Ulimpataje mwenza/mchumba/mpenzi wako?

Ulimpataje mwenza/mchumba/mpenzi wako?

Me nilikutana na my sweeee wangu...... Kwenye Bus Tulikuwa tunatoka Dodoma kwenda Mwanza...
 
Hii siredi jamani, mimi kuwa serious kwenye mapenzi wa kwanza nilikutana nae chuo, nilikuwa napenda sana story akamaindi nikakaa nae sana tu, nikaja pata mchepuko nilikutana nae nyumba moja hivi ilikuwa sikukuu full ucheshi nikamvizia nikapata no yake wiki nyingi mtoto akasafiri kunifuata nikakaa nae zaidi ya mwaka kama mchepuko kwenye mahusiano, nikapata mchepuko wa 3 ndani ya mchepuko, huyu nilipewa namba tu juu kwa juu na mwana, nikaanza mzingua full kumjali na ucheshi nikaenda kukutana nae nikala mzigo, du akawafunika wenzake wote, nikavurugwa basi nikaamua kuachana na wale wawili na mpaka sasa yupo yeye tu na yeye pia tumemaliza mwaka kwenye mahusiano, tupo kwenye mipango ya ndoa na kwa uweza wa Mungu tutafanikiwa, maana tupo hatua nzuri ndugu na wazazi pande zote wanafahamu uhusiano wetu. AMEIN.
 
Bi MkubwaTukiishi pamoja mtaani nae alikuwa akionekana mshamba kwa kuwa akibaki kwao muda wote. Vijana hawakushughulika nae na mimi nilipojizoesha kwake ikawa mimi ndio mimi tu, hivyo niliamua ndowa kabla ya uharibifu.
Bi Mdogo jee! Nilikuwa failure wa Form 4 na katika jitihada yangu ya kujiendeleza nikagongana na failure mwenzangu katika jitihada zetu za kujiendeleza. Baada ya muda jitihada zetu zilizaa matunda kielimu na urafiki uliojengeka ulisababisha ndowa halali ya pili.
 
Ni story nzuri kwa kweli hapo ndio utaona njembas wanavyotumia strategies mbali mbali katika kumnasa mrembo, huyu ile bank card ndio ilikuwa chanzo cha yeye kujipatia mke bora.

Yaaani ameniwowa Mke wa pili na mimba juu hahaha...ila honestly stori imenigusa haswaa
 
BAK, naona umekuwa mshehereshaji mzuri wa mada lakini sijaona ukitupia uzoefu wako jinsi ulivyompata shemeji..!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
LoL!!!! Hahahahaha unajua nilishawahi kufunguka hapa kuhusu hili lakini kiaina nami kujiweka kama third party 🙂🙂 nikahisi watu watanistukia lakini hakuna aliyestuka 🙂🙂 wala sitautaja huo uzi ulihusu mada ipi maana wafunyukuzi wataingia kazini lol!! Labda iko siku nitafunguka kuhusu hili tena directly badala ya kuwa third party.

BAK, naona umekuwa mshehereshaji mzuri wa mada lakini sijaona ukitupia uzoefu wako jinsi ulivyompata shemeji..!
 
tulikutanishwa na rafiki kipenzi,thank you girlfriend/wifi kwa kunipatia mume
 
Mkuu Eli79 funguka basi nawe Mkuu kuhusu mada hii, huwezi jua labda unaweza kunihamasisha 🙂🙂
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Eli79 funguka basi nawe Mkuu kuhusu mada hii, huwezi jua labda unaweza kunihamasisha 🙂🙂

hahaahaa...mkuu, ngoja kidogo nijipange..!
story yangu inaihusu sana jf, kila kitu kilianzia hapa.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mi nilikuwa Tabora pale CRDB kama bank officer na nilikuwa nakaimu nafasi ya MPB so hamna mtu atapata tembocard bila kupitia kwangu. Mwaka huo 2006 tunaenda saba akatokea mmasai binti mrembo balaa daah. Kaja kwangu kupiga picha ya tembocard nikapagawa. Wiki mbili baadae kadi zikaja take nikaificha so nikamwambia anipe namba ya cm I'll nikiipat basi nimpigie aje chukka. Haaa nikaanza msg za mapenzi kawa ananitukana balaa.

Basi nikaone yote heri. Nikampigia day moja, mama eehh kadi imekuja njoo uchukue. Ile kaja nikampa kadi yake lakini password paper nikampa ya mtu mwingine. Akashindwa kuaccess account through ATM. Kaja alalamika huyo kidume namuwinda tuuu. Nikampiga picha ingine, mama eehh hoi kadi imekosewa namba ntakupigia kila baada ya muda kukupa update. Kaniona msamaria kumbe nawinda. Sasa si wawajua wasichana wa pale uhaziri tabora wale warembo hupenda kuheshimiwa na ukubwa ilhali account zao ziko hoi.

Basi kawa aona aibu kuja counter kuchukua pesa na kama akija antaka mie tu. Siku alobugi kaja kutoa elfu hamsini kaandika vocha mie kanipa nikaona muda huuhuu. Nikatoa wallet nkampa pesa hiyo mama nenda siku ingine utanilipa Niko bize ati. Kaona kanpata kumbe hajui. Basi nikawa nunda mama eehh nope hela yangu Nate huyu mwanafunzi hana basi ikawa tarehe baada ya tarehe.

Kaja kustuka msg za luvluv kibao azijibu mara kaamkia nyumbani kwangu shaharibu hivyo. Leo ndo mke wangu Ana mtoto 6 yes na mwingine yuko tumboni aja ila roho yaniuma mie hajanilipa hata leo.

Watoto sita?? Duh
 
Matege njoo useme nimekupatia wapi
 
Last edited by a moderator:
Wadau,
"Ka jioni hivi, nipo kando ya mto nachunga mbuzi 16 wa home kando ya mto. Sasa pale mtoni kuna sehemu ya wasichana na sehemu ya wavulana. Ktk mbuzi wale nakumbuka kuna beberu moja sumbufu likakurupuka toka kundini nikaanza kulifukuza. Katika makona kona likatokezea upande waogao akina dada, hapo ndipo nilipagawa! Niliwakuta wadada watatu wanaoga mmoja mkubwa wa rika langu wengine vitoto tu. Basi yule mkubwa akakimbilia nguo fasta, akajifunga kanga. Nilimuomba samahani sana japo alinitusi kwa hasira. Mi niliendelea kumfukuza mbuzi huku image ya yule dada ikijirudia kichwani mpaka usiku sikulala vzr!
Baada ya mwezi nilikutana nae sokoni, looh si alinikumbuka! Kuanzia hapo ndo nikaanza kufukuzia kwa bidii maana hakika moyo wangu uligala gala kabisaaa kwake....! Mpaka naandika, sasa ni mama watoto wangu.

Mwana JF hasa hapa MMU, tushirikishane namna tulivyowapa wapenzi wetu. Karibuni....

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Mi nilimpata kwenye daladala
 
Hii siredi jamani, mimi kuwa serious kwenye mapenzi wa kwanza nilikutana nae chuo, nilikuwa napenda sana story akamaindi nikakaa nae sana tu, nikaja pata mchepuko nilikutana nae nyumba moja hivi ilikuwa sikukuu full ucheshi nikamvizia nikapata no yake wiki nyingi mtoto akasafiri kunifuata nikakaa nae zaidi ya mwaka kama mchepuko kwenye mahusiano, nikapata mchepuko wa 3 ndani ya mchepuko, huyu nilipewa namba tu juu kwa juu na mwana, nikaanza mzingua full kumjali na ucheshi nikaenda kukutana nae nikala mzigo, du akawafunika wenzake wote, nikavurugwa basi nikaamua kuachana na wale wawili na mpaka sasa yupo yeye tu na yeye pia tumemaliza mwaka kwenye mahusiano, tupo kwenye mipango ya ndoa na kwa uweza wa Mungu tutafanikiwa, maana tupo hatua nzuri ndugu na wazazi pande zote wanafahamu uhusiano wetu. AMEIN.

aisee wewe ni komesha... salute mkuu maana kwa kuchepuka una kacheti nadhani
 
Back
Top Bottom