenyewe na washirika wake wengine.
..Jenerali akaamua kumlipizia kisasi Mkapa kwa kuanza kumshambulia kwenye magazeti yake.
..Mkapa naye akachukia akiona kwamba Jenerali hana shukurani kwa ulaji wote aliokuwa akimpa. kwa hiyo Mkapa akaamua kumlipua Jenerali ktk masuala yake ya uraia.
NB:
..kwa upande mwingine Jenerali Ulimwengu ni nani?
..hili jina halina tofauti na majina tunayotumia hapa Jamii Forums. inashangaza kidogo.
..amezaliwa wapi, amesomea wapi?
..amefanya kazi gani tangu amalize shule na ktk taasisi zipi?
Just for the purpose of putting straight Jenerali's record naomba nimkosoe Mzee wa Mbuyu katika thread yake kwa hoja aliyojenga ili kuthibitisha uswahiba wa Jenerali na Mzee Mkapa. Mzee wa Mbuyu amesema Mzee Mkapa alikuwa MC katika harusi ya mtoto wa Ulimwengu,hii si kweli,Ulimwengu hajawahi kuozesha mtoto,binti yake mkubwa Sibongile alitangulia mbele ya haki kabla hajaolewa na ana vijana wengine wadogo tu. Kama ni kumsema tumseme mengine lakini sio hili.Kuhusu kunyang'anywa uraia siku hiyo walinyang'anywa watu wanne akiwemo Castico,Bandora,Jenerali na jamaa mmoja alikuwa CCM chairman Kagera.Tujiulize nini kisa hasa cha kuwanyang'anya uraia kwa pamoja na baadae kuwarejeshea uraia huo?Pili tujiulize ni viongozi wangapi nchi hii ambao wanajulikana kabisa kwamba kwamba asili yao si Tanzania na kwa mujibu wa sheria hawajahi kukana uraia wa nchi zao za asili na ni viongozi wakubwa nchi hii mbona hawaguswi au Mzee mzima Mkapa alikuwa hawajui? Wadau mnadhani Kambarage angekuwa hai Mkapa angethubutu kumnyang'anya Jenerali uraia?