Naipenda CCM ya kibepari ya kina Kikwete na Nauchukia Ukomunisti wa Serikali ya awamu ya tano

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,989
4,129
Vita kubwa iliyopo sasa hivi ni CCM ya ki Capitalisti dhidi ya Ukomunisti wa kina Yohana Mbatizaji anayetubatiza kwa moto.

JK alikuwa anahakikisha wananchi wanakuwa na mitaji ya kufanya mambo, PESA ilikuwepo inazunguka si serikali wala mtaani, nchi ilichangamka. Ndivyo mzee wa fursa Ben Mkapa alisababisha kila mtu atafute mtaji kwa namna yoyote masikini walitengenezewa miundo mbinu ya kujiletea maendeleo, kama ni wakulima walijengewa mabwawa ili wafanye umwagiliaji kupitia miradi ya TASAF.

Huyu wa leo ni mkomunisti, yeye muda wote ni kulalamika kuwa watu wameiba sana pesa, nchi imechezewa sana.

Kaamua kuchukua pesa zote, yaani anatamani hata maduka na viwanda vyote viwe vya serikali, anataka kufufua viwanda vilivyoendeshwa kwa hasara ambavyo Mkapa alivibinafsisha. Pesa za serikali amezipeleka BOT ili bank zifilisike, bank sasa zinahangaika kukopesha watumishi na wanajeshi.

Badala ya serikali kukusanya kodi imeamua nayo ifanye biashara, hadi leo hatujaambiwa reli inaletaje faida kila siku TRC ni hasara bado kaamua kujenga reli ili tufilisike kabisa tubaki tuna tazamana kila mtu akifilisika.

Ndege hivyo hivyo, watu kazi zimewashinda lakini wao wameona pesa zililiwa huko, kanunua ndege zake kwa matrilioni, makusanyo ya ndege tunaambiwa ni vibilioni tu, je uwekezaji utarudi lini hatupewi hesabu ya mapato na matumizi ya ndege zetu, kwani si tumenunua kwa kodi zetu!!

Hawa jamaa wanaosapoti Ujamaa wanataka tufilisike kabisa, binadamu asili yake ni kuwa capitalisti, hata Mungu ni Mkapitalisti ndo maana alisema asiyefanya kazi na asile, halafu akasema wanyonge hawataingia mbinguni.

Huyu wa leo anataka, wengi waitegemee serikali hata shule watoto watasomeshwa na serikali, utaweza kusomesha bure, unajibana na kuumiza kichwa, kumbe ungerudisha ada usingepata ma stress. Yaani wengine wabanwe kulipa kodi ili wasomeshe watoto wa wavivu wasio na pesa, Bahili anajibana anakuwa na mtaji.

Mwingine kazi yake kula pombe mtoto wake anasomeshwa bure, hii sio fair kabisa. Kila mtu akomae kufanya kazi, ndo maana anawatetea wanyonge ambao hata Mungu hawataki, "mimi ni raisi wa wanyonge" Mungu hawapendi hawa wanyonge. Mtu anatakiwa agangamale, hao walemavu tukiwa na nguvu wote tunawasaidia.

Ndo maana wajinga kila kukicha wanapandishwa kwenye mabasi kupelekwa mikutanoni bure, huko wanalishwa na mwishoni wanapewa nguo, tshirt na kofia za kijani na njano.

Huo ndo ukomunisti, serikali inataka kila kitu ifanye yenyewe, yaani kama China vile, watu ni masikini, serikali ndo yenye mapesa, hiyo ni kutaka control tu hamna chochote cha maana.

Ndio maana naiombea China ifilisike ili duniani tupate serikali nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom