Vitunguu vinachukua muda gani mpaka kuvunwa?
Heshima kwenu ndugu zangu..
Me napenda kuuliza hivi siwezi anza kulima vitunguu kipindi hiki..?
Kuanzia mwezi huu
Vipi Morogoro mikumi/kilosa hali yake huwa vipi kipindi hikiItategemeana na eneo ulilolopo, vitunguu vinachukua miezi 5-6 tangu kusia mbegu kitaluni mpaka kuvuna, hivyo kama utapanda mwezi wa 8 maana yake utavuna mwezi wa 12, sasa hapo itategemea na sehemu uliyopo, kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Kutoka iringa, njombe, ruvuma, mbeya na katavi) miezi hiyo masika huanza, hivyo kama uko maeneo hayo vitunguu vitakuharibikia tu shambani coz ya mvua.
Vipi Morogoro mikumi/kilosa hali yake huwa vipi kipindi hiki
Vipi Morogoro mikumi/kilosa hali yake huwa vipi kipindi hiki
Nashkuru mkuu...sema mm nataka limia mikumi na ndo nataka kuanzaMorogoro kitunguu kinakubali anzia maeneo ya magubike, magole, dakawa, dumila na kilosa pia, kikubwa uhakikishe una maji , mwezi wa 6 after masika kukata ndipo mashamba ya vitunguu huanza kuandaliwa, ili kuvuna november-december
Kama unaanza, anza na mbegu aina ya OPV kama hizo Red cleorel, Red Bombay, ili upate uzoefu kidogo anza hata na nusu eka kwanza, kisha badae ndipo uje utumie hizo hybrid kama Neptune F1 etc, Usije kupanda Jambari F1 zinasumbua sana sokoni maana ni vinene mnoo.
Kama unategemea mvua unasubiri msimu, hila kama unafanya umwagiliaji ni wewe tu kuangalia soko hili upishane na wanaotegemea mvua. Pindi wao wanaingia sokoni wewe ndio upo shamba, wao wakija shamba wewe unaingia sokoni.