Ulimpataje mwenza/mchumba/mpenzi wako?

Ulimpataje mwenza/mchumba/mpenzi wako?

Huu uzi tuutumie vizuri kuwatambua wake/waume za watu ili kuepuka usumbufu kule pm.

Umefikiria kwa busara japo wengine wataona ka unawazibia riziki. Asante kwa ushauri mzuri.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Jamani, ambao hawajapata machaguo yao, angalieni na jifunzeni tulivyowapata wenzi wetu na nyie mpate ka uzoefu hapa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Walikuwa ni wadada wawili wote tukiwa chuo, mmoja ndiye alikuwa amenizimikia zaidi kuliko mwenzake basi kwa kuwa walikuwa wanaishi bweni moja basi kila mara baada ya masomo walikuwa wanakuja kunifuata mimi ndio niwasindikize hata kama walikuwa wanajisomea na vijana wengine na yule aliyenionyesha kunipenda sana ndiye alikuwa kinara.Sikutambua yule mwingine ndiye alikuwa ananipenda zaidi ila haonyeshi.Kwa kuwa walisema simba mwenda pole ndio mla nyama na siku zote Mke mwema hutoka kwa Mungu basi mda ule natafakari kumtamkia mdada aliyenionyesha ishara ghafla akatokea rafiki yangu akaniambia anamhitaji yule mdada basi kwa kuwa sikuwa mzoefu basi nikahitaji mdada mwenyewe either aonyeshe hamtaki ndio niendelee na msimamo wangu.Kwa kuwa yule binti mwingine alikuwa ni mtoto wa mjini na alikuwa amesoma Jitegemee si akampiga mwenzake counter attack, kuja kushtuka nimeisha mvisha pete ya uchumba simba mwenda pole na ndiyo mama watoto wangu.Yule mwingine kwa hasira akamwaga rafiki yangu na yule mdada ananichukia mpaka leo.Ujumbe kwa wadada kama unampenda kijana na ghafla akatokea yule usiyemhitaji weka msimamo wako mapema maana vijana wengi wastaarabu huwa hawapendi kuchumbia msichana alie na mtu.Yule niliyemuoa ulikuwa ni mpango wa Mungu.
 
Hongera sana! Always hidden future has many answers!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hahahahahaha lol!!!!! ulimtongozaje wakati mrembo alikuwa bwiiiii? Dah!!! 🙂🙂🙂
Nilimsindikiza mpaka kwake then nikaanza kumpigia misele siku zilizofuata mpk kikaeleweka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Dahh umenikumbusha mbali kweeelii...Kuoga mtoni...:smile:

Dah wangu yupi hata sijui nikuambie, Wa kwanza au wa mwisho ?

Wadau,
"Ka jioni hivi, nipo kando ya mto nachunga mbuzi 16 wa home kando ya mto. Sasa pale mtoni kuna sehemu ya wasichana na sehemu ya wavulana. Ktk mbuzi wale nakumbuka kuna beberu moja sumbufu likakurupuka toka kundini nikaanza kulifukuza. Katika makona kona likatokezea upande waogao akina dada, hapo ndipo nilipagawa! Niliwakuta wadada watatu wanaoga mmoja mkubwa wa rika langu wengine vitoto tu. Basi yule mkubwa akakimbilia nguo fasta, akajifunga kanga. Nilimuomba samahani sana japo alinitusi kwa hasira. Mi niliendelea kumfukuza mbuzi huku image ya yule dada ikijirudia kichwani mpaka usiku sikulala vzr!
Baada ya mwezi nilikutana nae sokoni, looh si alinikumbuka! Kuanzia hapo ndo nikaanza kufukuzia kwa bidii maana hakika moyo wangu uligala gala kabisaaa kwake....! Mpaka naandika, sasa ni mama watoto wangu.

Mwana JF hasa hapa MMU, tushirikishane namna tulivyowapa wapenzi wetu. Karibuni....

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Naipenda JF, kuna mke na mume nawajua hapa, mke kaelezea alivompata mume tofauti na mume alivoelezea namna alivompata mke! Cha msingi ni wanandoa, nawatakia kila la kheri ktk ndoa yenu!
 
Dahh umenikumbusha mbali kweeelii...Kuoga mtoni...:smile:

Dah wangu yupi hata sijui nikuambie, Wa kwanza au wa mwisho ?
Niambie wote nijue uliwapataje, mi cnimemtaja wangu lakini?
Nakusubiria illuh

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Dahh umenikumbusha mbali kweeelii...Kuoga mtoni...:smile:

Dah wangu yupi hata sijui nikuambie, Wa kwanza au wa mwisho ?
Halafu kuna ka raha fulani kuoga mtoni! Mbaya zaidi pawe na njia watu wanakatia! Loooh, waweza kuvaa na sabuni mwilini.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Naipenda JF, kuna mke na mume nawajua hapa, mke kaelezea alivompata mume tofauti na mume alivoelezea namna alivompata mke! Cha msingi ni wanandoa, nawatakia kila la kheri ktk ndoa yenu!
Ha ha haaaaa! Hebu wataje waumbuke!

Back
Top Bottom