Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Mitandao ya kijamii imekuwa chombo kikuu cha mawasiliano, burudani na hata ajira duniani kote. Hata hivyo, kwa Afrika hususani Tanzania, mitandao hiyo mara nyingi inageuzwa uwanja wa vituko badala ya majukwaa ya kujifunza na kujenga jamii.
Katika siku za hivi karibuni kuna binti anayejulikana kama Mama Amina kwenye mtandao wa TikTok, ambaye amekuwa gumzo kutokana na video zake zinazoibua mjadala mzito.
Mama Amina, ambaye anaonekana kuwa na changamoto za mawasiliano, amejitokeza akiimba nyimbo za singeli. Lakini tofauti na matarajio ya wengi, badala ya kuonyesha kipaji cha muziki, amekuwa akitumia lugha chafu, matusi makubwa na ishara za fedheha mbele ya hadhira yake ya maelfu ya wafuasi.
Katika ukurasa wake wenye zaidi ya followers 88,000, video zake zimekuwa zikishangiliwa, kusambazwa na hata kusababisha baadhi ya wasanii maarufu kuonyesha nia ya kushirikiana naye.
EBU TUJIULIZE KAMA WATANZANIA
je, hii ni burudani au ni taswira ya kusherehesha ujinga? Wakati mamlaka husika zikiendelea kukaa kimya kana kwamba hakuna tatizo, jamii nzima inashuhudia kizazi kinacholelewa kuamini kuwa matusi na fedheha ndizo ngazi za umaarufu.
Ni hatari kuona kwamba badala ya kulinda utu na maadili, mitandao inatumika kuhalalisha tabia zinazoshusha heshima ya jamii. Sasa hivi anakwenda kufanya show kwenye kampeni za Chama cha CCM, akiimba hayo hayo matusi na watu hawana hata tatizo.
Hili sio suala la Mama Amina pekee, bali ni ishara ya kile kinachotokea mitandaoni kila siku. Watu wanatafuta njia ya kupata views na likes, hata kama ni kwa gharama ya hadhi na maadili. Inasikitisha zaidi pale tasnia ya muziki inaposhirikiana na matukio haya badala ya kuyakemea.
MTU MWENYE UGONJWA WA AKILI ANAFURAHISHA SANA KAMA HAJATOKA KWENYE FAMILIA YAKO.