Ulimpata vipi huyo uliyenaye sasa?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Wasalam,

Nadhani nainze kutirirka mimi mwenyewe

Nadhaani katika wale wanawake ambao wanaongelewa kwamba Laiti mwanamke mwenziye angelimwona basi nayeye angelitamani awe mwanaume ili apate japo kupata machache kati ya yale mengi wanaume wayahisiyo popote pale wanapobahatika kumwona msichana mzuri na mrembo

Uzuri usiomithilika na haiba ya pekee ya kike Laiti kama ,ule usemi wa kumsadifu mwanamke kwa kumfananisha na malaika ungelikuwa ni yakini ..basi Wallah mwanamke yule angekuwa mmoja wa wanaadamu ambao walikuja katika mgongo wa ardhi ya sayari ya Maji (Dunia) kwa bahati mbaya . Alipaswa kuwa malaika lakini haikuwa hivyo.

Ilikuwa ni mwanzo mwanzo, wa makutano yetu mimi na bibie yule
ilikuwa hafla fupi Nyumbani kwao ya dada yake , nami nilikwenda pale kumpa kampani dada yangu ambaye ndiye rafiki wa mwali wa hafla hiyo na yule bibie ni mdogo wa huyo mwanamwali

Yaani dada wa yule binti ndiye mwali wa kajisherehe hako na dada yangu mimi ndiye rafiki mualikwa wa mwali...hapa nadhani tumeenda sawa, kwao sikuwajua kabla ilikuwa mara yangu ya kwanza kwa mapenzi yake mwenyezingu nikabahatikwa kuwa mmoja wao..ilikuwa ni moja kati ya mitaa fulani huko zanzibar.

Tulijongea katika viunga vya nyumba yao mishale ya 2 kasoro usiku, haikuwa hafla ya watu wengi kama ilivyo miiko na desturi za ukanda ule vijihafla na vijisheherehe vya mtindo huo nadhani ndiyo sababu kubwa ya hafla hiyo kuudhuriwa na watu wachache tu yaani ndugu na marafiki, hapo kama tutaitoa ile sababu ya familia hii kumiliki vijisenti , vinavyowawezesha kupitia sheli muda wowote watakohitaji kwenda popote kwenye umbali kutoka kwenye makazi yao ...sio mi niliyezoea kudanda kwenye vijidalala vya umma mkono juu , siku nikijitahidi sana basi nimetumia UBER.

Baada ya kuwasili pale binti yule ndiye , alitulaki na kutukuribisha uzuri muda wote alikuwa katika condition niipendayo kila nikimtamzama mwanamke usoni, nyie huwa mnaita TABASAMU, Palikuwa na maongezi machache kati yake na dada kisha, dada yangu akachepuka upande wa jikoni kusaidizana na wenzie katika maandalizi ya maakuli na katika muda huo mchache wa maongezi yao usiozidi dakika hata 3,

Fisi mie Nlishatazama baadhi bibie yule na vitu vichache nlivyotamani kuviona basi nikaviona mwanya huu wa kumtazama ulitokana na yeye kujitanda kama ipasavyo na ifaavyo kwa wadada wa ukanda wa mwambao Lakini si katika mpangilio maalumu, viungo

Labda nimtetee pengine joto la jikoni lilimfanya hata vilemba na shungi zake ziwe zimeegeshwa huku kijijasho cha mbali kikimtiririka alivalia Abaya ndefu na nyepesi alikuwa ,si mrefu sana,wala si mfupi, mwenye weupe wa ule wa kihabeishia, nlimskiliza muda wote alikuwa mtaalamu wa rafudhi ya kimwambao na sauti yake nyembemba ya kati si ya kukwangua wala nyembamba sana. Sikubandua macho yangu Kwake.

Hapa pepo na shetani wa shari ya tamaa alishahama kwenye medula oblangata anakojifichaga muda wote na kuhamia katika ubongo wa mbele, yule malaika wangu wa upendo wa dhati sijui, mtulivu aliniacha nyuma... wakati huu, tamaa za malaya kuona pesa zisingefikia uchu wa hali ya juu.

Wakati wangu wa kubaki na yeye uliwadia wakati akiniongoza ambako nlipaswa kukaa na ndiko wanaume wenzangu walikokuwa wameketi,.
Muda wote alichangamka na kutabasamu,

Nami nikamshika mkono na nikapata wasaa wa kurejesha tabasamu
Huwa nafahamu uwezo wa tabasamu langu kwa wasichana , Da Vinci XV mimi huwa nahisi kitu kama hasira kuona halina athari zozote katika fikra wala sura ya msichana.

Bibie yule Hakulabadilika ila alishtuka.,na hata tabasamu lilimpotea. nadhani hakupendezwa na kitendo changu cha kumshika mkono na kumsimamisha nikimtazama.

Akarejelea jikoni kuendelea na mambo yake ,
Naam huyu binti alikuwa mashaallah hakuwa na hatua za kukata wala za pupa , nliendelea kumtazama umbo linalovutia japo lilikuwa ndani ya Abaya nyepesi.lskini baado kitabu kilisadifu yaliyomo.

Nadhani nlikuwa nmekosea sana kudhani kuwa mimi peke yangu ndiye nilikuwa nikimtazama msichana yule mzuri, nlijihakikishia hilo baada ya binti huyo kupotea machoni mwangu na kuingia korido iliyokuwa inaelekea jikoni, macho ya wanaume yote yalikuwa yameelekea upande huo

Nisingewalaumu mwanaume yoyote ambaye angekutana na binti yule hata barabarani ingekuwa Faradhi kumkodolea macho ,ingawa muda wote yu katika mavazi yake marefu.

Hafla iliendelea kwa mambo kadhaa wa kadhaa,itifaki ikizingatiwa na mitaradadi ikaitaradidiwa.

Ukafika muda wa kupata Msosi,

Nami kwa asilimia 100, nlitamani ile sahani ya madiko niliyopatiwa basi chakula chote kiwe na yule bidada,
Hapa nlisahau hata dada yangu alikwenda kusaidia....ningekumbuka vipi na ubongo wangu muda huu ulishaingia katika mitihani ya shetani na matamanio ya nafsii.

Wakati huu nlimwaona yule bibie akijishugulisha kugawa chakula na vinywaji kwa wale waalikwa wachache waliokuwa pale.
Nilitamani asogee upande huu ambao nami nilikuwa nmekaa lakini hilo nalo halikufanyika.

Nikajikuta nikitamani binti huyo anitazame ili nimkonyeze. Kwa bahati mbaya, hilo nalo pia halikutokea.

Wakati naendelea kujipatia diko langu , utamu wa chakula kile kama ilivyo desturii ya watu wa pwani na ladha ya Chakula..akili yangu ikakubali ni yeye pekee ndiye aliyepika.

Mpishi yule nlitamani kumsalima au kutamana naye tena au hata stori mbili tatu lakini ningewezaje kujifaraguza katika hilo.wakati ule.

Basi mambo yalikwenda huku kila muda nikiangaza angaza macho kwa tabasamu pana kwa yule bibie
wakati wote wa shughuli, hadi kutamatika kwake ,
na aliligundua hilo lakini hakujaribu kurejesha tabasamu kama lile la mwanzo wakati tunakaribishwa kule mlangoni na dada yangu.
Haikunistua bali ilinishangaza.

Hatimae wageni walianza kutawanyika, nami nikamfata dada yangu kumuelekeza hali halisi kama ningepata walau wasaa wa kukaa na yule bibie nitete naye mawili matatu, Yaani afanye connection ili niweze kuongea na bidada yule mrembo.

Hakukataa lakini alinisisitiza wazi wazi ugumu wa kumpata yule Bibie, ni ngumu si rahisi kama nidhanivyo mimi.

Hilo halikuwa suala kwangu , nlichohitaji ni ule wasaa au waswahili wanasema Njeo, kama hautopenda kutumia neno Muda au Wakati, ili niweze kuteta naye.

Dada alifanya hivyo.

Ukapita muda kidogo nje ya nyumba yao , ambapo fisi mwenye tamaa nlipokuwa nimesima nikisubiri qdada akiwa na bibie walifika mpaka nlipo , na dada yangu alirejea ndani.

Sikuitamani ile dhambi nyeusi inayoitwa kushindwa ilihali nina uthubutu.

Wakati huu nlisimama na msichana mrembo zaidi kati ya wengi nliowahi kuwaona,

Alinitazama kwa sura ya mkazo na viulizo akisubiri nianzishe mazungumzo. alihisi ameshawahi kuyaskia kwa kile mwanaume aliyewahi msimamisha huko njiani au popote pale.

Nikiri nmewaface na wanawake wengi warembo na wazuri, walionikataa na kunikubali....kwa kuwarubuni na kuwachota

Lakini hapa kwa urembo wa yule bibie nlibaki nimeduwaa , nlitegemea kwa culture yake awe na aibu aibu na ule upuuzi mwingine wa kike unaofariji wanaume., lakini hivyo vyote havikuwepo

Na hapa ndipo nlipoafikiana na akili yangu kuwa kuanza maongezi ya tija na yule Bibie ilihitaji utaalamu.

Na utaalamu siyo jambo ambalo lingepatikana kwa dakika moja.


ITAENDELEA








Ulimpata vipi huyo ulienae sasa hivi, hebu tumegee kidogo
 
Tulikutana chini ya muembe ktk harakati zetu sijui tulikosea wapi kumbe bhana ktk ule muembe kulikuwa na nyuki wale aina ya nyigu!,wanaviuno mbonyeo Kama wana nyodonyodo!. Tulitegemea ule ndo ungekuwa mwanzo wa mapenzi yetu lkn ndo ulikuwa mwisho si kwa shughuli ile waliyotutendea nyigu wale!. Sikuwahi kumuona tena dada wa watu namimi sijui kwanini niliwategea kisogo changu wale nyigu! Maana walintranslate toka kuwa kisogo mpk kuwa usogo!!. Anyway nachokumbuka yeboyebo moja nilikuta imefika magotini nyengine niliiacha eneo la tukio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom