Tulikutana chini ya muembe ktk harakati zetu sijui tulikosea wapi kumbe bhana ktk ule muembe kulikuwa na nyuki wale aina ya nyigu!,wanaviuno mbonyeo Kama wana nyodonyodo!. Tulitegemea ule ndo ungekuwa mwanzo wa mapenzi yetu lkn ndo ulikuwa mwisho si kwa shughuli ile waliyotutendea nyigu wale!. Sikuwahi kumuona tena dada wa watu namimi sijui kwanini niliwategea kisogo changu wale nyigu! Maana walintranslate toka kuwa kisogo mpk kuwa usogo!!. Anyway nachokumbuka yeboyebo moja nilikuta imefika magotini nyengine niliiacha eneo la tukio.